Kupatwa kwa jua [Solar eclipse] - swali

Kupatwa kwa jua [Solar eclipse] - swali

Njaa

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2009
Posts
1,022
Reaction score
412
Hello great thinkers

Nilisoma geography siku za nyuma, niliambiwa na mwalimu wangu wa shule ya kata kuwa, kupatwa kwa jua hutokea pale mwezi unapokuwa katikati ya dunia na jua, hii hufanya jua kuzibwa na mwezi kwa kiasi fulani na kutengeneza kitu kama kivuli kwenye uso wa jua. Inapotea hali hii, wale walio upande wa dunia ambao ni mchana watashuhudia kufifia kwa jua na wakati mwingine giza la kizushi mchana.

Swali langu ni hili, mwezi huzunguka dunia kwa siku 28, wakati huo dunia inaendelea na mzunguko wake kuzunguka jua. Kwa hali ya kawaida, nategemea kuwa ndani ya siku 28 ni lazima mwezi uwe katikati ya jua na dunia walau mara moja. Sasa mbona hii ishu ya solar eclipse ni nadra sana kutokea? au sikumwelewa vizuri mwalimu wangu wa jiographia?

Usiniambie niende ku-search google, hebu nisaidie kwa hili kama una uelewa nalo

Njaa
 
ndo mana huwa unauona mwezi katika siku 28 vipande vipande, huuoni sku zote upo full circle kutokana na position ya mwezi na dunia from sun, ikitokea eclipse mwezi unakua na postion ambayo siku ile hautakiwi uwepo
 
ila mkuu mwez huonekana hata mchana pia na muda mwingine unakua half circle sasa ianakuaje kwa hili
 
Back
Top Bottom