jerryperry2020
Member
- Jul 28, 2020
- 41
- 51
Nawasalimu nyote pamoja na kuwa bize kwa habari za soka la watani wa jadi nisiwachoshe sana.
Jana nikiwa mkoa wa Moro nikipata chakula cha mchana bar moja maarufu karibu na stendi ili niweze kuendelea na safari alikuja mama mmoja mtu mzima akanisalimia kwa bashasha na kueleza kuwa yeye ni muinjilisti wa makanisa ya TAG anakusanya mchango ili akahubiri injili mkoa wa Songea kuhusu Wimbi la mapenzi ya jinsia moja hivyo wanahitaji fedha kufanikisha safari hiyo muhimu.
Kutokana na umri wa mama huyo na hasa hali ya suala hilo lilivyo nchini nikaamua kutoa kidogo nilichonacho na kusaini kwenye fomu hiyo ambayo kulikuwa tayari imesainiwa na watu wengine ila alipoondoka tu yule mama mhudumu akaja akasema yule mama ni kawaida yake kuchangisha watu na hiyo pesa nimepigwa nikajua kweli sasa hali siyo kabisa wasanii ni wengi kuliko wenye mahitaji ya uhakika kuanzia leo sitachangia mdau yoyote atakayekuja kwangu shubamiti.