Kupitiliza muda wa kujifungua

Kupitiliza muda wa kujifungua

Mapondo Mapoka

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2015
Posts
269
Reaction score
121
Naombeni msaada kwa wajuzi na wazoefu.

Mke wangu kapitiliza muda wa makadirio ya kujifungua wiki 40 kwa mujibu wa ultrasound.

Toka wiki iliopita mpaka sasa anapata dalili kama uchungu lakini unakata, au akienda zoezi la kutembea akikaa tu hali kama ya uchungu humjia na kutoweka. Sasa ni takriban siku 8 ambazo zimepitiliza wiki iliopita tulienda hospitali na alifanyiwa ultrasound na hakuna dalili yoyote mbaya ilioonekana majibu yalikuwa mazuri.

Kwenu wajuzi, hali hii ya dalili kama uchungu unaokaa muda mfupi na kutoweka inaashiria nini?
Naombeni msaada kwani mke wangu anamawazo mengi sana juu ya hili kiasi cha kunipa hofu kidogo na mimi.

Karibuni wadau.
 
Poleni, kwa hali kama hiyo mngeenda hospital kwa daktari wake ili amshauro japo inaweza kwenda hadi 42 weeks zaidi ya hapo itabidi aanzishiwe uchungu.
Ila daktari anaweza kushauri zaidi.
Akazane mazoezi ya kutembea squats (kuchuchumaa) na kucheza mziki kama anapenda. Pia ale mananasi na spicy foods na chai ya rangi hivi vinaanzisha labour.
Asije akajaribu castor oil -imasaidia lakini haishauriwi imaweza sababisha kifo.
Poleni, kikubwa tuombe Mungu amsimamie ajifungue salama na apate mtoto mwenye afya njema. I feel your fear been there!
 
Mazoezi yanaweza yasimsaidie, aende hospitali gynecologist wake ata mshauri wa mu induce labor. Na ikishindikana kuzaa kawaida wamfanyie c-section.
Madhara ya kupitiliza siku 40 za kujufungua, unaweza ku google utayaona. Sio lazima ajigungue kawaida, hakuna kombe utakalopewa, cha msingi kaokoe maisha ya mama na mtoto.
Fanya hivyo haraka usipoteze muda kwa afya njema ya mwanao.
 
Aiseeee!!! Aende hospital.. Wengine huwa wanaanza kwa kupata false labour ...
Uchungu unakuja then unakata
 
Kupitiliza kujifungua yaweza fika hadi wiki2.Cha muhimu kuzingatia ni afya ya mama na mtoto aliyetumboni.
Hiko kinachomtokea(uchungu kuja na kukata)wenyewe wanaita false labour ni sawa na kusema uchungu wa uwongo.
Mpeleke hospital kwa ushauri zaidi
 
Back
Top Bottom