Kupata na kukosa. . . KUBALI MATOKEO!

Kupata na kukosa. . . KUBALI MATOKEO!

Dr Lizzy

Platinum Member
Joined
May 25, 2009
Posts
31,009
Reaction score
60,629
Kwenye maisha kuna kupata na kukosa pale tunapotaka, tunapohitaji, au tunapoomba kitu. Muhimu ni kukubaliana na hali halisi.

Linapokuja swala la mahusiano ni jambo la kawaida kijana/mwanaume kumtaka, kumpenda ama kumtamani msichana/mwanamke. Na nikawaida msichana kukubali ama kukataa ombi la mwanaume, kumpenda ama kutompenda.

Binafsi hua nashangazwa sana na wale wasiokua waelewa. Kwamba yeye mdada akimkatalia ombi lake basi anajenga chuki kabisa, wengine hufikia hata kutoa matusi na kashfa za kila aina kisa kaambiwa "HAPANA/HAIWEZEKANI". Wanashindwa kuelewa kwamba kama kila anaeomba angekua anapewa "NDIO" kisa tu kasema anampenda/mhitaji mdada basi wadada wengi wangekua na msururu wa wapenzi wanaowakubalia kwa huruma. Kwamba wanavyolazimisha wao wakubaliwe kwasababu wamependa ndivyo wanavyoweza wakafanya wengine watakaovutiwa na msichana yule yule, je atakubali mwenzake nae akubaliwe ili asiumie?

Mtu akikwambia "hapana haiwezekani" jitahidi kuheshimu maamuzi/matakwa yake. Usijenge chuki wala usianzishe ugomvi. Na ikibidi jaribu wewe kujiweka kwenye viatu vyake na ufikirie "je kama ningekua mimi ningemkubalia kila aliyenitaka/nipenda/nihitaji hata kama hanivutii ama nina mtu wangu mwingine?" Usiwe mbinafsi, kama ambavyo wewe unachagua wa kuwafuata kwa kutumia vigezo vyako binafsi ndivyo ambavyo na wao wana haki ya kuchagua wa kumkubalia kwa vigezo walivyojiwekea wenyewe.
 
Lizzy mama...wanao watakua na mama bora!...Nakutakia akili njema daima...km unaishi katika falsafa zako basi nikiri mume wako hajazaliwa bado...whoever uliyenae na mume wa mtu mwingine!
 
mmmh, Lizzy, unakumbuka taarabu hii
ya zamani kidogo

kukataliwa kubaya mwacheni ababaike2x
Unataka mshikaji kutaka mambo kwa pupa2x
na nguo hizi si zako
na viatu ni vya wizi
 
Lizzy mama...wanao watakua na mama bora!...Nakutakia akili njema daima...km unaishi katika falsafa zako basi nikiri mume wako hajazaliwa bado...whoever uliyenae na mume wa mtu mwingine!
Hhhmm... HA hapo mwisho umeniacha kapa. Unamaanisha kama ninae nimwache kwasababu mimi sio size yake/yeye sio size yangu na nisubirie milele maana hamna anaeniweza/nnaemuweza?
 
please wait while loading...
hili somo nzuri sana kwa online flirterz...
kila la kheli kwa maneno yako bibie lizzy..
 
mmmh, Lizzy, unakumbuka taarabu hii
ya zamani kidogo

kukataliwa kubaya mwacheni ababaike2x
Unataka mshikaji kutaka mambo kwa pupa2x
na nguo hizi si zako
na viatu ni vya wizi
Hahaha sijawahi kuisikia. . . inaitwaje niitafute!!
 
Mimi nakubaliana na wewe kabisa, kuna wanume wanawake chuki wakikataliwa na mwanamke mimi huwa siweki chuki....namtukana afu yanaisha:biggrin:
 
Mimi nakubaliana na wewe kabisa, kuna wanume wanawake chuki wakikataliwa na mwanamke mimi huwa siweki chuki....namtukana afu yanaisha:biggrin:

Hata kumtukana ni ulimbukeni mwingine. Kubali umeshindwa ukajaribu bahati kwingine.
 
Mimi nakubaliana na wewe kabisa, kuna wanume wanawake chuki wakikataliwa na mwanamke mimi huwa siweki chuki....namtukana afu yanaisha:biggrin:

Acha ubibi wewe.....lol!!! Unamtukana ili iweje???
 
