Kupata utajiri siyo suala la bahati, ni sayansi kama zilivyo sayansi nyingine

Kupata utajiri siyo suala la bahati, ni sayansi kama zilivyo sayansi nyingine

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,298
Reaction score
7,612
Kupata utajiri siyo swala la bahati au ujanja ujanja, bali ni sayansi, kama zilivyo sayansi nyingine. Ili moto uwake unahitaji kupata hewa ya oksijeni, hiyo ni sayansi, kadhalika kuna vitu vinahitajika ili mtu uweze kupata utajiri, hiyo pia ni sayansi. Sayansi ina sheria na kanuni zake, ambazo zikifuatwa basi matokeo yanakuja sawa wakati wote.

Hivyo utajiri pia una sheria na kanuni zake, ambazo mtu akizifuata ataweza kupata utajiri bila ya kushindwa. Uzuri wa sayansi ni kwamba hakuna kubahatisha, ukiweka kitu sahihi na utapata matokeo sahihi, ukiweka kitu ambacho siyo sahihi na matokeo yatakuja ambayo siyo sahihi, Kwa wale mliosoma masomo ya sayansi natumai mnanielewa vizuri.

Watu wengi wamekuwa wakifikiri kupata utajiri ni bahati, na hivyo kushiriki michezo ya kubahatisha na kamari wakiamini ipo siku yao. Rafiki, huwezi kupata utajiri wa uhakika na wa kudumu kupitia michezo ya kubahatisha, usijaribu kufanya hivyo na kama umewahi kufanya basi acha mara moja. Michezo ya kubahatisha siyo kanuni sahihi ya utajiri. Imeandikiwa Utajiri unatengenezwa na vitu viwili vikubwa;

NAMNA YA KUFIKIRI


Kuna namna ya kufikiri ambayo matajiri wanaitumia. Matajiri wana fikra chanya kuhusu fedha na utajiri, hufikiri kuhusu uwezekano na wanajua kuna utele wa chochote wanachokitaka kwenye dunia hii. Matajiri Wanajua dunia ina rasilimali za kutosha na haziwezi kuisha kamwe.

Kwa upande wa pili, masikini wana namna ya kufikiri ambayo inawaweka kwenye umasikini maisha yao yote. Kwanza wanaamini utajiri siyo kitu kizuri, wanajiambia umasikini ndiyo bora.

Pia wanaamini kwenye uhaba,kwamba dunia ina uchache na wachache pekee ndiyo wanaoweza kunufaika na rasilimali chache zilizopo. Kwa kuwa na mtazamo huu, masikini hufikiri ili wao wapate lazima wengine wakose, masikini wengi wao tena ni watu wenye nguvu wasiokuwa na ulemavu wowote ule hutumia andiko hili Kama silaha yao ya kujilinda.

NAMNA YA KUTENDA

Kiungo cha pili cha sayansi ya utajiri ni namna ya kutenda. Wale wanaotajirika wana namna ya kufanya mambo yao ambayo yanawaletea matokeo makubwa na mazuri sana. Wakishapanga kitu cha kufanya, wanachukua hatua mara moja, hawaahirishi kitu na hawaruhusu usumbufu wowote ujitokeze na uwatoe kwenye kile wanachofanya. Watu hawa wana vipaumbele ambavyo wanavisimamia na kufanyia kazi. Na chochote wanachofanya, wanakifanya kwa ubora wa hali ya juu sana. Kwa maana Imeandikiwa

Kwa upande wa pili, masikini wana namna yao ya kutenda mambo ambayo inawafanya waendelee kuwa masikini kwa maisha yao yote. Kwanza kabisa hawajui wanataka nini, hivyo muda wote wako ‘bize’ harakati zao hazina tofauti sana na harakati za Inzi lakini hakuna matokeo makubwa wanayopata kutokana na ubize wao.

Pili Masikini ni wazuri sana kwenye kuahirisha mambo, wanapanga wenyewe vitu vya kufanya lakini unapofika wakati wa kufanya utasikia wanajiambia Nitafanya kesho.

Imeandikiwa masikini wamezungukwa na kila aina ya usumbufu na hawataki kupitwa na jambo lolote katika maisha yao, hali hii inawachosha hata kabla hawajafanya kazi. Na hata pale wanapofanya kazi, wanaifanya kwa ukawaida sana, kama vile hawataki.

Kwa tabia hii utajiri kwao wataendelea kuusoma kwenye magazeti na kuuona kwenye TV.
 
Misemo ya kimasikini

1. Kupata ni majaaliwa
2. Mungu humpa amtakaye na humnyima amtakaye
3.Duniani tunapita, majumba na maghorofa ni fahari za dunia
4.Pesa sio kila kitu
5. Hata uwe na pesa dunia nzima ukifa huzikwi nazo
 
Ilimaanisha nini?
Ilimaanisha hauwezi KUUTUMIKIA UTAJIRI/MALI au KUUTANGULIZA na ukaweza kumtumikia au kumtanguliza Mungu, yani ilimaanisha huwezi kukufanya UTAJIRI kuwa jambo kuu maishani na ukaweza kumtumikia Mungu.

Kuwa tajiri sio dhambi na kuwa maskini haimaanishi hautangulizi pesa maishani, ni jinsi mtazamo wako ulivyo yani kipi umekipa kipaumbele, unaweza kuwa tajiri na ukamtanguliza Mungu badala ya pesa na wapo maskini ambao kwao pesa ndio jambo kuu.
 
Huyu maskini mwenzetu lakini anatukana daaaa.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Why don't you discuss issue presented instead you are making personal attack???
 
Why don't you discuss issue presented instead you are making personal attack???
🤣🤣🤣 Ewe maskini mwenzetu ina maana hujui tabia zetu za kujadili mleta mada badala ya mada?
 
Misemo ya kimasikini
1. Kupata ni majaaliwa
2. Mungu humpa amtakaye na humnyima amtakaye
3.Duniani tunapita, majumba na maghorofa ni fahari za dunia
4.Pesa sio kila kitu
5. Hata uwe na pesa dunia nzima ukifa huzikwi nazo
6. Matajiri wengi wanatumia uchawi/dawa/kafara/ ni freemason.
7. Matajiri wengi ni wezi/wauza madawa ya kulevya.
 
Back
Top Bottom