Kupangiwa kazi vijijini tayari unakuwa umeuliwa kifikra na kitaaluma

Kupangiwa kazi vijijini tayari unakuwa umeuliwa kifikra na kitaaluma

Aliyekwambia Vijijini Kuna maji machafu nani? Zahanati Kila Kijiji ,umeme upo Barabara zipo shida Iko wapi?

Network ipo unaingia kwenye mitandao Sasa hao wa kuzungukwa si unaamua mwenyewe au?

Hizo stori zilikuwa enzi hizo hakuna hayo niliyokwambia hapo Juu,siku hizi pesa unatoa huko huko rural Kuna mawakala nk.
Hauko serious
 
We shoga kweli, hivi una shughuli kweli ya kufanya mzee? 🤣Au ajira ndo huu uchawa. Sikujua kumbe kuna watu huwa mnanifuatilia kiasi hichi humu 😀😀😀!
Unethical according to jf policy
 
Pia kujiendeleza kitaaluma ni kutafuta umaskini
Mtumishi aliyeko vijijini huko kujiendeleza labda kulima na kufuga huko ila kwenye mambo ya kitaaluma inakuwa ndio mwisho wako.

Huwezi hata kujiendeleza kitaaluma kupitia evening classes maana hakuna vyuo, colleges wala VETA, vyote hivyo asilimia kubwa vipo vijijini.

Kupata ruhusa kwenda kusoma ni kwa mizengwe mingi maana unakuta watumishi wapo wachache.

Wale madaktari wanaotegemea vijiwe baada ya kazi, ukiwa vijijini kwishaaa.

Wewe ndio Daktari pekee zahanati ya kijijini huko, nani atakupa ruhusa ukasome?

NB: Mjini patabaki kuwa mjini tu.
 
Eee nshawahi kuwa mwalimu bana sisee hapakuwa mbali na mjini ila vimbi kha!

Ukisikia mtu ni mwalimu mpe heshima zake mimi yalinishinda.

Sijui mnanielewa ama? Ati wanafunzi wakifunga mimi nibaki maeneo ya shule yaani siwezi kwenda nyumbani kama sina likizo ati nibaki nareport shulen kila siku [emoji1787]

Kubwa kuliko yote nikibaki shulen kumbuka wanafunzi wako likizo shulen nakutana na mbuzi ndo zinakuwa zinazunguka viwanjani nyieeee!

Kuandaa sijui assessment sijui ya mwaka sijui nini dah!
Kunifanyia eti kukaguzi wa kustukiza tena niko darasani, siku hiyo nilimuacha darasani nikawaaga wanafunzi nikawaambia sijiskii vizuri.

Bado kufika kazini ikishafika saa 7:30 kitabu cha kusaini kusharudishwa kwa HM

Vumbi la barabarani nikiwa naenda kazini nyieeee!

Wachawi kulala wananiniga usiku!

Niliandika barua ya kwenda masomoni na ndo ukawa mwisho wa ualimu.

Nyie heshimuni watumishi walioko vijiji hasa walimu dah.
Saiv unajishughulisha na Nini na ulikua mwalimu wa msingi au secondary
 
Katika dunia ya utandawazi kuishi mahali pasipo na umeme wala mtandao kisa kilimo na nyumba za bure zisizo na umeme ni ufala.

Sitakaa eneo la namna hii tena bora kufa masikini.

Wanasiasa wanakula bata kwenye ma-V8 hawakumbuki wenzao wa vijijini eti kisa hata mbuyu ulianza kama mchicha.

Unaweza kuishia kuwa mchicha kiboya

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Nikipata ajira huko ni mwaka tu au miwili nawabwagia kazi yao.

Serikali inachezea sana hatima za watu

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kwa kweli wanachezea, yani watoto wao wakapate exposure ma nchi ya watu afu wewe wamekufungia kijijini usijue chochote chini ya jua kwa ajili ya nyumba walio kupangisha bure.

Zaid unakuta hapo kijijini kupanga nyumba nzima kwa mwezi ni 30k[emoji1544]
 
Kijijini fursa nyingi sana, hasa kwenye sekta ya ardhi, kilimo, ufugaji (ng'ombe wa maziwa, mbuzi...), usafirishaji, uvuvi (kwa baadhi ya maeneo), maji, na viwanda vidogo (kama kufyatua tofali, kutengeneza makochi, kushona nguo...).

Pia kijijini wana jamii wanakuwa na ushirikiano mkubwa sana kwa wataalamu wa afya, jambo linalokupatia faraja kubwa ambayo ina thamani kubwa isiyoweza kupimwa kwa kipato cha pesa.

Kijijini pia unapata muda wa kuwa karibu na familia yako kama unayo.

Kijijini unaweza kupata nyumba ya serikali bure, au ukapata nyumba nzuri kwa gharama nafuu, hivyo kusave something.

In short kijijini fursa ni nyingi kuliko mjini kwa watu wenye mshahara unaolingana, na kwa mwenye akili inachangamka zaidi nje ya your comfort zone kuliko kudumaa mjini na vijiwe (kufanya fani moja pekee).
Hizi za kwako zinaitwa Fursa za kufikirika
 
Eee nshawahi kuwa mwalimu bana sisee hapakuwa mbali na mjini ila vimbi kha!

Ukisikia mtu ni mwalimu mpe heshima zake mimi yalinishinda.

Sijui mnanielewa ama? Ati wanafunzi wakifunga mimi nibaki maeneo ya shule yaani siwezi kwenda nyumbani kama sina likizo ati nibaki nareport shulen kila siku 🤣

Kubwa kuliko yote nikibaki shulen kumbuka wanafunzi wako likizo shulen nakutana na mbuzi ndo zinakuwa zinazunguka viwanjani nyieeee!

Kuandaa sijui assessment sijui ya mwaka sijui nini dah!
Kunifanyia eti kukaguzi wa kustukiza tena niko darasani, siku hiyo nilimuacha darasani nikawaaga wanafunzi nikawaambia sijiskii vizuri.

Bado kufika kazini ikishafika saa 7:30 kitabu cha kusaini kusharudishwa kwa HM

Vumbi la barabarani nikiwa naenda kazini nyieeee!

Wachawi kulala wananiniga usiku!

Niliandika barua ya kwenda masomoni na ndo ukawa mwisho wa ualimu.

Nyie heshimuni watumishi walioko vijiji hasa walimu dah.
Inaonekana wewe ulikuwa mvivu au hukuipenda kazi ya Ualimu.
Vutu unavyolalamikia ulikuwa utaratibu wa kawaida kabisa ila wewe unaona kama vike ulionewa
 
Back
Top Bottom