Don Gorgon
Member
- Nov 21, 2024
- 35
- 68
Mara nyingi nimeona akina dada wakikataliwa kuhudumiwa katika ofisi za uhamiaji kwakuwa aidha wamevaa nguo zinazoelezwa maafisa kuwa ni fupi au za kubana. Nani anaweka vigezo hivi? Mbona neno uchi tumelikuza hadi kufikia maeneo ambayo hayapaswi kuwa uchi? Kwahiyo Maafisaa wakiona miguu ya akina dada wanashindwa kufanya kazi au ufanisi unapungua?
Huwa likija suala la mavazi Watanzania wengi tunakimbilia kuongelea maadili kana kwamba sisi sote tuna maadili.
Siku moja nimefika ofisi fulani ya Uhamiaji nikakuta walinzi getini wanawarudisha akina dada wawili waliovyaa suruali, tena ambazo hata hazina mbano wa namna ya kuleta “mfadhaiko” kwa afisa wa kiume, kama hiyo ndiyo hoja. Hivi huwa wanawarudisha hata wageni wenye rangi tofauti na nyeusi wanapoenda kushughulikia permits zao au nyaraka nyingine?
Well, huenda nimekengeuka kimaadili kutokuona na kutokuona shida ya mavazi hayo.