Kupitia Corona Serikali za Dunia inabidi zijifunze kwamba afya ndio mtaji wa nchi kujiendesha

Kupitia Corona Serikali za Dunia inabidi zijifunze kwamba afya ndio mtaji wa nchi kujiendesha

Hivi unajua kuwa waliomba ubalozi wa China kuwa wanataka kupeleka madaktari China kwenda kutoa msaada?
 
Wataalamu tupo tatizo ni selekali kutokutenga budget kwa ajili ya research lab ya dawa na magonjwa,
Kwa mfano mim nimesoma jinsi ya kutengebeza chanjo kwa kutumia purified virus rakin hakuna sehemu ya kuiapplay

Sent using Jamii Forums mobile app
Uko sahihi kabisa !!

Hatujawekeza vya kutosha kwenye tafiti hasa kuhusu afya.
 
Mbona kuna yule Dr. Rahabu Lubago wa Kiomboi Kisiriri pale Buguruni sheli, aligundua dawa ya vidonda vya tumbo na ikawa imeidhinishwa na wizara ya afya na TFDA itumike na mzigo ukaingia sokoni fuleshi tu.
 
Mazingira ya kufanya majaribio ya kutafuta kinga(chanjo) au tiba ya magonjwa mapya kwa Tanzania sio rafiki. Facilities na pesa Ni mtihani.

Serikali imewekeza katika kutibu tu. Miundombinu inayoboreshwa Ni kwa ajili ya kuwezesha wataalamu wa afya kutoa huduma kwa wagonjwa basi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna hospital kubwa sana hapa nchini n ya serikali nilikuwa na mueleza tatizo langu LA kiafya yule daktari kabaki anashaangaa ananiambia APA Tanzania amna matibabu yake mpaka uende ulaya,,,,tena n specialist uyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tofauti na malalamiko, we we ushabuni nini?. Hakuna nchi inayojitosheleza wala kujitegemea kwa kila kitu, hata Marekani na China pamoja na maendeleo yao, bado ni tegemezi kwa nchi zingine katika baadhi ya mambo.
Ndomaana Marekani pamoja na ubabe wake, hutafuta suruhu kwa Korea, Iran, China na Urusi.
Umeshakuwa MTU mzima sasa, acha malalamiko, saidia nchi yako, Mjenga nchi ni Mwananchi
Amebuni kulalamika lalamika nyuma ya keyboards

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tofauti na malalamiko, we we ushabuni nini?. Hakuna nchi inayojitosheleza wala kujitegemea kwa kila kitu, hata Marekani na China pamoja na maendeleo yao, bado ni tegemezi kwa nchi zingine katika baadhi ya mambo.
Ndomaana Marekani pamoja na ubabe wake, hutafuta suruhu kwa Korea, Iran, China na Urusi.
Umeshakuwa MTU mzima sasa, acha malalamiko, saidia nchi yako, Mjenga nchi ni Mwananchi
Mleta mada anahoja ya msingi, sasa kama kila siku wanafanya research lakini hawajawahi kugundua dawa yoyote au ni uongo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona wanaotengeneza vipodozi,sabuni,mafuta ya ngozi,wao wanatengeneza na mzigo unaingia sokoni,vipi wao tafiti wanazifanyia wapi? au kwakua uhai wa binadamu ni tofauti na vipodozi,sabuni na mafuta ambavyo yana pakwa juu ya ngozi pekee
 
Readiness to calamities is very relative in the world leave along the claimed first world countries
 
Tofauti na malalamiko, we we ushabuni nini?. Hakuna nchi inayojitosheleza wala kujitegemea kwa kila kitu, hata Marekani na China pamoja na maendeleo yao, bado ni tegemezi kwa nchi zingine katika baadhi ya mambo.
Ndomaana Marekani pamoja na ubabe wake, hutafuta suruhu kwa Korea, Iran, China na Urusi.
Umeshakuwa MTU mzima sasa, acha malalamiko, saidia nchi yako, Mjenga nchi ni Mwananchi
Ndio maana hatuendelei, kila kitu tunachukulia kisiasa! unataka kufananisha Tanzania na hizo nchi ulizo zitaja hapo? unauliza mimi nimebuni nini! wao wamebuni nini? research Tangu uhuru! hakuna kilicho buniwa!
 
Tumewekeza nguvu kubwa sana ya pesa na miundombinu kusomesha watu wetu. Tumetoa mamia ya "wanasayansi".

Mpaka muda huu sijasikia angalau mwanasayansi mmoja kutoka Tanzania akitupatia japo matumaini ya jitihada zao katika kutafuta kinga dhidi ya corona.

