nimeshuka wanajamvi baada ya kukaa manyasini nikichungulia chungulia jamvi. Nimejaribu kujiuliza bila ya kupata jibu, hivi katika karne hii bado kuna mababa wanapiga wake zao!!.
Imenitokea mimi mwenyewe binafsi, ikabidi nihame nyumba, sababu jirani alikuwa na tabia mbaya ya kutwanga mke, natumai mwanipata..sio eti kuchapa vibao ama kuchapa mijeledi, laa kupiga na nia ya kuuuaa magumi mateke, jamaa anakanyaga kama ataka washa bajaj.
Ilikuwa usiku mmoja jamaa jirani(mtu na heshma zake,ofisaa fulani wa benki,sio eti vijana hawa wakihuni) kaingia nyumbani baada ya kutoka ulevini, majira ya saa za manane, twasikia mayowe na vurumai!!, kama majirani wema tumetoka kusaidia. Mara twagundua bwana apiga bibi. Hasira zikanipanda nikataka kuingilia lakini mwenzangu akaniambia "watu walalao blanket mmoja mambo yao usiiingiliee", nikapoesha hasira, na kwa kweli baada ya masiku kidogo hivi niliona majirani hao hao wameshikana mikono watoka shopping.......daahhhh nilihama mtaa huo.
Nimekuwa mpaka mtu mzima, sikuwahi kuona baba yangu na mama wakipigina, sasa imagine hio "trauma", kawaida mimi ni mtu mtulivu lakini nachukia sana maonevu!!!!
Jamani...hata kama ni itikadi zetu, (kuna makabila, bila kutaja yana mambo haya), jamani wana jf, kama kuna waume wenye tabia kama hizi humu, jamani wacheni tuwe wastaraabu. Kuna njia mbadala za kusuluhisha migogoro ya nyumbani sio kupigaaaaa......grrrrrrrrrrr