Kupigwa na jua ni muhimu kuliko tunavyodhani

Kupigwa na jua ni muhimu kuliko tunavyodhani

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Moja ya vitamin ngumu kabisa kupatikana kutoka kwenye vyakula ni Vitamin D. Mahitaji ya siku ya vitamin D kwa binadamu ni wastani wa 600IU(International Unit). Ni vyakula vichache sana vinaweza kukupatia kiasi hiki cha vitamin D kwa siku.

Vitamin hii hupatikana kwa wingi kwa kupigwa na jua. Mtu ukipigwa na jua la wastani, kwa siku unaweza kutengeneza hadi 10,000IU! Yaani karibia mara ishirini ya kiasi kinachohitajika kwa siku. Jua likipiga kwenye ngozi yako miale ya ultra Violet inasababisha mafuta(Cholesterol) kwenye ngozi yako yabadilishwe kuwa vitamin D.

Tumesikia sana kuwa vitamin D inahusika na unyonyaji wa madini ya Calcium ambayo huimarisha mifupa. Ndiyo maana watoto wenye upungufu wa vitamin hii mifupa yao huwa lege lege na kupelekea kupinda(Matege). Lakini tafiti za karibuni zimeonyesha kuwa kuna uhusiano mkubwa sana wa upungufu wa vitamin D na unene wa kupita kiasi, kuzuia insulin kufanya kazi na kisukari aina ya pili.

Uwezo wa ngozi kubadili miale ya jua kuwa vitamin D inategemea sana rangi ya ngozi. Watu weupe ngozi zao hubadili miale hiyo kuwa vitamin D kwa ufanisi mkubwa kuliko watu wenye ngozi nyeusi. Mtu mweusi anatakiwa kupigwa na jua kwa muda mrefu ili aweze kubadili miale kuwa vitamin D kuliko mtu mweusi. Watu weusi wanaoishi maeneo yenye kiasi kidogo cha jua kama Ulaya wanapatwa sana na tatizo la upungufu wa vitamin D, pengine ndiyo sababu wamarekani weusi wanaongoza kwa kupata magonjwa ya kisukari na kuwa na unene wa kupitiliza.

Jitahidi sana upigwe na jua. Hata ukijenga nyumba hakikisha unaweza kufungua madirisha na mwanga wa jua ukafika ndani(Miale ya UV haipenyi kwenye kioo, so kupigwa na jua kupitia kioo hakuwezi kukupatia vitamin D).

Wazee wanauhitaji mkubwa wa vitamin D kuliko vijana. Kama una mzee wako hakikisha anapata jua la kutosha. Kama haiwezekani basi hakikisha anapata ya kutosha kwa njia nyingine kama dawa za kuongeza vitamin D.

Lakini angalizo: Kupigwa sana na jua kunaweza kusababisha kuungua ngozi na kuongeza hatari ya kupata kansa ya ngozi.
 
Mmhh kibongo bongo siyo kwa jua la Dar na Dom, hata hivyo ni jua la asubuhi ndio lenye faida, sasa we jianike mchana wa kiangazi uone kama hujazeeka kabla ya wakati
Wengi wanaenda job kabla jua halijatoka, wanashinda ndani hadi jioni wanarudi nyumbani. Wiki nzima hapati jua la kutosha japo anaishi eneo leo jua kali.
 
Wataalamu wanasema kupigwa na jua kali la mchana kwa muda mfupi ndiyo njia nzuri zaidi ya kupata vitamin D. Muda wa kupigwa inategemea mambo mengi, rangi yako, ukali wake, sehemu ulipo nk nk.
Sema maisha yetu haya nadhani tutakua tunazidisha kabisa
 
Najiandaa kwenda church nashangaa jua hilo limeingia ndani..,nikafungua mlango Kabisa linipige vilivyo☹️...bahati iliyoje kufuatwa na jua kwa sebule😜
 
Back
Top Bottom