Hata kumtukana ni ulimbukeni mwingine. Kubali umeshindwa ukajaribu bahati kwingine.
Lizzy; Kwani namtukana nayeye anasikia...mimi namtukana kimya kimya hata hajui kama nimemtukana na wala hatasikia ....Sisi tunaita technology mpya za matus....Yani data za matusi ( dirty data) tuna baki nazo wenyewe.... :biggrin:
 
..."Kinachoniuma ni kitendo cha kunitangaza kuwa ameniacha wakati mimi ndiyo nimemuacha"

...lol...hayo ndio maneno niliyoyasoma dogo Almasi akilalama kuhusu mlimbwende "Goodness"...
kukataliwa/kuachwa kunauma, ...unahitaji uwe na moyo wa chuma kama mbu hapa ninavyojifariji na "...likuepukalo lina heri nawe!"
 
Acha ubibi wewe.....lol!!! Unamtukana ili iweje???
Njoo basi unavalisha gaguro na sindiria, afu uchukie silaha yangu uizamishe kabisa ndani ya kikapu chako nisi-ione tena.
 
Njoo basi unavalisha gaguro na sindiria, afu uchukie silaha yangu uizamishe kabisa ndani ya kikapu chako nisi-ione tena.

fazaaaaa......mbona umekimbilia kunena kwa lugha as if hujaliona swali jombaaa??
 
fazaaaaa......mbona umekimbilia kunena kwa lugha as if hujaliona swali jombaaa??
Wewe swali lako unuliza kwa kihuni, inabidi tukujibu kihuni kama wewe.

Any way wacha maneno yasio na mana, tusiharibu thread mana hii thread inaongea ukweli mtupu na hapo nampa Lizzy 8.5 points over 10.
 
Hata kumtukana ni ulimbukeni mwingine. Kubali umeshindwa ukajaribu bahati kwingine.
Mwanamke kamili bado ujanijibu kule kwenye thread yako nyingine!!.........otherwise unirudishie asante yangu au uzibe wewe hilo pengo.
 
Nafikiri pia namna unayomuambia mtu ina determine reaction yake....kuna wadada/wakaka wana lugha za kejeli sana....kama una sababu za kutokukubali ombi la fulani,basi fanya hivyo kwa heshima na busara...wengine hadi kijiji kijue alimkataa fulani,au unaanza mkosoa as if yeye hastahili kuwa na mtu kama wewe....Heshima kitu kizuri sana,hakuna duniani anayependa kukataliwa,so lets do it kindly,kama ambavyo ungependa wewe ufanyiwe....ushauri mzuri dearest!
 
Lizzy; Kwani namtukana nayeye anasikia...mimi namtukana kimya kimya hata hajui kama nimemtukana na wala hatasikia ....Sisi tunaita technology mpya za matus....Yani data za matusi ( dirty data) tuna baki nazo wenyewe.... :biggrin:

Kwahiyo ukishantukana kimya kimya unapata unafuu?
...lol...hayo ndio maneno niliyoyasoma dogo Almasi akilalama kuhusu mlimbwende "Goodness"...
kukataliwa/kuachwa kunauma, ...unahitaji uwe na moyo wa chuma kama mbu hapa ninavyojifariji na "...likuepukalo lina heri nawe!"

Hahahahha!
Hao wanaowahigi kutangaza wao ndio wamaecha/badili mawazo/wamemuona binti hafai wakampotezea au hata wameshapata walichotaka ndio wabaya sasa. Maana akitokea mtu akasema "Sio kweli" basi binti wa watu atashushiwa mvua ya matusi weeee!!
 
Mwanamke kamili bado ujanijibu kule kwenye thread yako nyingine!!.........otherwise unirudishie asante yangu au uzibe wewe hilo pengo.
Matola unadhanu mwanamke kamili anapatikana baada ya lisaa?Nipe muda bana. . .
Alafu wewe. . . hehehehehe eti nizibe pengo!Ntaharibu!!
 
Nafikiri pia namna unayomuambia mtu ina determine reaction yake....kuna wadada/wakaka wana lugha za kejeli sana....kama una sababu za kutokukubali ombi la fulani,basi fanya hivyo kwa heshima na busara...wengine hadi kijiji kijue alimkataa fulani,au unaanza mkosoa as if yeye hastahili kuwa na mtu kama wewe....Heshima kitu kizuri sana,hakuna duniani anayependa kukataliwa,so lets do it kindly,kama ambavyo ungependa wewe ufanyiwe....ushauri mzuri dearest!

Dearest kuna wengine hata uwawie wastaarabu vipi watakuchukia tu, kuzushia maneno au kutukana kisa umesema "hapana" na sio "ndio".
 
kibuti kinauma aisee...kama alivyosema mtu hapo juu,akijibu kunya namtukana,akijiheshimu na kunijibu kistaarabu namshukuru
 
Back
Top Bottom