Kupisha machungu ya ndugu kupotezwa au kuuawa kwa sababu za kisiasa kwanini tusikubaliane walioko madarakani wadumu milele?

Kupisha machungu ya ndugu kupotezwa au kuuawa kwa sababu za kisiasa kwanini tusikubaliane walioko madarakani wadumu milele?

Nakubaliana nawe.Tusikaze sana shingo.Ngoja waendelee mpaka wachoke

Kimsingi ni heri tukubaliane hawako tayari kwa lolote si uchaguzi wala demokrasia.

Kwamba yawezekana demokrasia si kwa manyani kama demokrasia ni kwa binadamu?

Ya nini kupotezeana muda, uhuru hadi maisha Bure?
 
2pac once said," The death is not the great loss in life. The great loss in life is what dies inside you when you're still alive"
 
Njia pekee ya kuwatoa ni mapinduzi ya kijeshi, jee tunao askari wazalendo wa kuweza kuikomboa nchi toka kwa hawa makaburu weusi ccm?
Bahati mbaya sana mapinduzi ya kijeshi ( coup d'etat) hayajawahi kuleta matokeo chanya Afrika.

Imethibitika wapinduaji baadae hung'ang'ania kubaki madarakani bila ya kikomo hata kama wakati wanapindua walisema watarejesha utawala kwa kiraia.

Madikteta wengi Afrika waliingia madarakani Kwa mapinduzi. Tujiulize tunashindwaje kuilazimisha CCM iheshimu uchaguzi na matokeo yake?
 
Hawa wendawazimu wamenogewa na staili ya Magufuli ya kuengua wapinzani na mwakati watafanya kama walivyofanya 2020 ili waendeleze bunge la kijani tupu na watazidi kutunga sheria kandamizi zaidi ili waendelee kutawala. CCM wamekataa ustaarabu wa kuheshimu maoni ya Watanzania kupitia sanduku la kura hivyo kuwaondoa madarakani ni lazima kwa nguvu. CCM imekoma kuwa chama cha siasa na imekuwa ni genge la kigaidi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendeleza utawala wao wa kidhalimu.
 
Hahaha mkubaliane na nani na iko hivyo tangu mwanzo, kumbe wewe ulitaka kuwatoa madarakani?

Angalia usitekwe na kuuwawa ccm hawana utani kwenye hilo.
 
Ni machungu kiasi gani kwa familia za waliopotea au kuuwawa kwenye kadhia hizi za kisiasa?

Ni familia ipi inaweza kuhalalisha unyama huu kutokea katika familia yao?

Imekuwa ni kawaida watu kupotea au kuuwawa kwa sababu za kisiasa, huku kukiahidiwa chunguzi zisizokuwa na majibu.

Kama haya yanatokea na tatizo ni dhana ya demokrasia na utawala jumuishi tu, kutokuwa zimeridhiwa vilivyo?

Kwamba kama waliopo madarakani wakiachwa watawale milele ndiyo suluhisho la haya?

Kwa hakika kupisha machungu ya namna hii ipendekezwe walioko madarakani waendelee kutawala hadi watakapojichokea!

Naomba kutoa hoja.
Mimi nilishawahi kumwambia jamaa siku moja, ifike hatua wanaojihusisha na siasa waachane nayo hasa vyama pinzani vikubwa harafu tuangaliane
 
Ni machungu kiasi gani kwa familia za waliopotea au kuuwawa kwenye kadhia hizi za kisiasa?

Ni familia ipi inaweza kuhalalisha unyama huu kutokea katika familia yao?

Imekuwa ni kawaida watu kupotea au kuuwawa kwa sababu za kisiasa, huku kukiahidiwa chunguzi zisizokuwa na majibu.

Kama haya yanatokea na tatizo ni dhana ya demokrasia na utawala jumuishi tu, kutokuwa zimeridhiwa vilivyo?

