Kupata Mtoto Bila Ndoa: Utamaduni Wetu Unapoteza Mwelekeo?


Kwa Sasa nchi hii Haina kitu kinaitwa ûtamaduni wetu

Kîla mwananchj anautamaduni wake anaoona unamfaa.
Mfano wàpo wanaoishi na Mwanamke au mwanaume na hiyo Kwao NI Ndoa na hawavunji Sheria za Nchi. Unaposema wanafanya vibaya lazima ueleze wanafanya vibaya Kwa misingi Ipi?

Sisi siô Kabila Moja.
Sisi siô damu Moja.
Kûna Makabila zaidi ya Mia ishirini.

Kumbuka hayo Makabila Zamani zilikuwa nchi au mataifa ila walipokuja wazungu ndîo wakaita Makabila .
 
Unaleta hoja kali sana hapa, na unaeleza ukweli ambao mara nyingi tunaupotezea. 🙌 Ukiangalia kwa undani, ni kweli kwamba Tanzania ni mchanganyiko wa tamaduni nyingi – zaidi ya makabila mia mbili, kila moja likiwa na mila, desturi, na maadili yake. Na kama ulivyosema, kabla ya ukoloni, haya makabila yalijiona kama nchi au jamii zinazojitegemea, zikiwa na utaratibu wao. Kwa hiyo, unaposema "utamaduni wetu," inaweza kuwa vigumu kwa watu wote kukubaliana nini hicho "utamaduni wetu" unapaswa kuwa.

Pia, unachosema kuhusu watu kuishi na wapenzi wao bila ndoa rasmi ni kweli – kwao ni uchaguzi wa kimaisha, na hawavunji sheria yoyote. Kwa hiyo, kusema wanafanya vibaya inahitaji sababu inayokubalika kwa misingi mipana, labda ya kidini, ya kisheria, au hata maadili ya familia zao binafsi.

Kwa hali ilivyo sasa, labda hatuwezi kuwa na "utamaduni mmoja" kama zamani. Tunaishi kwenye jamii ya mchanganyiko wa utandawazi, mila za asili, dini mbalimbali, na sheria za kitaifa. Sasa tunachouliza ni kama kizazi hiki kipya kitatengeneza utamaduni wake wenyewe unaowaunganisha – na kama tutauita huu kuwa ni "utamaduni wa Kitanzania." Unaonaje, unadhani jamii inaenda kwenye mwelekeo sahihi au kuna kitu kinapotea? 🤔🌍
 

Jamii Ipo sehemu Sahihi Wakati ujao pakihitajika ulazima wa mabadiliko patabadilika
 
Trust me ndugu wengi wanaoshikilia mambo ya mila na desturi siku ukiwa na shida kwenye ndoa wanakung'ong'a..
Eish, umeongea ukweli mtupu! 😅 Kwenye jamii nyingi, wakiwaona wanandoa wana shida, baadhi yao wanaweza kuwa na mitazamo ya kizamani au kuhukumu bila kuelewa undani wa hali hiyo. Mara nyingi, wanaweza sema "ndoa ni kwa ajili ya maisha yote," lakini wanasahau kuwa ndoa pia inahitaji maelewano, upendo, na msaada wa kisaikolojia ili kudumu.

Hii ni changamoto kubwa – kuna wakati mila na desturi zinakuwa kikwazo badala ya msaada. Kumbuka, kila ndoa ni ya kipekee, na si kila mtu anahitaji "mkono wa mila" ili kuendelea. Je, unadhani jamii inapaswa kubadilika na kuonyesha huruma zaidi kwa watu wanapokuwa na changamoto katika ndoa? 🤔
 
Kama hupendelei ndoa zinazohusiana na waarabu au wazungu kuna ndoa za kimila na bomani hizi zilikuwepo kitambo na bado zipo na serikali inazitambua
Mhimu basi tuone watu wanazaa mtoto wakiwa tayari wanaishi pamoja kuliko mwanamke kuzaa akiwa kwa wazazi wake
 
Ndoa ni concept ambayo ishapitwa na wakati, labda kwa mwanamke inaweza kuwa na umuhimu kwa sababu inalinda masilahi yake na akiitumia ndoa kimkakati inaweza kumtoa kimaisha lakini kwa mwanaume ndoa haina maana tena.

Zile nadharia tulizoaminishwa kwamba ndoa ni pingu za maisha, ni foundation ya familia, ni kiapo cha kuwa pamoja kwenye shida na raha n.k siku hadi siku tunazidi kuona ni uongo mtupu.
 
Kwanza utamaduni ni kitu gani? Standards zake ni nini? Zipo wapi watu waweze kuziona na kuzifuata? Na ukishea references hapa utapanua sana huu mjadala!
Swali zuri sana.

Tatizo kubwa tulionalo weusi ni kwamba hatujatengeneza document ya kutuongoza. Kila siku tunalia lia sana na utamaduni, Mila na desturi ila hatuna reference yoyote ya kwetu tofauti na kutumia reference za kigeni kama biblia na Quran.

