Kupotea kwa cheti cha kidato cha nne (academic certificate)

Kupotea kwa cheti cha kidato cha nne (academic certificate)

makua

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2013
Posts
208
Reaction score
39
Habari zenu wadau,
Kwa kipindi hiki cha mvua za dar nimepotelewa na academic certificate ya kidato cha nne japo sijajua katika mazingira gani ila ni katika hekaheka za kuweka mambo sawa....
Sasa naomba nisaidiwe nifanyeje ili niweze kurenew cheti na process zake zikoje....

Tafadhar naomba mnijuze.
 
Nijuavyo mie cheti kinatolewa mara moja tu
ukipoteza huwa wanatoa barua tu za kukuthibitisha kuwa ni kweli ulimaliza shule na ukapewa cheti
ila kwa uhakika zaidi nenda katoe taarifa polisi then utapewa maelekezo pole....
 
Katoe taarifa polisi, upate polisi report na risiti (unalipia tzs 500/=)

then unaenda necta, ofcourse watakuambia ukatoe tangazo kwenye gazeti la serikali na baada ya siku 21 unarudi kwao wanakuandikia barua. Kila wakati ukihitaji kutumia cheti watakupa barua ya kupeleka unakotaka.

kama haukumbuki namba yako ya mtihani na ya shule unaanzia necta wakupatie. Pole baba.
 
Habari zenu wadau,
Kwa kipindi hiki cha mvua za dar nimepotelewa na academic certificate ya kidato cha nne japo sijajua katika mazingira gani ila ni katika hekaheka za kuweka mambo sawa....
Sasa naomba nisaidiwe nifanyeje ili niweze kurenew cheti na process zake zikoje....

Tafadhar naomba mnijuze.

fanya hivi 1. Nenda polisi kapate Police Loss statement.( Uipige kopi pia) Necta watahitaji kopi
2. Nenda magazeti ya serikali (yana bei chee kidogo) katoe tangazo la kupotelewa cheti huku likiwa na picha yako, likionesha cheti cha mwaka gani na namba ya mtihani wako. Ukienda leo baada ya siku tatu ivi litakuwa limetoka gazetini na unapiga kopi ukurasa mzima wenye lile tangazo (sio kipisi cha tangazo-ukurasa mzima)
3. Ingia mtandaoni www.necta.go.tz tafuta sehemu pameandikwa fomu mbalimbali tafuta fomu ya maombi ya statement. Printi ile fomu na uijaze kadiri inavyoelekeza. Kumbuka statement haupewi mkononi mwako, inapelekwa kule mahala cheti chako kinahitajika so ukimaliza process pale wao NECTA ndio watakaopeleka huko cheti chako kinakohitajika (MAMLAKA INAYOHITAJI na SIO MTU BINAFSI) iwe m.f. Vice Chancellor UD au Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya, kuna sehemu ya kujaza hizo information kwenye fomu hiyo.
4. Nenda Benki kalipie sh 10,000 au zaidi kutegemea na uharaka wako hapo utaitaji kulipa kama 21600 kwa EMS kwenda mkoani. Ila kama ni DAR ni 15,000 kwa EMS kama nakumbuka vizuri. Chukua Bank pay in slip na copy yake na fomu yako nenda NECTA.

Ukienda kule uwe na picha 2 passport size, copy ya kitambulisho chako kinachofahamika, Kura, Bima ya Afya, Cha kazi, passport labda, ila sio kadi ya benki watakukatalia. Hapo mchezo kwisha ukifika pale unaikabidhi tu. Mchezo kwisha.

Kumbuka Tangazo la gazeti ulihifadhi vizuri pamoja na original ya police loss report, as utavitumia siku nyingine ukihitaji cheti chako kiende sehemu nyingine, una utaratibu huo ndo utaufanya mara zote. YALINIKUTA NDO MAANA NAJUA KILA KITU. Na bahati mbaya kama huna hata copy hapo utapata tabu maana utaenda NECTA mara nyingi zaidi. Unahitaji ushauri zaidi leta maneno. Nimejitosheleza?
 
