Kupima HIV mara kwa mara: Je, ni kuangalia afya tu au kutokutulia kwenye mahusiano ndio sababu?

Super women 2

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2016
Posts
5,164
Reaction score
6,540
Mimi huwa napenda Sana kucheki afya yangu na hasa vipimo vikubwa Kama H.I.V ninaweza kucheki mara 3 kwa mwaka au chini ya hapo ila mwenzagu yeye ni mbishi wa kupima H IV balaaa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sidhani hata kama alishawahi kupima.

Ukitaka kukosana nae mwambie twende tukapime, nikimwambia nimetoka kucheki afya utasikia naomba majibu haraka utafikiri kapima yeye. Ataanza sasa kuniambia ohoo utakuwa unachepuka, kwa nini unapima mara kwa mara.

Sijui hivi na vile mpaka anakasirika na mimi wala sichepuki ila napenda tu kujua afya yangu. Mara anishauri nisiwe napima mara kwa mara na mimi napenda. Je, kwani mtu kucheki afya mara kwa mara ni uhuni???
 
Endelea kupima siku ukikutwaa nao ndio utaacha kupimapima
 
To me check ups muhimu kama mwanandoa ni zile annual exams za kike mfano pap smear, dental check up na breast checkup.

Nikiwa mja mzito ndo nitafatisha ninayohitajika kupima na Dr wangu.

Otherwise vipimo vingine ni kama nikijisikia vibaya. Mfano Malaria na UTI

Am married, sichepuki na sina sababu ya kum doubt hubby wangu so HIV kiukweli sipimagi mara kwa mara.

Ushauri wangu kwa vijana ambao hawapo kwenye ndoa ni watulie wajizuie kuzini. Hapo wataepuka ulazima wa kupima HIV kila mara na watapunguza exposure kwa magonjwa kama Hepatitis
 
pima tu kila mara maana serekali ilishasema kuwa mwaka huu italeta dawa ya ukimwi ata ukikutwa nao utapata dawa ila mm siendi pima Ata kwa kisu shingoni bila dawa kupatikana
 
Najitahidi sana kujilinda. Ntajitahidi kumshauri akapime asee. Mambo ya kuja kuumizana mabaya Sana.
 
Endelea kupima siku ukikutwaa nao ndio utaacha kupimapima
Siku nikikutwa nao ntaanza kutumia doze. Na ntaendelea kupima.
Ila usiniombe hivyo bana [emoji23]
Ila hujui tu. Kujua afya yako raha sana.
 
Hongera kwa kumwamini u hubby [emoji23]
 
Ukimwi nimewahi kupima mara 2 tu tena kwa sababu nilikuwa nampeleka mama watoto clinic na nyingine nilikuwa namtolea damu baba yangu wakat anaumwa
 
pima tu kila mara maana serekali ilishasema kuwa mwaka huu italeta dawa ya ukimwi ata ukikutwa nao utapata dawa ila mm siendi pima Ata kwa kisu shingoni bila dawa kupatikana
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119]
 
Nimepima Mara ya mwisho 2013 sijawahi pima tena kazi yangu kusukumiza wengine wapime maana wakiwa Safi mi pia safi
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kumbe mpo wengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…