Kupotea sehemu unayoijua inasababishwa na nini?

Kupotea sehemu unayoijua inasababishwa na nini?

man dunga

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2013
Posts
3,358
Reaction score
5,783
Kipindi hicho nakaa Tegeta kwa Ndevu niliwahi kupotea, yaani baada ya kushuka kwenye daladala nikawa siioni njia ya kuelekea nyumbani nilikokuwa nakaa.

Nilizunguka sehemu moja kwa muda mrefu huku nikiona kama baadhi ya watu wananisema. Mpaka leo sielewi kilinipata nini maana hiyo sehemu sikuwa mgeni nilikuwa nimeishi karibu miaka 5.

Baada ufahamu ulivyorudi nilikuwa nazunguka maeneo hayo hayo ya njia ya kuelekea nyumbani.
 
Hali hiyo najua inakupata hasa ukiwa porini,inaitwa kupigwa ndui kwa sisi wanyiramba,nilikuwa nachunga ng’ombe gafla nikawa sijui tena uelekeo wa nyumbani katikati ya pori halafu nipo peke yangu sijui narudi Vipi nyumbani ,mbinu niliyowahi kupewa na babu yangu ni kwamba hali kama hiyo ikikukuta ukiwa unachunga ng’ombe ni kwamba Hakikisha unawachunga vizuri wale washimbe ikifika tu jioni ng’ombe wenye watoto ndio huongoza kwenye nyumbani ili wakanyonyeshe,na kwenye nilifanya hivyo jioni ng’ombe waliniongoza hadi nyumbani,yaani nakuja kustuka ndio naingia home kabisa kama vile nimetoka usingizi kumbe live,nilishangaa sana wakati nilikuwa naenda kuchunga sehemu hizo hizo miaka 3 bila kupotea
 
Kipindi hicho nakaa tegeta Kwa ndevu niliwahi kupotea, yaani baada ya kushuka kwenye daladala nikawa siioni njia ya kuelekea nyumbani nilikokuwa nakaa. Nilizunguka sehemu moja kwa muda mrefu huku nikiona kama baadhi ya watu wananisema. Mpaka leo sielewi kilinipata nini maana hiyo sehemu sikuwa mgeni nilikuwa nimeishi karibu miaka 5.
Baada ufahamu ulivyorudi nilikuwa nazunguka maeneo hayo hayo ya njia ya kuelekea nyumbani.
Umenichekesha sana, siku niko na bro tumetoka party kula mitungi sasa e bana turudi home tuchukue taxi nikazereu taxi hapo dk 5 tumefika huku namponda "tutembee wewe kata mafuta hayo🤣🤣🤣"
Aisee tulizunguruka siku hiyo na lile bwii mpk kunakucha.
Dah akili ikanijia bro turudi tulikotokea.
Hapo shalaumiwa njia nzima😅😅😅.
Tukarudi tunafata alama njia tuliyotokea ka misukule.
Dah tukafika bahati nzuri taxi hii hapa.
Tunamueleza jamaa atufikishe hakuchukua dakika tushafika.
Sasa mpk leo najiuliza si tulienda wapi?
Sipati majibu😁
 
Iliwahi kunitokea ughaibuni!! Nishakaa miezi sana, kituo cha metro hichohicho nashukia kila siku na gate hilo hilo ninalotokea!! Ajabu natoka getini sioni uelekeo na sijui naenda wapi!!

Nilizunguka kuanzia saa mbili usiku mpaka saa nne unusu, wazo la kuuliza liliponijia kuna binti wa Kizungu nikamuuliza kupitia duka la miwani lilikuwa maarufu sana hapo, mimi nilikuwa naishi ghrofani katika jengo hilo hilo!!

Ajabu akanionesha hilo hapo (nilikuwa hapo hapo ila silioni) ikawa ni kama kanifumbua macho, cha kwanza nilikimbilia kulala! Nilichoka kuzurura

Nilijipa moyo labda mawenge ya nchi za wenyewe lakini bado! Nahisi kuna kitu kilinitokea
 
Hatari sana,mi nakumbuka utotoni iliwahi kuntokea hiyo, nilishtukia nimo ndani ya nyumba ya bibi flani alikua anaishi mtaa wa pili kutoka mtaani kwetu,msaada wa majirani walioniona wakati naingia lasivyo ....... ,
 
Kipindi hicho nakaa tegeta Kwa ndevu niliwahi kupotea, yaani baada ya kushuka kwenye daladala nikawa siioni njia ya kuelekea nyumbani nilikokuwa nakaa. Nilizunguka sehemu moja kwa muda mrefu huku nikiona kama baadhi ya watu wananisema. Mpaka leo sielewi kilinipata nini maana hiyo sehemu sikuwa mgeni nilikuwa nimeishi karibu miaka 5.
Baada ufahamu ulivyorudi nilikuwa nazunguka maeneo hayo hayo ya njia ya kuelekea nyumbani.
Hutokea sana kwa wengi hasa ukiwa eneo geni kidogo kwasababu ya kupoteza ramani ya mahali na kushindwa kuwauliza wenyeji kutokana na hofu au kiburi pia. Lakini yaweza kuletwa na michezo ya wachawi kutaka kukupima upoje kimazingara au hata kujifurahisha tu. Mara nyingi mtu hakumbuki cha kufanya wakati amepotea ila atakuja shtuka baadaye wakati ameshafika eneo husika.
 
Hapo mwishoni huko sahihi, ni kweli hukumbuki cha kufanya ndio maana utazunguka sehemu moja kwa muda mrefu mpaka ufahamu urudi. Kiukweli sio usahaulifu ndio maana ufahamu ukirudi utashangaa Sana kuwa pale Kwa muda mrefu bila kufika sehemu uliyokuwa unaenda na unaijua Kwa 100%
 
Back
Top Bottom