ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 631
- 1,577
Kupigwa na kujeruhiwa kwa Msichana Songwe:
Tunataka Mkuu wa Wilaya awajibishwe haraka!
Utangulizi
Chama cha ACT Wazalendo kupitia kwa Msemaji wa Ustawi na Maendeleo ya Jamii, tumepokea kwa masikitiko makubwa kitendo cha Mkuu wa Wilaya wa Songwe Ndg. Simon Peter Simalenga kumshambulia binti wa miaka 20 anayetambulika kama Florencia Chrispin Mjenda kwa kumpiga makofi hadi kumjeruhi eneo la jicho.
Tunalaani na kukemea kwa nguvu zetu zote kitendo hicho hususan kufanywa na Kiongozi aliyeteuliwa na Mheshimiwa Rais na kukabidhiwa Ofisi ya Umma kwa ajili ya kuwahudumia Wananchi. Badala yake, Mkuu huyu wa Wilaya amejibadili na kuwa nyapara na mtu katili dhidi ya Wananchi tena katika masuala ambayo hayahitaji kutumia nguvu.
Tunashangazwa zaidi, kuona kwamba tangu alhamisi tarehe 29 Novemba 2022 alipofanya tukio hilo la kikatili bado yuko kwenye Ofisi ya Umma hadi leo.
Wakati Dunia inaadhimisha siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya makundi mbalimbali kwa kutafakari, kuhamasisha mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake, wasichana na hata wanaume yeye anaongoza kuimarisha ukatili.
ACT Wazalendo pamoja kukemea vikali tukio hilo tunataka hatua zifuatazo zichukuliwe katika kujenga heshima ya Ofisi za Umma na kulinda haki za Msichana huyo:
1. Mamlaka ya Uteuzi wa Mkuu wa Wilaya (ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) huyo kuchukua hatua za haraka kwa kutengua uteuzi wake.
2. Hatua za kijinai zichukuliwe dhidi ya Ndg. Simon Peter Simalenga ili kutoa fundisho kwa viongozi wengine kuheshimu mipaka ya kazi zao kwa kufuata taratibu, kanuni na sheria za nchi.
ACT Wazalendo tunatoa wito kwa viongozi wa umma kuacha kuongoza kwa vitisho dhidi ya Wananchi, kuacha kujichukulia sheria mikononi na kuzima uhuru wa watu. Matumizi ya vitisho katika kuongoza wananchi hakutowafanya kupendwa, kuheshimiwa wala kuwaletea watu maendeleo badala yake kutajaza uhasama, chuki, hofu na kushusha heshima za ofisi wanazoziongoza.
Imetolewa na;
Ndg. Janeth Joel Rithe
Twitter: @JaneRithe
Msemaji wa Sekta ya Ustawi na Maendeleo ya jamii, wanawake na watoto,
ACT Wazalendo
06 Disemba, 2022.