Mzee Mkandara nimekusoma vizuri.
Zipo haki za aina nyingi lakini katika hili nitatofautisha haki mbili ambazo ni za msingi nazo ni haki za binadamu na haki za raia.
Haki za binadamu
Haki za binadamu ni haki ambazo mwanadamu yeyote yule anazo na anazo kwa sababu moja tu, ni mwanadamu. Haki ya kwanza ya mwanadamu ni haki ya kuishi. Haki ya pili ni haki ya kujitapatia maisha yake hifadhi na usalama. Na nyingine ni haki ya kujipatia mahitaji yake yatakayomwezesha kuishi. Sasa karibu mataifa yote yanatambua haki za binadamu na mataifa hayo yameridhia mkataba wa Kimataifa na wanatambua kile kinachoitwa Azimio la Umoja wa Mataifa Juu ya Haki za Binadamu. Unaweza kusoma Azimio hilo
HAPA
Sasa ukiangalia haki ambazo zinatambuliwa (haziundwi au kuwekwa na Umoja wa Mataifa) ni pamoja na:
Article 20.
(1) Everyone has the right to freedom of peaceful assembly and association.
(2) No one may be compelled to belong to an association.
Article 21.
(1) Everyone has the right to take part in the government of his country, directly or through freely chosen representatives.
(2) Everyone has the right of equal access to public service in his country.
(3) The will of the people shall be the basis of the authority of government; this will shall be expressed in periodic and genuine elections which shall be by universal and equal suffrage and shall be held by secret vote or by equivalent free voting procedures.
Sasa hizo ni haki za binadamu.
b. Haki za Raia.
Hata hivyo zipo haki za raia ambazo mara nyingi zinatokana na haki za binadamu. Lakini hizi ni haki ambazo zinatambuliwa na nchi fulani kwa raia wake. Kwamba ukiwa raia wa Tanzania una haki hizi na hizi na zile. Sasa hizi haki za raia ni haki ambazo huwezi kumfanya mgeni aziifurahie nazo. Miongoni mwa haki hizo ni pamoja na haki ya kupiga kura, kupata ajira, kuchagua kiongozi wake, n.k n.k Sasa haki za raia huwezi kumpa raia mmoja halafu ukamnyima mwingine. Ukitoa haki fulani kwa raia mmoja ni lazima raia mwingine naye awe na access ile ile.
Haki ya kuchagua unayetaka akuongoze:
Sasa haki ya kumchagua mtu unayetaka akuongoze ni haki ya kila raia na tumesema ataweza kutumia haki hiyo akiwa na miaka 18, na akili timamu na ambaye ndani ya muda fulani hakuwa mtu aliyekutwa na hatia ya kosa kubwa. Mtu mwenye kutimiza masharti hiyo basi anaweza kushiriki katika uchaguzi wa kumchagua, diwani, mbunge, Rais, n.k n.k Hivyo huwezi kusema upande huu wa Tanzania nyinyi mnaweza kumchagua mkiwa na miaka 18 halafu upande ule wa TAnzania wao waanze kupiga kura wakiwa na miaka 16. Raia wote wana haki sawa.
Haki ya kuchaguliwa kuongoza.
Katika hili tunasema kuwa raia wote wenye kutimiza masharti fulani basi wana haki ya kuchaguliwa kuongoza. Katika nchi yetu tumeweka mipaka; kwa upande wa wabunge tumesema kila raia mwenye akili timamu, na ambaye ametimiza miaka 18 na hajashtakiwa uhalifu ana haki ya kuchaguliwa kuongoza. Kwa upande wa Rais tumeongeza awe na angalau miaka 40 na awe hajachaguliwa Rais vipindi viwili huko nyuma.
Lakini kwa namna ya kushangaza tukasema lakini mtu huyo lazima awe mwanachama wa chama cha kisiasa. Hapo ndipo penye tatizo.
Ibara ya 20 (2) ya UDHR niliyoweeka hapo juu inasema mtu yeyote hatoshurutishwa kujiunga na chama chochote kile. Sasa kwa kusema anayetaka kugombea uongozi "lazima" awe mwanachama wa chama cha siasa tunavunja hiyo ibara. Kinachosemwa hapo ni kama kusema "mtu hatoingia kanisani hadi awe ni muumini wa parokia fulani" au kusema "mtu hatoingia msikitini hadi awe muumini wa msikiti fulani". Ukifanya hivyo ina maana unamlazimisha mtu ambaye hataki kuwa muumini katika msikiti wowote ule ajiunge na msikiti ili aweze kuingia msikiti mwingine.
Inakuwaje kama mtu anamuamini Mnyezi Mungu na Mtume wake na anataka aende kuswali anakopenda bila kuulizwa anatoka msikiti gani? Itakuwaje kama mtu anataka kwenye kusali Jumapili tu na anaamini Biblia nk lakini hataki kuwa chini ya mchungaji yoyote?
