Kupotea kwa TMK ya Juma Nature na Chege ni Pigo kwa Muziki Industry, walinogesha sana matamasha, waliopo wanajichetua sana

Kupotea kwa TMK ya Juma Nature na Chege ni Pigo kwa Muziki Industry, walinogesha sana matamasha, waliopo wanajichetua sana

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,778
Reaction score
7,145
Wana JF,

Kama ulikuwa hujui, kundi pekee la kibongo lilioanzoshwa chini ya Juma Nature na Chege Chigunda ndilo kundi pekee lililokuwa linashambulia jukwaa, kiasi kwamba kwenye kiti linahakikisha Hawaii mtu.

Hata hivyo nashindwa kuelewa walifeli wapi? Mfano tuliambiwa Juma Nature alipata pesa nyingi kwenye hii industry, pia alikuwa na uwezo wa kutunza mashairi lukuki na zinakubalika. Aliibua vipaji vingi hadi wazee wako.

Kundi hili kilikuwa linajituma sana na halina dharau kwa watanzania kiasi kwamba lilipendwa sana. Ccm kwenye kampuni hasa Mkapa na JK aliwatumia sana. Hivi ni kweli waliishiwa tungo, mbinu za kucheza, au walijaa umimi na kushindwa kuendelea

Makundi yaliyoibuka baada ya wao kufeli, wanaishi kwa kujichetua sana, malinga mengi, majivuno ndio usiseme, kwa sasa wameanza kuwekeza na mwalifu na dhuruma nyingi kisa ukwasi kuwa mkubwa, wanaharibu jamii kwa majimbo yao ya ujenzi ushenzi
 
Hahahaa mkuu hapo mwishoni umemwaga povu la hela yote.

Nature bado yupo ila nadhani muda umemuacha sio kama kipindi kile juma kiroboto sir nature msitu wa vina enzi za mugambo,ugali na msela.
Huyu alikuwa diamond wa kipindi hiko. Fela kawazulumu sana hawa jamaa.
 
Nature mwenyewe kutwa anashinda anakunywa k vant tu.
 
Lile li diwani sijui meneja la diamond ndio liliua na litapeli sana hili limewadhulumu sana.. Wangekuwa matajiri wakubwa
 
Back
Top Bottom