Kupanuka kwa kundi la BRICS na kuongezeka kwa pato lake la jumla kunaweza kuleta changamoto kwa mataifa ya Magharibi

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1740970598969.png

Kundi la nchi za BRICS linaendelea kupanuka, na likiwa sasa limeongeza nchi washirika mwezi Januari mwaka huu wa 2025, baada ya kuingiza wanachama wapya mwaka jana. Sasa kundi hili lina takriban ya nusu ya idadi ya watu duniani na zaidi ya 41% ya Pato la Taifa (GDP), ambapo limekuwa nguvu ya kiuchumi, yenye wazalishaji wakuu wa bidhaa muhimu kama vile mafuta, gesi, nafaka, nyama na madini.

Wakati huohuo hivi karibuni Russia ilisema mataifa ya BRICS yatavuka nusu ya pato la uchumi wa dunia katika miaka 10 hadi 15. Kauli hii inaashiria mabadiliko makubwa ya kimamlaka ambayo yanaweza kuleta changamoto kwa mataifa ya Magharibi ambayo ndio yanayotawala kwa sasa.

Mataifa ya BRICS hivi sasa yanaendelea kuibuka kwa kasi na kuwa wadau wakuu katika uchumi wa dunia, huku Pato lao la jumla likitarajiwa kuvuka nusu ya pato la uchumi wa dunia ndani ya miaka 10 hadi 15 ijayo.

Makadirio haya yalitolewa na Naibu Waziri Mkuu wa Russia Alexander Novak, wakati alipokuwa akihojiwa na kituo cha Televisheni cha Russia-24. Kiongozi huyo alisisitiza ushawishi unaokua wa kundi la BRICS. Novak alibainisha kuwa BRICS ambayo inajumuisha nchi kubwa zikiwemo China na Brazil, ina uwezo wa kuwa na kiasi kikubwa cha Pato la Taifa duniani, karibu 35%, na kila mwaka kinaendelea kukua.

Kwa mujibu wa mahojiano hayo yaliyochapishwa na tovuti ya BRICS, makadirio haya yanayoleta matumaini kwa nchi hizi yanaonesha ongezeko kubwa la kiuchumi kwenye mataifa ya BRICS ambayo mapato yake yakichanganywa kwa pamoja tayari yanazidi yale ya G7.

Itakumbukwa kwamba BRICS, ambayo mwanzoni ilijumuisha nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini, imepanua uanachama wake kwa kiasi kikubwa mwaka 2024 na kuzijumuisha nchi kama vile Misri, Ethiopia, Iran, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Kujumuishwa kwa mataifa kama vile Saudi Arabia, UAE, na Iran katika BRICS kunabadilisha mpangilio wa uchumi wa dunia na kuipa changamoto G7 ambayo imekuwa ikitawala kwa muda mrefu. Wanachama wa BRICS wanalenga kupanua ushawishi wao wa kiuchumi na katika siasa za kijiografia kwa kurekebisha mifumo ya fedha ya kimataifa na kupunguza utegemezi wa dola ya Marekani.

Upanuzi wa kundi hili sio tu unaimarisha nguvu yake ya pamoja bali pia unaashiria mabadiliko ya mwelekeo wa uchumi duniani kutoka magharibi kwenda Nchi za Kusini. Kwa vile BRICS sasa ina 45% ya idadi ya watu duniani, umuhimu wake kiuchumi na kijiografia utaendelea kuongezeka. Upanuzi huu unaonesha ushawishi unaokua wa BRICS ambao utaleta usawa kwa taasisi za kiuchumi zinazotawaliwa na nchi za Magharibi. Kundi la BRICS linaongeza ushawishi wa nishati duniani, huku nchi za Saudi Arabia na UAE zikiwa wazalishaji wakuu wa mafuta, na kuimarisha uwepo wake wa kijiografia na kisiasa kwa kujumuisha nchi za Mashariki ya Kati na Afrika.

Wanachama hao wapya wanaleta nguvu mbalimbali za kiuchumi, ambapo Iran inaongeza nishati ya kimkakati na uhusiano wa kibiashara, huku Misri na Ethiopia zikiimarisha uwakilishi wa Afrika. Mabadiliko haya yanaonesha dhamira ya BRICS ya kuunda upya usimamizi wa kimataifa kwa kukuza sauti kutoka Nchi za Kusini.

Nchi za Magharibi zina sehemu ndogo tu ya idadi ya jumla ya watu duniani, lakini inatawala taasisi zote za fedha za kimataifa na kufanya sheria za kimataifa ziwe nafuu kwa upande wake. Nguvu hii isiyo na uwiano haikuanza jana au leo, bali ilianza tangu enzi ya ukoloni hata hivyo sasa inakabiliwa na ushindani mkuwa wa ukuaji wa kasi wa uchumi wa nchi zinazoendelea, ambazo sehemu yake ya Pato la Taifa inaendelea kuongezeka.

Nchi za BRICS ziliipita G7 kwa pato la taifa (GDP) linalopimwa kwa kiwango cha uwezo wa kununua (PPP) mwaka 2018. Hadi kufikia 2024, pengo lilikuwa limeongezeka zaidi, BRICS ikichukua 35% ya Pato la Taifa Duniani, ikilinganishwa na la G7 ambalo ni 30%.
 
View attachment 3257036

Mambo ya wasomi hayo...
 
Back
Top Bottom