Kuporomoka kwa Bei ya Brevis

Mkuu V6 petrol Toyota Kwa 13km/l sio kamba kweli?
 
Gari kwenye picha ni za 2004, Kodi umeweka mwaka 2007
 
Si vema kupost magari ya watu humu ila unakuta Brevis namba DL.. inasoma 7.5M na Brevis namba DF... inasoma 7M kitu ambacho ni ngumu kukuta IST ya namba hizo ikiuzwa kwa bei hiyo

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
IST inapendwa Sana na Hawa vijana wanaofanya Uber, bolt,paisha,indrive nk
Nadhadi kwakuwa ulaji wake wa mafuta mdogo ndio maaana
 
Zinakula wese ni hatar, kuna mdau kapark ndani ananipigia kila day chukua hiyo gari endesha tu hapo mjini utambie

Namwambia hapana hii gari ni chuma ulete inakausha damu hatar

Mana nikiwa naye katika misere mara kaweka wese la 60k mara kaongeza 30k

Najisemea hiiiiiii, bora nipande daladala mia tano kuliko kukikausha damu kiasi hiki.
 
Watu wanapenda kitonga.. Brevis ni mnyama ni gari ya kazi kama una mkono wa birika ni ngumu kuimiliki

Sent from my LM-V500N using JamiiForums mobile app
 
Nlimaanisha izo used, kuna watu wanazichukua hivyo hivyo na changamoto zake
Kama wamkoani sawa.....waulize wamiliki wa hizogar wanavyopata tabu kupata wateja....madalali wanaongea maneno yote na bado kupata mteja ni ishu, kuna mzee alikuwa nayo DB alikosa mteja hapa Dar madalali wakamletea mteja katoka mkoani akaichukua kwa 5 na ilikua kali...sijajua kwann watu wa mkoani wanazielewa sana...sijui ni kwasababu ya bei kuwa chin maana mapya hawayanunui.

Kuna mshikaji wangu alikuwa na Crown athlete namba DL alipata nayo ajali upande wa mbele akaamua kuisukuma kwa 7....nakubuka walengaji kidogo wazichape maana kila mtu anaitaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…