DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Anaandika Godlisten Malisa
Hii inaweza kuwa political spinning tu. Kwenye strategic communication & media framing kuna kitu kinaitwa “biased interpretation” yani kutafsiri picha kwa upendeleo ili kuunda taswira chanya kwa jamii.
Hujawahi kuona mtu anapiga picha na mtu mashuhuri halafu anaifanyia biased interpretation? Kwa mfano mtu anapiga picha na Rais halafu akigombea ubunge anasema Rais kamtuma? Au mtu anapiga picha na Mkuu wa Majeshi halafu anaitumia kutishia wananzengo?
July 1978 kwenye mkutano wa dharura wa OAU uliofanyika Khartoum, Idi Amin alijigamba kuutwaa mkoa wa ziwa magharibi wa TZ (Kagera) kuwa sehemu ya Uganda. Baada ya hotuba akamfuata Nyerere kwenye kiti kumpa mkono na kupiga naye picha.
Picha hiyo ikatumika kufanya spinning kwenye media za Uganda. Radio na magazeti yakaripoti kuwa Nyerere amekubali kuiachia Kagera. Mengine yakaandika Nyerere aogopa kushindana na “Conqueror of British Empire” kama ambavyo Idi Amin alikuwa akijiita.
Lakini je ni kweli Nyerere alikubali kuiachia Kagera kwa ushahidi wa picha tu? Hapana. Haikuwa kweli. Idi Amin alitumia picha hiyo kufanya spinning. Kwenye siasa mabingwa wa spinning huitwa Spin doctors. Wapo duniani kote. Hao wape picha tu story watakuandikia.
Oktoba 9, 1978 Idi Amin aliingiza majeshi yake Kagera na kutangaza rasmi kuwa eneo hilo ni mali ya Uganda. Oktoba 25 Tanzania ilijibu mapigo, na kilichotokea wote tunakijua. Ilikuwa fundisho.
Sasa jiulize kwanini story ya UN imeripotiwa na media za bongo tu? Na zote zimeripoti kama “makasuku” kuonesha wazi muandaaji wa script ni mmoja. Yani UN ipongeze TZ halafu story kubwa kama hiyo iripotiwe na Jamvi la Habari? Kumbuka UN wana radio yao, tena yenye idhaa ya Kiswahili. Je umesikia ikitangaza hizo pongezi? Yani UN iache kutumia radio yake kutoa pongezi itumie Nangurukuru FM? Hivi mnatuonaje? 😄
Kumbuka UN ililaani mauaji ya Oktoba 29 kwa waraka rasmi. Sasa iweje wapongeze gizani? Kama walilaani kwa waraka basi hata pongezi wangezitoa kwa waraka pia. Lakini ukienda kwenye website yao utakuta waraka uliopo ni ule wa kulaani tu. Je wa pongezi uko wapi? Next time tumieni watu wenye akili kufanya spinning. Bata, Wahed.!