Kupotezwa nyeti(wanaume) ni drama ya kuwapotezea watu kifikra!

Kupotezwa nyeti(wanaume) ni drama ya kuwapotezea watu kifikra!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
18,653
Reaction score
31,010

Mchezo huu wa ati mtu anaguswa began, halafu nyeti zinapotea, ni ujinga uliokithiri.
Ujinga huu umepewa promo ili kuondoa majadiliano Makali yaliyokuwa yakiendelea juu ya kupanda kwa gharama za maisha kutokana na kupanda kwa bei za nishati ya mafuta.

Ilianzia Tunduma Mbeya, mara tukasikia Mwanza na Dar.
It was well orchestrated.

Hatujasikia nyeti za wanawake kupotea wakiguswa bega.

Tuache mjadala wa mafuta uendelee.
 
Vijana tuamke, huu sio muda wa kuamini kwa kila kinachosemekana katika miji hapa nchini ikitokea upo sehemu na kuna kijana analalamika kupoteza nyeti, jambo la kwanza kufanya mpekueni kuangalia kama nyeti zake zipo lakini ikibaikina hakuna ukweli ashushiwe kipondo tu!!! Tumeshachoka kuaminishwa uzushi.
Yaani sahv vijana wana amini sana pini na rubberband kuliko 🙌🏽🙌🏽🙌🏽
 
Idadi kubwa ya Watanzania wamekosa Elimu bora utotoni haya ndio madhara yake huu ujinga hauwezi kuwapelekea Zimbabwe wakakuelewa..
 
Back
Top Bottom