sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
A. KUPIGA & KUGOMBEZA WATOTO KWASABABU YA UWEZO SHULENI NI UJINGA
Unakuta mtoto kila siku anaenda shuleni, anahudhuria kila kipindi, anafanya home work, n.k. ya nini kumchapa au kumgombeza huyu pale anaposhika namba za kawaida au chini darasani. nimesema namba kwasababu ndicho kigezo ambacho wazazi / walezi wengi hukiangalia, yani hata kama mtoto kafaulu vizuri mitihani lakini wao wanaangalia kashika mafasi ya ngapi.
Wengine huenda hatua za ziada kusomesha watoto wao shule za gharama huku wakiamini pengine ndio suluhisho kwa asilimia 100, matokeo yake mtoto akienda huko na kuwa na uwezo ambao bado shaujafikia mategemeo ya wazazi wake, wanamgombeza kwamba wamejibana sana ili asome huko, mtoto anapewa kipigo kwa makosa ambayo sio yake mithiri farasi aliepelekwa shule ya mamilioni ili awe na uwezo wa kuogelea kama wa samaki.
Ipo hivi wazazi wenzangu, hata sisi binadamu tunatofautiana uwezo,mtoto anaweza kuwa kajaliwa uwezo mkubwa shuleni kiasi kwamba hata akisoma shule hizi za kata zenye changamoto kubwa, unakuta anafaulu vizuri kabisa,
lakini kuna watoto wengine uwezo wao wamejaliwa zaidi sehemu nyingine , hivyo uwezo wa darasani unaweza kuwa mdogo , hawa kuwasaidia inabidi ufanya haya:
hapo lengo liwe aweze kupata hata ufaulu wa kawaida wa kumfanya asonge mbele, kama ni form 4 basi apate walau division 3
B. KUPUUZA "PLAN B" NI UJINGA ULIOTUKUKA!!
Haijalishi mtoto ana uwezo kiasi gani huko shuleni, kwenye haya maisha haya ya sasa apa bongo huwezi kuweka mategemeo yako yote kwenye njia moja tu ya mafanikio, Nadhani sote ni mashahidi wa jinsi utitiri wa wasomi unavyozidi kujaa mitaani kadri miaka inavyoenda, kwa siku hizi kumaliza degree hapa nchini ni kama kumalza darasa la saba, degree zipo nyingi sana huku mitaani. (Mwenye uhakika wa elimu yake kumpa ajira ni mzanzibari tu, asilimia 21 za ajira za huku kwetu ni zao na pia huko kwao, ni wao tu wenye sifa za kuajiria na serikali yao)
ni wakati wa kusimama na miguu miwli, zile enzi za kusimama kwa mguu moja kusoma ili uajiriwe zilishapita, unahitaji "plan b" ili "plan a" ikifeli bado uwe umesimama na sio kulalamika tu umesoma sana
Kwa watoto wenye vipaji au uwezo flani tangu wadogo, hawa watoto ni mithiri ya chui mwenye mbio na uwezo mkubwa wa kuwinda lakini unapompima kwa kigezo cha uwezo wake wa elimu ya darasani mithiri ya uwezo wa kuogelea, hapo utakua umeufungia uwezo wake wa chui. Kama mtoto unaona wazi kabisa ana kipaji au uwezo flani wewe muendeleze huko, huenda ni kitu alichobarikiwa na ni baraka waliyopewa wachache kufanya vitu vigumu kwa wepesi, wengine inabidi wasomee, kufundishwa na kutia bidii sana lakinii yeye kazaliwa na hiyo baraka, kama anatimiza jukumu lako la yeye kusoma kadri ya uwezo wake basi na yeye apewe nafasi kuendeleza alichojaliwa endapo kina manufaa maana si kila kipaji kina manufaa. unakuta mtoto anapenda sana upishi, ufundi, ushonaji, mpira, kuhubiri / kusoma koran, n.k huyo jua tu ya kwamba hio baraka yake ni zawadi na si ya kupuuzwa, ni baraka inayoweza kuwa plan b.
Kwa watoto wengine, akimaliza form 4 nashauri umpeleke veta mwaka mzima kisha ndio aenelee na shule, huko veta nadhani kozi ni miezi miwili lakini hi huwa ni elimu ya darasani kwa kiasi kikubwa, miei inayobaki inabidi aingie kazini kupata ujuzi zaidi kujua changamoto, kuzoea mazingira, n.k. hapa itamsaidia sana hata akiwa likizo akianza shule au chuo basi atakuwa hashindi mitaani kusubiri likizo iishe, atakuwa bize kujitaftia ridhiki yake, na hii ni mpaka hata akihitimu chuo, yani hatakuwa amekaa tuu yupo yupo anasubiria kuitwa kwenye ajira, hapa atakuwa anafanya mambo yake na neema ikimjia anaweza kusahau kabisa hizo ajira .

- kuwasaidia wasome shule zenye walimu wa kutosha.
- kuwalipia tuition, kama hela ipo mletee kabisa mwalimu nyumbani ili kama hajaelewa aelekezwe upya bila kuogopa wenzake.
- usiwapeleke boarding - huko boarding ni kazi sana kujua ana yopitia, pia tuition hakuna.
- kuwapa moyo,
- kufatilia mahudhurio yao, homework, n.k