Kupokea pesa kwa Wire Transfer

Kupokea pesa kwa Wire Transfer

Evvy jr

Senior Member
Joined
Apr 23, 2017
Posts
148
Reaction score
189
Habari zenu wana jamvi,

Naomba kufaham kwa mwenye uelewa kuhusu wire transfer. Huchukua siku ngapi kwa pesa iliyotumwa kutoka nje ya nchi kwa njia ya wire transfer kukufikia kwenye account yako ya bank hapa nyumbani?

Kuna mtu niliekua namtumia mzigo mara kwa mara nje lkn pesa ilikua ikitumwa inaingia moja kwa moja kwenye simu (airtel money) wakati huohuo, lakn safari hii kachukua mzigo ambao ni mkubwa kidogo hivo pesa imeongezeka na ikashindikanaa kutuma kwa sim ikabid atumie njia ya bank (wire transfer) na leo ni siku ya tatu sijapata sms ya bank kuonyesha pesa imeingia.

Siku zote huwa mpaka pesa iingie ndio namtumia mzigo, so mpaka sasa mzigo sijatuma nikisubiria hiyo pesa, kinachonipa wasiwasi mzigo ukikaa mda mrefu unapoteza ubora wake na siwezi kutuma bila kuona hiyo pesa.
 
Habari zenu wana jamvi,
Naomba kufaham kwa mwenye uelewa kuhusu wire transfer. Huchukua siku ngapi kwa pesa iliyotumwa kutoka nje ya nchi
Kwa kawaida inachukua siku 3-5 za siku ya kazi ukitoa weekend, lakini pia inaweza kuwahi kutengemeana na nchi kuna pesa uwa nalipwa kutoka USA kwa wire transfer ndani ya masaa 24 mzigo unakuwa umeingia, mwambie akutumie swift copy ya benki ili zikipita siku kadhaa bila kuiona unaenda kwenye bank yako na ushahidi wa hiyo slip.
 
Habari zenu wana jamvi,
Naomba kufaham kwa mwenye uelewa kuhusu wire transfer. Huchukua siku ngapi kwa pesa iliyotumwa kutoka nje ya nchi kwa njia ya wire transfer kukufikia kwenye account yako ya bank hapa nyumbani?
Uwa ni siku 3 mpaka 5 business days ndivyo wanavyosema officially, ila mimi CRDB kesho yake tu jion salio linasoma
 
Kwa kawaida inachukua siku 3-5 za siku ya kazi ukitoa weekend, lakini pia inaweza kuwahi kutengemeana na nchi kuna pesa uwa nalipwa kutoka USA kwa wire transfer ndani ya masaa 24 mzigo unakuwa umeingia, mwambie akutumie swift copy ya benki ili zikipita siku kadhaa bila kuiona unaenda kwenye bank yako na ushahidi wa hiyo slip.

Hata mimi inatoka US sijajua kwa nn imechukua muda! Itabidi baada ya siku tano niende ofisini kwao
 
Kwa wazoefu, pesa kutoka Netherlands huwa mnaipata baada ya siku ngapi kupitia CRDB Bank?
 
Back
Top Bottom