Habari zenu wadau,
Kwa kipindi hiki cha mvua za dar nimepotelewa na academic certificate ya kidato cha nne japo sijajua katika mazingira gani ila ni katika hekaheka za kuweka mambo sawa....
Sasa naomba nisaidiwe nifanyeje ili niweze kurenew cheti na process zake zikoje....
Tafadhar naomba mnijuze.
fanya hivi 1. Nenda polisi kapate Police Loss statement.( Uipige kopi pia) Necta watahitaji kopi
2. Nenda magazeti ya serikali (yana bei chee kidogo) katoe tangazo la kupotelewa cheti huku likiwa na picha yako, likionesha cheti cha mwaka gani na namba ya mtihani wako. Ukienda leo baada ya siku tatu ivi litakuwa limetoka gazetini na unapiga kopi ukurasa mzima wenye lile tangazo (sio kipisi cha tangazo-ukurasa mzima)
3. Ingia mtandaoni
www.necta.go.tz tafuta sehemu pameandikwa fomu mbalimbali tafuta fomu ya maombi ya statement. Printi ile fomu na uijaze kadiri inavyoelekeza. Kumbuka statement haupewi mkononi mwako, inapelekwa kule mahala cheti chako kinahitajika so ukimaliza process pale wao NECTA ndio watakaopeleka huko cheti chako kinakohitajika (MAMLAKA INAYOHITAJI na SIO MTU BINAFSI) iwe m.f. Vice Chancellor UD au Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya, kuna sehemu ya kujaza hizo information kwenye fomu hiyo.
4. Nenda Benki kalipie sh 10,000 au zaidi kutegemea na uharaka wako hapo utaitaji kulipa kama 21600 kwa EMS kwenda mkoani. Ila kama ni DAR ni 15,000 kwa EMS kama nakumbuka vizuri. Chukua Bank pay in slip na copy yake na fomu yako nenda NECTA.
Ukienda kule uwe na picha 2 passport size, copy ya kitambulisho chako kinachofahamika, Kura, Bima ya Afya, Cha kazi, passport labda, ila sio kadi ya benki watakukatalia. Hapo mchezo kwisha ukifika pale unaikabidhi tu. Mchezo kwisha.
Kumbuka Tangazo la gazeti ulihifadhi vizuri pamoja na original ya police loss report, as utavitumia siku nyingine ukihitaji cheti chako kiende sehemu nyingine, una utaratibu huo ndo utaufanya mara zote. YALINIKUTA NDO MAANA NAJUA KILA KITU. Na bahati mbaya kama huna hata copy hapo utapata tabu maana utaenda NECTA mara nyingi zaidi. Unahitaji ushauri zaidi leta maneno. Nimejitosheleza?