Mzee Mwanakijiji,
Mimi ni mmoja wa hao Wapumbavu lakini pamoja na Upumbavu wangu nakuomba unipe somo kidogo pengine huo Upumbavu unaweza kuwa ujanja wa kibongo bongo..
Mkuu kwana nitaanza na kuelewa kwa nini kumekuwepo na mfumo wa vyama vingi duniani.. Swala hilo halitokani na wagombea Binafsi hata kidogo isipokuwa linatokana na itikadi za vyama kutofautiana. Watu ama viongozi hujiunga na vyama hivyo kutokana na kile kinacho simamia..Na ndio maana tuna mrengo wa kushoto, Kulia kati Kulia na kadhalika..Vyma vyote hufunguliwa kwa sababu wana imani tofauti kisiasa na chama ama vyama vilivyopo..Ndi tumekuta vyama kama vya Green Party na kadhalika ambavyo sio mtu anayejitangaza isipokuwa sera za hicho chama kusimamia malengo fulani..
Tatizo langu kubwa kuhusu haki ya wagombea binafsi ni pale wanapojaribu kuendeleza siasa ambazo sisi tunaoishi nje tunafahamu zinawapoteza wananchi...Yaani wananchi kuchagua wagombea kutokana na sifa zao badala ya kutazama nini chama hicho kimekusudia kuwafanyia wananchi..Na kwa bahati mbaya uchaguzi uliopita ulikuwa mfano bora wa uchaguzi wa mgombea kutokana na sura ama mfuko wake..
Kama hawa kina Mtikila wangekuwa wamesimama kutafuta haki ya wagombeaji binafsi ambao watawekewa sheria inayohusiana na kuonyesha sera zao tofauti na vyama vilivyopo bila shaka nadhani inaweza kukubalika lakini tusikubali KUIGA tu ile haki maadam wenzetu Ulaya wanaitumia wakati wao tayari wamekwisha shiba kisiasa na wana upeo mkubwa wa mrengo na sera ambazo vyama vikubwa wameziacha nje..
Ni kweli CCM wanaogopa hili lakini at the same time tusiwataze CCM hofu yao zaidi na kusahau maslahi yetu sisi wenyewe. Haki zote hupokelewa kulingana na mazingira na zipo haki ambazo Ulaya zinakubalika lakini kwetu Afrika inabidi tuzitazame mara mbili mbili kama zinalingana na mazingira yetu hivyo hivyo sisi tunazo haki ambazo hazikubaliwi Ulaya, hii haina maana kuna mtu anakosea.
Kwa mfano, kuna baadhi ya states zinaruhusu ndoa za Wasenge lakini hawakubali ndoa za kiislaam kuoa mke zaidi ya mmoja. Ndoa za Mkeka au kupangiwa na wazazi zinakubalika kisheria India na Asia na ni Haki ya mzazi lakini hazikubaliki nchi hizi hata kama wapo wazazi wanaopanga ndoa hizi..
kwa hiyo, tujaribu kutazama kilke kinachokubalika kwetu badala ya kutazama sheria za wenzetu Kuiga mfumo ambao kwanza haulengi tofauti za kimrengo na sera..
Kama utakumbuka niliwahi sema kuwa hadi leo hii Ukimuuliza Mdanganyika yeyote nini mrengo wa CCM watakwambia hawafahamu, hizo sera zao ndio zinachanganya kabisa maana wao ndio wameshika leo hii dira ya Kitaifa iliyoanzishwa na mwalimu... UJAMAA na KUJITEGEMEA, kisha wao ndio wa kwanza kuzivunja na wananchi ama washabiki wake wanaona poa tu maadam wachezaji wapo..
Kwa hiyo mkuu nitarudia kusema pamoja na Upumbavu wetu mimi nadhani haki ya wagombea binafsi bado muda wake itakuja wakati wake kwanza tujenge demokrasia kwa maana yake halisi.. Vyama vyote ni lazima viwe na mrengo kisheria ili kuwawezesha wananchi wajipanga nyuma ya vyama hivyo badala ya kutazama sura gani zipo chama gani..Lakini kwa hali iliyopo sasa hivi, wananchi tunashabikia vyama kama vile Yanga na Simba, mpira mmoja kiwanjani..Sura za wachezaji, rangi za jezi ndio kielelezo kikubwa cha kushabikia..
Hivyo mkuu binafsi naona kama tutakuwa tunazidi kujifukia ktk kiza kikubwa cha vyama vyetu nchini hata kama kuwepo kwa wagombea binafsi ni moja ya silaha kubwa kuivunja CCM...Kama walivyovunjika KANU ya Kenya halafu watu wale wale waliokuwa KANU wamekimbilia vyama vingine na baadhi (mafisadi) kushika tena madaraka..