Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 17,434
- 27,177
Chapati na Maharage Matamu 🙃🤔Wewe huwa unatumia Nini kufuta? Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetoa tahadhari kuhusu matumizi ya sponji au vipande vya godoro kufutia vikaango vya moto wakati wa kupika vyakula, ikiwemo chapati. Tahadhari hiyo imetolewa kupitia kipeperushi kilichochapishwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za shirika hilo, kikilenga kuhamasisha usalama wa chakula kwa walaji.
Kutumia sponji (iwe kipande cha godoro au sponji ya vyombo) kukandia au kufutia kikaango cha moto wakati wa kupika chapati kunaweza kusababisha saratani (kansa) baada ya matumizi ya muda mrefu. Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limepiga marufuku kabisa desturi hii kwa sababu za kiusalama na kiafya.
Madhara Makubwa ya Kutumia Sponji Kukaanga Chapati
Ushauri wa Kitaalamu:
- Kutengenezwa kwa Kemikali za Saratani: Sponji hazikutengenezwa kuhimili joto la jikoni (hazina sifa ya food-grade). Zinapokutana na kikaango cha moto, huungua na kuyeyuka, jambo linalozalisha kemikali zenye sumu (kama vile polyurethane au mabaki ya viwandani). Kemikali hizi huingia kwenye chapati na zikiliwa mara kwa mara kwa muda mrefu, huongeza hatari ya kupata saratani ya tumbo, ini au figo.
- Chembe za Microplastics: Sponji inapochanika na kusagika kutokana na joto na msuguano, huacha vipande vidogo sana vya plastiki (microplastics) na ungaunga wa godoro kwenye chapati ambavyo mlaji anavimeza bila kujua.
- Kusambaza Bakteria na Uchafu: Sponji huwa na matundu yanayohifadhi unyevu, mafuta na mabaki ya chakula kwa urahisi. Hali hii huifanya kuwa mazalia makubwa ya bakteria hatari na vijidudu vya magonjwa vinavyoweza kusababisha maumivu ya tumbo na kuharisha. [
Acha mara moja matumizi ya sponji jikoni. Badala yake, tumia vifaa salama vilivyotengenezwa maalum kwa ajili ya kupikia na kugeuzia chakula (kama vile miiko ya miti, vyuma maalum vya kukamata chapati, au silicone brushes/spatulas).
USHAURI KWA SERIKALI:
Tunaomba sheria kali ipitishwe, watendaji wapiie wauza chapati wote, faini iwe si chini ya laki 3 na kifungo cha miezi 3
View attachment 3689747
Tunasubiria 😃😃Tunasubiri mtuambie sabuni za kufulia zinaleta kansa endapo tutaogea au kuoshea vyombo
Watu wengi hawafahamu kama sponji au godoro ni plastic.Hili halihitaji tbs waseme sponji ni plastic Ile halafu inakutana na moto mkali lazima sponji liishie kwenye chapati tu
Sponji zina matumizi mengine tofauti na kupikia,wanaopikia ndo wanakosea.Sasa kwanini wasizuie tu matumizi ya hizo sponji!
Mzee hata sigara imeandikwa ni hatari kwa afya ,kwa hiyo ni akili kichwaniDuh,
Mamlaka yenye wajibu wa kulinda afya za wana jamii inatoa tahadhari tu kwa jambo hatari kama hilo badala ya kuchukua hatua kali na madhubuti mara moja kukomesha tabia na mazoea hatarishi !!
Kufa mwenyewe siyo uue watu we bwegeJamani1 vitisho kwenye misosi mpaka lini?? Acheni tujifie bwana!!!!
Wapi huko watoto wa kike hawapelekwi shule?Na kuna wanaofunika chakula cha moto na mifuko ya plástic hata majumbani inafanyika sana hii. Mtu akiwa anapika wali lazima afunike na mfuko wa plastic ndo anaona unaiva vizuri. Na wale wa kuwasha moto na mifuko ya plastiki.Yote haya kisa ukosefu wa elimu. Tupelekeni watoto wa kike shule, inasaidia kuepusha mambo kama haya.
Vyoo vya shimo na vile vya sink pia husababisha kansa, watu wanashauriwa wawe wanaenda maporini kuchimba na majembeWewe huwa unatumia Nini kufuta? Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetoa tahadhari kuhusu matumizi ya sponji au vipande vya godoro kufutia vikaango vya moto wakati wa kupika vyakula, ikiwemo chapati. Tahadhari hiyo imetolewa kupitia kipeperushi kilichochapishwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za shirika hilo, kikilenga kuhamasisha usalama wa chakula kwa walaji.
Kutumia sponji (iwe kipande cha godoro au sponji ya vyombo) kukandia au kufutia kikaango cha moto wakati wa kupika chapati kunaweza kusababisha saratani (kansa) baada ya matumizi ya muda mrefu. Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limepiga marufuku kabisa desturi hii kwa sababu za kiusalama na kiafya.
Madhara Makubwa ya Kutumia Sponji Kukaanga Chapati
Ushauri wa Kitaalamu:
- Kutengenezwa kwa Kemikali za Saratani: Sponji hazikutengenezwa kuhimili joto la jikoni (hazina sifa ya food-grade). Zinapokutana na kikaango cha moto, huungua na kuyeyuka, jambo linalozalisha kemikali zenye sumu (kama vile polyurethane au mabaki ya viwandani). Kemikali hizi huingia kwenye chapati na zikiliwa mara kwa mara kwa muda mrefu, huongeza hatari ya kupata saratani ya tumbo, ini au figo.
- Chembe za Microplastics: Sponji inapochanika na kusagika kutokana na joto na msuguano, huacha vipande vidogo sana vya plastiki (microplastics) na ungaunga wa godoro kwenye chapati ambavyo mlaji anavimeza bila kujua.
- Kusambaza Bakteria na Uchafu: Sponji huwa na matundu yanayohifadhi unyevu, mafuta na mabaki ya chakula kwa urahisi. Hali hii huifanya kuwa mazalia makubwa ya bakteria hatari na vijidudu vya magonjwa vinavyoweza kusababisha maumivu ya tumbo na kuharisha. [
Acha mara moja matumizi ya sponji jikoni. Badala yake, tumia vifaa salama vilivyotengenezwa maalum kwa ajili ya kupikia na kugeuzia chakula (kama vile miiko ya miti, vyuma maalum vya kukamata chapati, au silicone brushes/spatulas).
USHAURI KWA SERIKALI:
Tunaomba sheria kali ipitishwe, watendaji wapiie wauza chapati wote, faini iwe si chini ya laki 3 na kifungo cha miezi 3
View attachment 3689747
Hawa TBS nao ni Changamoto.Wewe huwa unatumia Nini kufuta? Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetoa tahadhari kuhusu matumizi ya sponji au vipande vya godoro kufutia vikaango vya moto wakati wa kupika vyakula, ikiwemo chapati. Tahadhari hiyo imetolewa kupitia kipeperushi kilichochapishwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za shirika hilo, kikilenga kuhamasisha usalama wa chakula kwa walaji.