Sasa tatizo hili siyo la hiyo Ibara ya Umoja wa Mataifa tu bali pia tunaliona kwenye Katiba yetu kwani Katiba yetu na yenyewe inapigisha mwangwi kipengele hicho hicho. Inasema hivi: Ibara 20(4)
Bila ya kuathiri sheria za nchi zinazohusika ni marufuku
kwa mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote au
shirika lolote,
Sasa, ninachojengea hoja ni kanuni ya haki na sijagusia hata kidogo jinsi haki hiyo inavyoweza kufanya kazi katika Tanzania. On principle, serikali haina uwezo wa kufuta haki ya mtu kuchaguliwa kwa sababu hataki kujiunga na chama cha kisiasa.
Je twaweza kuwa na wagombea huru?
Ndiyo. Tukikaa chini tunaweza kufikiria ni jinsi gani mgombea huru katika Tanzania anaweza kugombea. Tunaweza kufanya kwa kuangalia levels za uongozi na hivyo kuona kuwa kizingiti cha kugombea kama mtu binafsi kinakuwa kikubwa zaidi unapopanda ngazi za juu lakini bila kufanya kiwe kikubwa hadi kigeuke kuwa kizuizi.
Pia tukumbuke kuwa tunaposema mgombea huru hatuna maana asiye na chama bali hata mwenye chama ambaye hataki kugombea kupitia chama chake au chama chake hakikumpa nafasi ya kugombea lakini anaamini wananchi wanamtaka.
Hebu tuangalie kwenye level mbalimbali. Pamoja na mtu kutimiza masharti ya mpiga kura, mgombea huru katika nafasi zifuatazo afanyiwe hivi:
a. Udiwani:
- Awe ni mkazi wa eneo hilo kwa angalau miaka mitatu mfululizo
- Apate wadhamini angalau asilimia 30 ya wakazi wa eneo hilo
- Kila mdhamini awe amewahi kuwa mkazi eneo hilo angalau miaka 2
- Awe na Ilani yake (platform) na ilani hiyo isiwe kinyume na Katiba ya nchi au sheria.
- Ilani yake iwe na wadhamini angalau wa tano ambao watatia sahihi kuwa haipingani na sheria.
- Aunde timu ya timu ya watu wasiozidi 20 kusimamia kampeni yake na hakuna mipaka kwa wale watakaofanya hivyo kwa kujitolea. Wale ishirini lazima wajulikane kwa tume.
- Afungue mfuko wa mgombea ambao utaonesha wachangiaji na matumizi ni nini. Kwa mgombea atakayepoteza nafasi yake, fedha hizo anaweza kuzitumia kuanzisha mfuko wa jamii wa eneo analotoka au kuziweka dhamana kwa ajili ya mfuko wa kampeni ya mgombea atakayemuunga mkono.
b. Ubunge:
- Awe ni mkazi wa jimbo husika kwa angalau miaka mitatu
- Awe na wadhamini angalau asilimia 20 ya kura za maoni
- Wadhamini hao wawe ni wa kazi wa eneo hilo kwa angalau miaka miwili mfululizo
- Awe na timu isiyozidi watu 50 kusimamia kampeni yake na wajulikane kwa NEC. Kwa wale wanaojitolea hana mipaka.
- Awe na Ilani yake inayofafanua agenda yake kwa wapiga kura wake na Ilani hiyo isipingane na Katiba au Sheria za nchi. Ilani hiyo lazima ipitishwe na Mahakama ya Wilaya Ilani hiyo idhaminiwe na angalau watu 20 wa Jimbo lake hilo kwa kuweka sahihi zao kuwa wanakubaliana nayo.
- Kama ni mwanachama wa chama cha siasa akichaguliwa hatotakiwa kuwa chini ya nidhamu ya chama chake.
c. Urais
- Apate udhamini wa watu 150 na kutoka kila mkoa angalau wananchi wasiopungua wasiopungua 5 kutoka kila mkoa.
- Awe na timu ya watu wasioziidi 50 kusimamia kampeni yake na hana mipaka katika wale wanaoijitolea
- Awe na Ilani yake ya mgombea ambayo itapitiwa na Jaji yeyote wa Mahakam Kuu.
- Lazima awe na mgombea mwenza ambaye atatoka upande mwingine wa Muungano.
- Kama ni mwanachama wa chama cha siasa akichaguliwa hatotakiwa kuwa chini ya nidhamu ya chama chake.
Well.. kuna ubaya gani kufikiri vitu kama hivi badala ya kuamua kufuta tu haki ya mtu? Ndio maana nakubaliana na kauli kuwa serikali kuamka na kufuta haki ya mtu kwa vile haiipendi haki hiyo ni uamuzi wa kipumbavu.