Kupata fremu za biashara maeneo yenye muingiliano wa watu ni tabu sana

Chakula hakiuziki online?
Nilishakujibu mdada kuwa labda utusaidie ni mitandao gani watanzania huwa wanaagiza chakula online? Tunajua kuwa ukitaka usafiri, zipo Bolt, InDrive, etc, kwamba karibia kona nyingi za Dar unaweza ingia online ukapata usafiri kwa wakati unaouhitaji. Vitu kama nguo, vyombo vya nyumbani etc... kuna WhatsApp, Telegram, FB na mitandao mingine, wafanyabiashara wanajitahidi kutangaza huko. Sasa labda utuambie, nikiwa Kimara nikataka kula let's say Biryani, naingia mtandao upi ninakoweza kupata delivery ya biryani kwa wakati huo ili nile na maisha yaendelee?
Unaweza nisahihisha.
 
Unanionaje mimi hapo kwenye Facebook whatspp ni sio platform za kufanyia biashara ni semu ya kutangazia biashara na watu wengi wanatapeliwa Kisha wanasingizia online business

Ngoja nikupe somo kidogo online platform Kuna vigezo ambavyo unaweza usivijue ukifikiri kila mtu niwakuagiza au kununua mazao Facebook sijui jf hapa Kuna watu wengi lakini sio platform ya online business kwamba tunaweza kufanya biashara mimi niko UK wewe uko njombe ningumu
 
Huh!!! Asante sana kwa somo. Ingawa sina uhakika kama hata ukirudia kusoma ulichoandika mwenyewe unaweza kuelewa. Anyway, asante sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…