Biblia na Quran ni vitabu vya jamii zingine ambazo ziliona umuhimu wa kutengeneza document ya kuwaongoza na ndiyo maana inakua rahisi kwao kufanya reference.


Africa tunaitaji kitabu chetu kwa ajili ya reference ya tamaduni zetu. Tuachane na vitabu vya kigeni vyenye reference zao.

Tutengeneze kitabu chenye tamaduni zetu.

Kwa kuchangia mada, mimi naona ya kuwa mtoto ni mtoto anapaswa kupata stahiki zote anazostahili.

Haya mambo ya mtoto wa nje, mara mtoto Haram, mara mtoto wa ndoa zote hizi ni tamaduni za watu wa nje, siyo tamaduni zetu. Waafrica tunadhamini watoto wote na Kila mtoto ana haki sawa.
 
Kwa hiyo tufanyeje?

Sorry sijasoma hadi mwisho kwa sababu Sina sababu!
 
Kwa watt hawa wanaozaliwa bila ndoa na kupelekea kuwa na idadi kubwa ya single mother tutegeme kuwa na kizazi cha hovyo apo baadae
 
Kama unazungumzia ndoa za kidini huo siyo ustaarabu wetu,si mila zetu,si desturi zetu bali hayo tumeyapokea tu kwa wakoloni, wafanya biashara ya watumwa na mabaharia walio-settle katika maeneo yetu.
Tukirudi kimila kila jamii zilikuwa na taratibu zisizofanana, wengine waliteka tu mabinti wakienda shambani au kuchota maji na kuja kujitambulisha baada ya hapo(huo ni mfano mmojawapo) hivyo taratibu na desturi huwa zinabadilika kutona na factors mbalimbali.
Tusikariri.
 
Kama wanawake hawataendelea kufundwa kama zamani, basi ustawi wa ndoa utabaki kuwa hadithi, na kamwe ndoa hazitakaa zitengamane
 
Kiburi cha fedha na ufeminist kinawapa ujasiri wanawake kujiona wanaweza kulea bila wanaume na kuona mwanaume hana maana.

Kuna vijana wakiume wao wanakazi ya kuwajazia watoto wazazi wao wao huku wao wakiendelea kubwiyanga,kisa babu na bibi wapo.

Tunaishi kwenye jamii isiyojali, haina miiko,wala taratibu kila mtu anaenda kivyake na kimpango wake.Halafu siku hizi wanawake kuzaa na wanaume za watu nayo ishakuwa fashion na hawajali.
 
Aisee, umechambua kweli hapa! 👏 Ni ukweli kabisa kwamba ndoa za kidini na taratibu tunazozijua leo si asili yetu, bali ni matokeo ya mchanganyiko wa historia, dini, na utandawazi ulioletwa na wageni. Kabla ya hapo, jamii nyingi zilikuwa na njia zao maalum za kuanzisha familia na kuendeleza uhusiano, na hizo njia zilikuwa tofauti sana kutoka kabila moja hadi jingine.

Hapo ulipogusia kuwa desturi hubadilika kulingana na mazingira – hiyo ni pointi muhimu sana. Jamii inaendelea kubadilika, na mila haziwezi kusalia pale pale kama zamani. Sasa kinachobakia ni kutafakari: je, tunataka kufuata misingi ya asili ya mila zetu, au tumechagua njia nyingine yenye kuunganisha mila, dini, na utandawazi? Na je, tunapopokea mabadiliko haya, tunazingatia pia faida na changamoto zake? 👀🌍
 
Hujitambui kwa hyo hata ukielekezwa utapinga tu nikuuliźe unaweza kuvua nguo mbele ya mama au baba yako jee unachukua standard zpi za kukataa fikiria
 
Hujitambui kwa hyo hata ukielekezwa utapinga tu nikuuliźe unaweza kuvua nguo mbele ya mama au baba yako jee unachukua standard zpi za kukataa fikiria

Lete standards acha kuleta mistari kama msanii hapa! Kama hujaelewa sema hayo unayosema ni mapokeo na kila mtu anayajua! Kwani ningezaliwa nikakuta hawavai nguo ningevaa?

Wabongo tumepoteza kabisa ufahamu wa kuchambua mambo na kutafakari, tunasahau kwamba maisha ya mwanadamu yanaevolve na kilichokua na maana mwaka 70 kinaweza kuwa kichekesho leo hii, na kwamba mila na desturi zinabadilika na kimsingi zinatakiwa kutafsiriwa na kuwa rasmi kwa kuwekwa kwenye sheria na regulations kila mara ili sasa ziwe mfumo wa maisha unaoenda na wakati! Hili ni gonjwa la kila mtu ndio maana hata sheria tunatumia za muingereza alizotuachia baada ya ukoloni, hatuna maarifa ya kuboresha hata kama tunaona zimepitwa na wakati na tuna watu wanajiita madaktari wa kutosha tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…