Sisera imagine kama unataka utumie statement of results katika sehemu mbili kwa muda huohuo Necta watatuma kote? Mfano; unaply TCU pia unaomba mkopo Loan board, hapo inakuaje?
 
Last edited by a moderator:
Dah......basi kazi ninayo,huo mlolongo....
Nashukuru kunijulisha wapendwa.

Swali lingine, je kama nikitumia njia ya kureseat mtihani wa form four sitawezapata cheti kingine?
Maana hata procedure za kureseat sizijui coz sijawahi......

Nawasilisha
 
Yes. Na hata wakati unatafuta kazi, kila unapoomba lazma uwaeleze necta na wao ndio watatuma hivyo vyeti. Yaani ni hustle!

hata sis tuna kazi wale wa vyeti vyetu vilivoungua pale ifunda tech mwaka jana, yaan nateseka pamoja na kwamba uzembe ulisababishwa na shule ,hawakuweka vyeti kweny safe box,
 
Yes. Na hata wakati unatafuta kazi, kila unapoomba lazma uwaeleze necta na wao ndio watatuma hivyo vyeti. Yaani ni hustle!

kuna umhimu mtu kuscan vyeti na kuweka kwenye mitanda mfano unaweza kuiweka hata kwenye email hata ikupotea hutateseka sana kama huna kabisa...
 
Kuna dogo alipoteza cheti chake cha kurist form 4, lakin akatumia result slip kuomba chuo akachukuliwa, lakin aliattach kile original chenye credit 2 na slip ya kurist yenye credit 1, ndo cjajua kama result slip iko invalid inakuaje hapo?
 
uko sawa kabisa. tengeneza folder hata kwenye skydrive uweke vyeti. lakini cheti cha form four na form six huwa sio issue ukishakuwa na uzoefu kazini walau wa miaka kadhaa. labda uwe unaomba kazi kwa JK ndo hajiamini anataka hata cha std 7
kuna umhimu mtu kuscan vyeti na kuweka kwenye mitanda mfano unaweza kuiweka hata kwenye email hata ikupotea hutateseka sana kama huna kabisa...
 
Sisera imagine kama unataka utumie statement of results katika sehemu mbili kwa muda huohuo Necta watatuma kote? Mfano; unaply TCU pia unaomba mkopo Loan board, hapo inakuaje?

Hata kama ni sehemu 10 wanakutumia tu, hela yako tu ya kupost. Mimi niliapply vyuo sita wakapeleka kote na nikapata chuo. Nilipomaliza chuo nikaaply kazi sehemu 5 wakapeleka kote. There are some good guys pale kwenye ofisi yao pale getini nadhani wanasema namba tatu. Japo kuna siku nyingine unaweza kukutana na sura ngumu haikupi ushirikiano, ila wanafanikisha tu, hadi dada mmoja anayeshughulikia nime crame jina lake. Ukilitaka njoo PM.
 
Dah......basi kazi ninayo,huo mlolongo....
Nashukuru kunijulisha wapendwa.

Swali lingine, je kama nikitumia njia ya kureseat mtihani wa form four sitawezapata cheti kingine?
Maana hata procedure za kureseat sizijui coz sijawahi......

Nawasilisha

Kila mtihani una cheti chake, ukireseat utapata cheti cha mitihani utakayoifanya.
 
Nawashukuru kwa ufafanuzi na ushirikiano wenu.....mimi niko mtwara mjini sasa naomba msaada kama kunamtu anacontact za mtu wa necta anipe ili nichekianenae anisaidie kufanikisha wepesi kidogo coz saizi nimebanwa na masomo....
Tafadhali wapendwa mnisaidie hilo
 
Sisera imagine kama unataka utumie statement of results katika sehemu mbili kwa muda huohuo Necta watatuma kote? Mfano; unaply TCU pia unaomba mkopo Loan board, hapo inakuaje?

Wanatuma bila shaka. Mimi ni muhanga kama wewe na mkopo nilipata na ajira nilipata hivo hivo
 
Back
Top Bottom