Wanabodi,
Leo tena naendelea na zile Makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa. Topic yangu ya leo ni kutuhusu sisi Watanzania, ili tupate maendeleo ya kweli, ni lazima tujifunze kuupokea na kuubali ukweli halisi, ukweli bayana, hata huo ukweli ukiwa mchungu vipi, ukweli ni ukweli tuu, na siku zote ndio husimama mpaka mwisho. Kauli ya rais wetu Dr. John Pombe Magufuli, kuwa "CCM itatawala Milele " ni kauli ya ukweli kabisa kuwa ni ukweli halisi na ukweli bayana, katika mazingira ya sasa ya nchi yetu na uendeshaji wa siasa za vyama vingi, chini ya katiba hii ya JMT ya mwaka 1977 ambayo ni katiba ya mfumo wa chama kimoja, kama hakuna kitakachobadilika kama kupatikana kwa katiba mpya, na kuunda kwa Tume huru ya Uchaguzi, then rais Magufuli yuko very right kuwa CCM itatawala milele!.
Moja kati ya sifa kubwa za rais Magufuli, ni kusema ukweli Daima tena bila kukopesha, wala kurembaremba, japo kuwa mkweli sana sometimes sio nzuri sana kidiplomasia katika baadhi ya maeneo, ambapo diplomasia hutumika, haya mambo ya diplomasia ndio yametufikisha hapa tulipo, sasa ili tutoke hapa na kusonga mbele kimaendeleo, Watanzania ni lazima tujifunze kuubali ukweli jinsi ile ulivyo, bila kurembwa rembwa, hivyo hili la CCM kutawala milele ni ukweli mtupu ambao lazima tuukubali.
Kuna wengi wanadhani siasa ni kupiga blah blah tuu, hivyo kwao, kila kinachosemwa na wanasiasa, wanakiona kama ni blah blah!, no!. Siasa sio blah blah tuu, japo blah blah zipo, ila pia kuna ukweli bayana, dhahir, shahir!. Siasa ni sayansi, social science, hivyo sayansi ya siasa ni political science, inafuata kanuni zile zile za kisayansi za Newton's laws of motion, ile kanuni ya "a body in motion" or
" a static body", itaendelea kubaki hivyo hivyo milele, hadi kutokea nguvu nyingine itakayoibadilisha, hivyo kwa hali hii ilivyo sasa, CCM is the body in motion, itaendelea kutawala milele, kwa sababu watu wenye uwezo wa Kimungu, wameishaona kuwa kwa Tanzania, hakuna kabisa uwezekano wa kutokea nguvu nyingine ya kuizuia CCM isitawale milele nchi yetu ya Tanzania, hivyo CCM, itatawala milele!.
Japo kila lenye mwanzo, huwa lina mwisho, na CCM kama chama, ina mwanzo hivyo ni lazima nayo iwe na mwisho, unless CCM ndie Mungu mwenyewe, ambaye Yeye ndiye Pekee Alfa na Omega hivyo CCM hii iliyopo sasa nayo ni CCM Alfa na Omega, haina mwisho, hivyo pia katika utawala wa Tanzania, CCM ndio alfa na omega wa siasa zetu, ndicho chama pekee chenye hati miliki ya kuitawala Tanzania milele!, huu ni ukweli bayana ambao lazima sote, tuupokee, tuukubali na tuutekeleze. Wale wote wasioukubali ukweli huu, ni kweli kabisa watapata taabu sana!.
Jee Milele ni Muda Gani?.
Kuna aina mbili za milele, milele ya kwanza ni milele ya kiroho, eternal ambayo inaongozwa na Mungu, na hata sisi binadamu, tutaishi milele, hivyo hapa duniani tuko tuu safarini kuelekea kwenye ama uzima wa milele mbinguni au peponi kwa Mungu kwa watenda wema, au kwenye jehanum ya ziwa la moto wa milele kwa shetani kwa watenda maovu.
Milele ya pili ni life span ya kudumu mpaka mwisho. Hii ni milele ya kidunia, ukizaliwa ukaishi, siku utakapokufa hiyo ndio milele yako na hapo ndipo mwisho wako. Life span zinatofautiana, mtoto akizaliwa na kuishi siku moja, hiyo siku moja, ndio milele yake, na mtu mwingine ukiishi miaka 100, hiyo ndio milele yake, kama ilivyo nyumba, ukizaliwa na kuvikuta vitu fulani, ukaishi navyo mpaka ulipokufa na kuviacha, vitu hivi vitasemwa vimeishi milele. Hivyo kwa wale wote walioishuhudia CCM ikizaliwa, kisha wao ndio wamekufa na kuiacha CCM, kwao CCM imedumu milele. Hivyo hata hawa waliopo sasa, ambao wamezaliwa na kuikuta CCM, na watakufa na kuiacha CCM, kwao CCM ni chama cha milele.
Hizi kauli za CCM kutawala milele, hazikuanza leo, na wala hazikuanza na rais Magufuli.
Hebu tembelea bandiko hili, umsikilize mwana CCM huyu alisema nini na uangalie alisema
lini na alisema wapi!, kwa wavivu wa kufungua links, kauli hii ya CCM kutawala milele, ilitolewa na Mhe. Pinda ndani ya Bunge letu tukufu na hakuna aliyetia neno!.
PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!
Nilidhani Mhe. Pinda amekosea, kumbe mimi ndiye niliyekosea baada ya ukweli huu kuzidi kuthibitishwa na kutamkwa wazi wazi na bayana, itabidi tuu nimtafute Mtoto wa Mkulima, nimuombe msamaha kwa kudhani he was wrong, kumbe mimi ndio I was very wrong.
Humu jf, mtu wa kwanza kusema kuwa CCM itatawala milele ni mwana jf huyu
Je, CCM Itatawala Milele Au?
Na nilipokutana naye, nilifanya nae mahojiano haya.
lini
Watch TBC Live!. " William Malecela na Ndoto ya CCM Kutawala Miaka 50!.
Wenye Matumaini na Upinzani Kushika Dola!, Sahauni! CCM Inajiandaa Kuua Kabisa na Kuuzika Jumla !.
Kuhusu hili la CCM kutawala milele, pia niliwahi kulisema hapa
CCM kutumia Hooks & Crooks Kushinda Chaguzi, Inajua Ikishindwa Ndio Itakufa Jumla, Itakubali?
Katika awamu hii, viongozi wa upinzani walipoamua kujiengua kwenye vyama vyao kujiunga CCM, japo walibezwa, nikasisitiza humu, wasibezwe, wanaona mbali
Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja?
Jee Umilele wa CCM Kutawala Tanzania Milele, Unatokana na Nini?.
Umilele wa CCM kuitawala Tanzania, unatokana na mungu kuiteua CCM na kuipatia hati miliki ya milele kuitawala Tanzania, ndio maana katika baadhi ya makala zangu za nyuma, niliwahi kushauri tuifute ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, tuifute ruzuku kwa vyama vya siasa, Tanzania turejee kuwa nchi ya chama kimoja cha milele, CCM.
Ruzuku kwa vyama vya Siasa: Mnaonaje tumshauri Rais Magufuli aifutilie mbali ruzuku hii? Ni ufisadi
Kidumu Milele Chama Cha Mapinduzi.
Pascal