moto ya mbongo
JF-Expert Member
- Sep 9, 2009
- 484
- 337
Naomba kuomba msaada wenu wanajamvi wa JF kuna kijana ametoweka wiki 2 sasa anaitwa JABIRI TIMBULA. Alikuwa ameajiriwa kama VEO kijiji cha Mwongozo Tarafa ya Ulyankulu Wilaya ya Kaliua mkoa wa Tabora. Pamoja na kuajiriwa alikuwa mwanafunzi wa shahada ya kwanza wa chuo kikuu huria (OUT) tawi la Tabora akisoma Bachelor of Arts in Sociology, kabla ya hapo alimaliza kidato cha IV shule ya sekondari Sikonge mwaka 2015 kisha akasomea cheti na astashahada ya Sociology ya chuo cha TEKU cha Tabora. Baada ya kuwa hapatikani katika simu zake hizi 0786 445757, 0767 445757 na 0626 055099 nduguze waliamua kwenda kijiji cha mwongozo kuulizia. Huko waliambiwa kuwa alikuwa ameaga kuwa anaenda Tabora mjini kuendelea na masomo yake hivyo aliondoka kijijini. Wadau tunaomba mtusaidie angalau tujue yupo wapi.