Kwamba kama waliopo madarakani wakiachwa watawale milele ndiyo suluhisho la haya?

Kwa hakika kupisha machungu ya namna hii ipendekezwe walioko madarakani waendelee kutawala hadi watakapojichokea!

Naomba kutoa hoja.
Hiyo ni kumsusia fisi bucha
Tutawathibiti muda ukiwadia
Wacha wajilshe upepo waendelee kujiona wajanja
 
Muovu anapofanikiwa usimwonee wivu, kila teneo linahesabiwa na kulipwa hapa Duniani.
Hii dhana ya malipo ni hapa hapa duniani hutumiwa na wanyonge baada ya kushindwa mpamabano.

Wazungu walitutawala kwa mijeredi na vipogo vya risasi mbona hawajalipwa mabaya hadi leo? Au wao hii dhana haiwahusu?
 
wakoloni waliacha tawala za mitaa kwa machifu na watwale, watwale walichaguliwa na DC na kuidhinishwa na machifu, huu utaratibu wa watu kugombea ilikuja baada ya mwalimu kufuta uchifu. sasa hili la kampeni za uongozi wa mtaa kufanywa kichama sijui hili jambo la hovyo nani alilileta.

mimsingi uongozi wa kijiji ungefaa ufanywe kwa kugombea pasi kufuata ushawishi wa kichama, jamii ndogo ya mtaa kusema huu nibuongozi wa ccm na ule wa cdm na ule wa chauma tunapanda mbegu ya kishenzi sana.

fikiria kimara iwe ya ccm mbezi iwe ya chadema goba iwe ya act wazalendo tunatengeneza mfumo ambao mbeleni nchi haitatawalika. leo cdm inalalamika ccm kuua watu wao hiyo mitaa iliyoko chini ya cdm wana ccm watakaa kwa utulivu kweli?

napendekeza uongozi wa mtaa upatikane pasipo kufuata itikadi za vyama mtu agombee yeye kama yeye. hii itaondoa mgawanyiko wa kisiasa ngazi ya mtaa

hili la mtu kutoka ubelgiji anaenda kupiga kampeni ikungi na wala sio mpiga kura kwenda kuleta fujo tu, mwingine anatoka dar anaenda kazuramimba, mwingine anatoka dar anaenda shinyanga mbaya zaidi wengine ni mawaziri. huku ni kuleta taharuki tu zisizokuwa na maana yeyote.
 
Njia pekee ya kuwatoa ni mapinduzi ya kijeshi, jee tunao askari wazalendo wa kuweza kuikomboa nchi toka kwa hawa makaburu weusi ccm?
tatizo la kijeshi wakishaitoa ccm hautawapangia nani atawale na atawale vipi? wanaweza baki ccm haohao katika mfumo wa kijeshi
 
Njia pekee ya kuwatoa ni mapinduzi ya kijeshi, jee tunao askari wazalendo wa kuweza kuikomboa nchi toka kwa hawa makaburu weusi ccm?

Mapinduzi huwa si ya kijeshi peke yake.

Kulikoni kuwekeza matarajio kutokea kwenye jitihada za wengine?
 
Nakubaliana nawe.Tusikaze sana shingo.Ngoja waendelee mpaka wachoke

Hatua hii ilikuwa ni njema sana kuwafahamisha kwa vitendo wenye kudai hawajawahi kuuwa hata nzi, kuacha kuendelea kutucheza shere.
 
2pac once said," The death is not the great loss in life. The great loss in life is what dies inside you when you're still alive"

Kutegemea quotes za wala unga kama kina Tupac ni sawa na kutegemea quotes za kina Amber kutuvusha.

Hudhani labda sana sana zingekuwa kama za kina Nyerere, Maalimu, Tutu, Lissu, Maalimu, Museveni, Kagame, Samora, Mugabe au wa namba hiyo waliokuwa tested kwenye field?
 
Back
Top Bottom