Wote wako kimya. Tunamsubiri mzungu.

Tanzania haijulikani mwanasayansi nani wala ngumbaru nani. Ni kama wote hatukwenda shule.

Wakemia wote hoi. Hakuna hata jitihada za kuchanganya madawa huko maabara wapate chochote cha kututia matumaini.

Hivi huwa wanashughulika na nini haswa hawa wanasayansi wetu!

Kwanza, hivi Tanzania tuna "wanasayansi" (just to begin with)?

Wana shughuli gani haswa hawa "wanasayansi" wa hii nchi?

Hata kufurukuta furukuta tu hakuna angalau tujue wanafanya kitu cha kututia moyo?

Wameshindwa japo tu kutambua kwamba klorokwini ina uwezo wa kufubaza corona?!
Afrika Mashariki combined hakuna mtu hata mmoja anayeweza kutoka kifua mbele kukiwa na kusanyiko la wanasayansi duniani labda sisi tunao wanasayansi wa kukandamiza upinzani na kujilimbikizia mali

Wengi ni bookish tu
 
Niliwahi kuandika hapa, nchi pekee ya kiafrika/weusi yenye wanasayansi ni Nigeria labda na ghana na South Africa.Wengine tumesomea sayansi tu.Likija suala la tafiti hutia visingizio Vingi sana na kuilaumu serikali.

Serikali ta sasa hivi in PhD ya sayansi lakini hakuna cha maana kilichobadirika.
Project za wahitimu mqaka was 3 sayansi hupewa 150000 sijui kama imeongezeka.Sasa ni ugunduzi gani uraufanya kwa lKi na nusu.

Watanzania hawana muda wa kuboresha maabara ziwe za kisasa wanadai ni jukumu la serikali.Kila Kaya ina shule lakini kutest udongo wa shamba la mkulima mpaka upelekwe taasisi za utafiti(huu ni utani!!).
 
Kupitia Corona Serikali za Dunia inabidi zijifunze kwamba AFYA NDIO MTAJI WA NCHI KUJIENDESHA;

Ndio, yaani inabidi huduma za afya zitolewe bure na zigaramiwe na serikali.

Serikali za dunia mpaka sasa zimeshuhudia hasara kubwa sana kutokana na janga la CORONA, kwamba watawaliwa hawafanyi kazi, mfano shule zimefungwa na mikusanyiko ya hela hakuna n.k

Hii inamaana kwamba HAKUNA UZALISHAJI HUKU SERIKALI ZIKITEGEMEA KODI.

Sasa serikali zinaingia gharama za kununua madawa kwa bajeti isiyopangwa.

Maana yangu ni kwamba Serikali za dunia kama zitagaramia huduma zote za afya haswa matibabu ya KANSA, FIGO, UPASUAJI MBALI MBALI na magonjwa yote MAKUBWA KAMA MOYO, maana yake ingetengeneza mtaji afya wa walipa kodi wengi ambao wasingepoteza muda wao kuhangaika na matibabu badala yake wanapona wanaingia mtaani.


Mfano niliwahi kuisikia taasisi 1 ya moyo inasema 'KUTIBU MOYO HUANZIA MILIONI 15- 30'

Rafiki yangu mmoja alienda India akatibiwa figo kwa milioni 36 jumlisha nauli n.k

SERIKALI ZA DUNIA HASWA ZA AFRIKA ZITOE MATIBABU BURE KWA WANANCHI WAKE, NCHI KAMA TANZANIA INAWEZA KABISA KWA KUTUMIA RASILIMALI WALIZO NAZO.

(kuna wakati nikitumia sanitaza huwa naandika point)

View attachment 1393127

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakubaliana nawe 100%
Bora wastuke sasa hasa hapa kwetu tz ambako unamdai mtu hata kama amepona na ni maskini ati anazuiwa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuwa ni kwamba kiongozi yeyote wa kiafrika akiugua kidogo tu, ataondoka na kundi kubwa la wasaidizi kwenda nchi za ulaya kutibiwa. Walisafiri kwa anasa, waliishi kwa anasa na kutumia gharama kubwa kutibiwa.

Inashangaza, ghafla baada ya kuzuka kwa Korona, wote wamepona na kutulia nchini. Licha ya yote, hakuna ncho yoyote inayoweza kupokea mgonjwa wa korona toka nchi za kiafrika. Kwa maana hiyo dawa iliyobakia, ni hawa viongozi kutumia zile fedha za safari na anasa katika kuboresha huduma za afya mapema, vinginevyo watapukutika kama panya.
 
Back
Top Bottom