SoC03 Kupenda, kujali (Kusaidia), kuamini watu kulipelekea maumivu nikiwa shule

SoC03 Kupenda, kujali (Kusaidia), kuamini watu kulipelekea maumivu nikiwa shule

Stories of Change - 2023 Competition

Taelyn

New Member
Joined
Jul 29, 2022
Posts
1
Reaction score
1
Miaka ya nyuma sikuwa najua kuwa sio Kila anaekuja kwenye maisha yako basi ni rafiki yako.

Nimesoma shule Moja hivi nikiwaa secondari(ya wasichana tu)kiukweli nilikuwa mpweke sana kwa sababu sikuwa na mtu wa kumuita rafiki wa karibu ,japo wote niliyokuwa nasoma nao nilikuwa nawaita marafiki.

Kwahiyo nilikuwa ni wakushinda darasani tu(sio kwamba Kila muda nilikuwa ninasoma) ila kwasababu sikuwa na mtu wa kuzungumza nae na kubadilishana mawazo kwahiyo nilijiona mpweke sana na kujiuliza mbona watu wote kwangu ni marafiki ,Sina ugomvi nao lakini nipo peke yangu sana na hata nikienda bwenini kuchangamana nao sioni ushirikiano?.

Kwahiyo nilibidi niizoee ile Hali kwa namna yoyote ile japo ilinichukuwa mudaa sana kuikubali ile hali,maan nilitegemea kupokea upendo mkubwa sana kutoka Kwa hao niliyokuwa nawaita marafiki sababu Mimi nilikuwa nikiwajali sana nikimaanisha wakiwa na shida yoyote ile na akija kwangu yeyote yule kikiwa ndani ya uwezo wangu basi namsaidi sijili itanigarimu vipi ila tu yule mtu afurahie.

Kwahiyo nilikuwa nimeweka furaha za wengine kama kipaumbele bila kujua nilipasawa kujipenda Mimi kwanza, yaan ata kikiwa njee ya uwezo wangu kuifanya basi nitaifanya lolote lile Ili tu nimfanyie au nimpe alichonoimba nimsaidie ,kuna wakati Hadi mimi mwenyewe nilikuwa najinyima Ili nifanye kwaajili ya mwingine kumbe sikuwa najua wao walikuwa hawanijali wala kinithamini.

Nilipofika form four nikama ndio nilikuja kuelewa. Nilikuwa mtu amber ni mkimya sana kiasi kwamba mtu akiniongelea vibaya kwa uwongo sikuwa najali sababu nilikuwa sipendi ugomvi kabisa kwahiyo baadhi Yao walichukulia Kama udhaifu wangu na baadhi yao wakitaka kusema kitu kibaya Kwa mtu wanatumia jina langu kwamba Mimi ndio nimesema wakati ni Moja ya njia zao za kufikisha taarifa. Sikuwa nakuja kinachoendelea sababu pia sikuwa nachangamana.

Siku moja nikiwa form four ndio kama nilianza kuelewa kuwa nasaidia sana watu amabao hawanisaidi hata kidogo nikikwambia yangu, nawapenda watu amabao sioni ule ule upendo kutoka kwao,na ninajali sana watu wasijalika ,nilitafakari sana kuwa Kuna mengi sana nimejitoa kwaajili ya wengine ila yangu hakuna anaejali, baadhi ya watu wakawa wanakuja kunikopa Hadi pesa na kuomba ushauri kutoka kwangu ,ila muda wa raha zao wanatumia watu wengine ila shida zao wanataka nizibebe Mimi.

Sitosahau, niliwahi kumuomba msichana mmoja akiwa anaamka usiku kusoma awe ananiamsha na Mimi sababu Kuna watu alikuwa anawaamsha na wanaenda kusoma wote.

Baadhi ya niliyojifunza kwenye maisha ni kubaliana na Hali uliyokuwa nayo na utafute suluhisho (changamoto haikimbiwi inatatuliwa);sali sana ; ishi na watu vizuri huijui kesho yako.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom