Mkuu hii ni hatua ya kwanza katika kupata Tina,Yaaani mtu kujigundua Kisha kutafuta msaada.
Maana kihalisia tatizo la akili ni pale kupungua sana au kuongezeka sana kwa yale mambo Ambayo amezoea kuyafanya.mfano kulala sana,kula kidogo au kutopenda kula kabisa, mzigo wa mawazo usio na majibu kwa wakati husika nk.
Hatua ya pili ni utafute mtu ambae unamuamini na UMUELEZEE kwa marefu na mapana yale unayopotia Maishani na kwa namna gani unayaona ni changamoto.
Moja ya gharama unayopaswa kutoa ni muda wako,Acha haraka kabisa utakapoenda kuonana na huyo mtu,itenge ni maalum kwa ajili ya kutafuta msaada,hivyo jiandae kwa hilo.
Kingine ni kuwa muwazi kwa yule utakayeonana nae na akakupa muda wake kukusikiliza,Mwambie vile unajisikia,ulianza lini,yapi yanatokea na nini unatamani kukipata kama suluhisho.
Kwa lolote karibu sana PM