Kupata utajiri siyo suala la bahati, ni sayansi kama zilivyo sayansi nyingine

Kupata utajiri siyo suala la bahati, ni sayansi kama zilivyo sayansi nyingine

Vipi wale waliopata utajiri kwa urithi, au kwenye madini hawa walitumia sayansi gani.
 
Sio kila kitu chenye sheria na kanuni ni Sayansi.

Na ukweli ni kwamba bahati ina mchango mkubwa katika watu kuwa matajiri au maskini.

Hizi hapa ni baadhi ya bahati;

1. Aina ya familia mtu anayozaliwa na kukulia
Ukibahatika kuzaliwa kwenye familia bora mfano ya matajiri wakubwa au watawala wa nchi una nafasi kubwa ya kuwa tajiri, ukibahatika kuzaliwa kwenye familia duni na ukazungukwa na watu hoehae maishani mwako kuna uwezekano mkubwa ukabaki kuwa maskini maisha yako yote.

2. Uwezo wa akili kuchambua mambo
Kuna watu wanazaliwa na uwezo mkubwa wa kuchambua mambo na kujuwa lipi litakuwa na manufaa wakati mwingi, hawa ndio huwa mameneja wazuri hata wakiwa na degree tu inawatosha kufanya mambo makubwa.Kuna watu hata wasome wafikie kuwa maprofesa uwezo wao wa akili kuchambua mambo unakauwa bado hafifu.

3. Kuna watu wanabahatika kupewa nafasi au fursa ambazo sio rahisi kwa watu wengine kwenye level zao kupatiwa na hatimaye maisha yao yote yanabadilika wanapozifanyia kweli hizo nafasi au fursa.
 
Misemo ya kimasikini
1. Kupata ni majaaliwa
2. Mungu humpa amtakaye na humnyima amtakaye
3.Duniani tunapita, majumba na maghorofa ni fahari za dunia
4.Pesa sio kila kitu
5. Hata uwe na pesa dunia nzima ukifa huzikwi nazo
Maneno ya kujifariji ili tuendelee kuishi kwenye umaskini [emoji3][emoji3]
 
Ila nataka nikwambie kwenye kufanikiwa hakunaga formula,na kama ingekuwepo formula kila mtu angetumia hio kanuni kufanikiwa
 
Ungeanza na Definition ya Utajiri, wadau wengi wangekuwa sambamba na unachoongelea.
Mmoja kwake utajiri ni kuwa na Wake wengi.
Mwingine ni kuwa na uhakika wa kula, kuvaa na pa kulala. Na mwingine kuwa ni mifugo mingi..Bila kusahau mwengine ambaye ameandaa maisha ya vizazi vyake vitatu vijavyo.

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
 
Hello mkuu@ Ben zen tarot
Umesoma kitabu cha "the science of getting rich " cha wallace naona umequote baadhi ya concept zake
 
Back
Top Bottom