MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,580
Moyo ukija kupenda, wenda ukidundadunda,
Mtu aanza kukonda, anapomkosa nyonda,
Alalama kama konda, mwenzenu kumbe kapenda,
Mtu akiisha kupenda, huogopa kuvurunda
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!
Nakupa pole kaka, kwa hili lako saibu
Utafute muafaka, hili silo la ajabu
penzi kazi wangu kaka, waliyasema mababu
Naomba sikurupuke, kuutoa uamuzi
Nilimpenda fulani, yule binti wa jirani,
Kaniingia moyoni, penzi hadi mifupani,
Leo kanuna jamani, amepata kisirani
Kosa langu miye nini, najiuliza watani,
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi
Kaka wajipa presha, kwake binti jirani
Rohoyo kupaisha, pengine kitu utani
Wajua kina Aisha, tunapenda utani
Pengine anakupima, hebu punguza munkari.
Kusema nami hataki, akija kwangu habaki,
Kwenye miadi hafiki, nikichekesha hacheki,
Nisimuite rafiki, hata mpenzi hataki,
Hata kudeka hadeki, vya kuvila haviliki
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!
Ah hapa nimekubali, goma lina mpigaji
nawe mbinu ibadili, jifanye si mhitaji
Hata njia ibadili, kimwona simpe taji
kama wako tajibadili, akupe penzi la shata.