DOKEZO Kupata huduma kwenye Ofisi za Uhamiaji kunahusiana nini na mavazi mtu aliyovaa?

DOKEZO Kupata huduma kwenye Ofisi za Uhamiaji kunahusiana nini na mavazi mtu aliyovaa?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Vituo vya polisi huruhusuwi kuingia kama umevaa nguo ya kubana. Utawaona wadada wanavyoangaika kujifunga kanga
 
Ndivyo inavyotakiwa. Hata wasanii wa muziki na maigizo wanaoongoza kuvaa kihuni huwa wanavaa vizuri wanapokuwa mbele ya mkuu wa mkoa su wilaya. Kuvaa nguo kihuni ni kukosa heshima kwa watu usio na mazoea nao.
 
Mara nyingi nimeona akina dada wakikataliwa kuhudumiwa katika ofisi za uhamiaji kwakuwa aidha wamevaa nguo zinazoelezwa maafisa kuwa ni fupi au za kubana. Nani anaweka vigezo hivi? Mbona neno uchi tumelikuza hadi kufikia maeneo ambayo hayapaswi kuwa uchi? Kwahiyo Maafisaa wakiona miguu ya akina dada wanashindwa kufanya kazi au ufanisi unapungua?

Huwa likija suala la mavazi Watanzania wengi tunakimbilia kuongelea maadili kana kwamba sisi sote tuna maadili.

Siku moja nimefika ofisi fulani ya Uhamiaji nikakuta walinzi getini wanawarudisha akina dada wawili waliovyaa suruali, tena ambazo hata hazina mbano wa namna ya kuleta “mfadhaiko” kwa afisa wa kiume, kama hiyo ndiyo hoja. Hivi huwa wanawarudisha hata wageni wenye rangi tofauti na nyeusi wanapoenda kushughulikia permits zao au nyaraka nyingine?

Well, huenda nimekengeuka kimaadili kutokuona na kutokuona shida ya mavazi hayo.
Pale uhamiaji makao makuu siku moja ilinilazimu kwenda kukodi kanzu pale nje posta mpya
 
Wabongo utendaji kazi ni mgumu ndo maana wanafocus na vitu visivyo na msingi , sioni mavazi yakiathiri utendaji kazi wa mtu yeyote !
 
Ni ushamba tu huo ila unaondoka muda unavyozidi kwenda, kwa watu wanaofanya kazi kwenye ofisi zinazojielewa hakuna hizo restrictions za kipumbavu hata kwa staff, mavazi na performance ni vitu ambavyo havitangamani hasa kwa dunia ya leo
basi wawe wanaenda uchi kabisa ili tuzingatie performance tu au vipi?
 
Waendelee kurudishwa mpaka wazichukue suruali sipendi mwanamke anayevaa suruali
 
Nenda siku HOSPITAL LUGALO uone ukivaaJEZI au TRACKSUIT unapelekwa uwanjani ukacheze mpila na kifanya mazoezi ya VIUNGO
HESHIMU maadili yako ya KITANZANIA acha kuigaiga UZUNGU
Kwa hiyo atakaekwenda amevaa uniform ya benk yeyote atapelekwa kuhesabu hela sio?
 
Fuata utaratibu. Kutozingatia taratibu zilizowekwa na wenye mamlaka ni ishara ya upungufu wa maadili, kiburi, na ukosefu wa malezi bora. Kukosa heshima kwa taratibu zilizopo si ujanja wala si usasa.

Kuwa mwangalifu na mzingatifu wa sheria ni kuonyesha ukomavu na heshima na kuonesha kwamba umestaarabika.

"Lawlessness is the mother of disorder." - Aristotle
 
Wakina dada pamoja na masela wanapenda kujaribu hadi visivyo jaribiwa. Pale ni ofisi mbona msikitini hawaendi hivyo na hakuna kelele.
 
Back
Top Bottom