Fundi ukimpata kanjanja utajenga hata nyumba iliyopaswa kugharimu milioni 50 iwe milioni 80, ndio maana huwa sishangai mtu anaposema kajenga nyumba kwa milioni 100 wakati nyumba hio hio mwengine kajenga kwa milioni 70 maeneo hayo hayo..
Maana wengi wanapoanza kujenga huwa ni wageni wa haya mambo. Fundi atakwambia nondo bei flani yeye anaenda kununua za bei ya chini zenye strengtyh ndogo.
Finishing huko ni bei lakini sasa na mafundi kwa kujua hili kwamba wajenzi wanajua finishing ni gharama nao wanatwanga zaidi, kisingizio chao "finishing ni gharama"
Mambo ya mifuko ya cement hapa ndio pana upigaji mpaka basi, mifuko inatumia 50 yeye anaomba hela ya mifuko 80 na kweli unaiona lakini hio 30 anakuwa kaazima tu anarudisha ama atairudisha alikonunua.
Kwanza kabisa ili fundi asikupige patana nae vizuri,
Mpe pesa aliosema kuwa anaihitaji,
Usimbane sana kwenye malipo,
Pili muamini sana,
Tatu muoneshe kuwa unamtegemea sana ili upate kilichobora kabisa,
Mahirikishe kwenye kilakitu,
Mafundi tuko kama watoto [emoji23]
Ukitujali kwa vitu vidogo tuu tunaona huyu Boss ni mtu mwenye roho nzuri basi upgaji wakipuuzi hautakuwepo,
Nikupe mfano,
Nilienda kufanya kazi Kampala Uganda kunakitongoji kimoja kinaitwa LUBOWA,
Mshua aliona kazi mtandaoni akanichek akatuma milioni moja na laki 2 kama nauli na pesa ya kupima Covid(kipindi kile chanjo bado) kwa mafundi wanne,
Just imagine tumechat maramoja tuu tena mesej kama kumi tuu katuma milion na laki mbili,
Hapo tayari unaona mahua kaonesha imani kubwa sana kwetu kwahyo hata ile roho ya tamaa inaondoka,
Lakini kunamaboss wengne nauli ya moro elfu 10 kwa watu wanne elfu 40 tuu anaanzavipengele kibaoo oohh je nikiwatumia afu msipokuja mkanitapeli mara kunamtu namtumia mkutanenae akawakatie ticket na vitu kama hvyo,
Haya tumefika kampala katupokea fresh mpaka site kesho kazi inaanza katulipa hela yote ambayo ni zaidi ya milioni 8 alikuwa na mjengo mkubwa sana na kulikuwa na decoration nyingi sana,
Siku ya pili yeye huyo kapanda pipa kaenda Bahrain [emoji1041] ndipo anafanya kazi huko(ni injinia wa QATAR AIRWAYS) hajarudi mpaka tumemaliza kazi, yeye anaona kwa picha tuu,
Anaondoka ananiambia nakuamini kilakitu nimekuachia wewe,
Asikupangie yeyote yule chakufanya(maana kulikuwa na muangalizi wa site pale anasema anapenda sana kuendesha mafundi anavyitaka yeye)katuachia hela ya kununua mazaga ya kutosha kulazaidi ya mwezi mzima na sisi kazi yetu ilikuwa kama ya wiki tatu tuu,
Jamaa tunamuita Big huyo msimamizi wa site akawa anatushawishi tupige cement na tile maana jamaa alinunua tile nying sana fundi aliepima alizidsha sana SQM zaidi ya SQM 150,
Kwahyo cement zilikuwa zakitosha na tiles zakutosha na tile box moja ilikuwa inauzwa elfu 72 kwa bei ya TZ kwahyo kwa UGANDA ingekuwa inafika kama laki2 hivii kwahyo kulikuwa na box zaidi ya mia za kupga na cement zaidi ya 50 za kupga,
Tile tuu kwa hela ya uganda ilikuwa tukipiga tunapata kama milioni 30 hivi,
Kwahyo na cement kwahyo ingefika hata milioni 22 hivii,
Apo anaongea na mimi kwasababu ndio fundi mkuu,
Sawa mimi mambo ya kupga sio tabia yangu na sijawahi kufanya hivyo,
Lakini kwa milion 22 za uganda kwa watu wawili kama huna roho unabutua unapita hivi,
Lakini ukifikiria trust ya mshua juu yangu dah unaona kama ni usaliti mkubwa sana unaenda kuufanya,
Yale mazaga tuu mafundi wenzangu wenyewe wanakwambia oya wanangu simnaona mshua alivyokuwa na roho kwahyo tufanye kazi ya kueleweka,
Kilamtu anajikagua mwenyewe kabla hata ya mm kwenda kumkagua,
Tena mtu akipita kwa mwenzie anaona kafanya kitu cha ajabu anamfumulisha yeye mwenyewe,
Katika kazi zetu bora kabisa tulizowahi kufanya ile ni yakwanza na mpaka sasa hakuna kazi bora zaidi ya ile tuliowahi kufanya ni made correction ya ajabuajabuu tuliyaweka,
Mwenyewe mshua aliongeza milioni kama Asantee na hapo aliona kwa picha tuu alivyorudi Uganda sisi tukiwa tumeondoka akatuma tena milioni kama asante tena,
Sasa njoo kwa hawa maboss wetu vichefuchefu kwanza wanakuwaga na zarau,
Wanapenda sana kuzarau kazi za watu,
Utasikia kwahyo unanitajia mabei makubwa ili ukitoka hapa kwangu na ww ukajenge?
Kunamwenzio ananisumbua kilasiku hata nusu ya hela yako hajafika,
Mara oohh kwanza kazi zenyewe kawaida tuu,
Mwisho wa siku mnashushanaa mpaka mnafikia hatua ya kufanya kazi,
Kwenye kazi hata kamistake kadogo tuu kaufundi makelele yake kama nini vile oohh tile hii mbona huku mwisho imeinuka kidogo unamuelekeza anakwambia aaahhh itoe hii,
Ukitoa ni kama umeanza upya tile zishashikana kwahyo unafumua karibu chumba kizima yeye haelewiii kashang’ang’ania,
Tiles zenyewe kanunua za bei chee full kupshana fundi unapambana nazo kama nn lakini akiona sehemu zimepishana hapa fumuaa kama hutaki mm silipi dah ushafanya kazi kubwa utafanyaje unafumua unaanza upya,
Vipengele milioni kidogo,
Sasa Boss kama huyo ukipata sehemu ya kuzabua unazabua kuziba vipengele vyako vile vya kufumua fumua na kupatana kwa hela ndogo,
Mwisho wa siku mnarudi kulekuleee,
Ndiomaana sisi wengine kwasababu ya kukataa dhambi kama hizo tumeamua kujichagulia aina ya washua wakufanya nao kazi tunasema kuna BOSS na BOSINGWA [emoji23][emoji23]
Boss site Survey tuu ya elfu 30 anasema hawezi kutoa ataweza kutoa milioni 3 mfanye kazi ?
Kunameng sana ya kuandka sema tupo busy jaman
[emoji3513] +255 714 122 011