Kupunguza Fraud mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Uhudumie hospitali za umma tu

Kupunguza Fraud mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Uhudumie hospitali za umma tu

Jackbauer

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Posts
6,053
Reaction score
2,207
Ieleweke kuwa kuna mlipuko wa uanzishwaji wa Hospitali binafsi almaarufu Polyclinics na Specislized clinics hapa nchini ambazo kwa maoni yangu nyingi zimejibatiza majina tu.

Nyingi ya clinic hizi zinategemea malipo kutoka mfuko wa bima ya afya (NHIF) na kiukweli bila NHIF nyingi zitakufa.
Clinic hizi ndio vinara wa kuandika vipimo na dawa bila justification.

Kwa muktadha huu ni vyema Sera ya Afya ihuishwe na kuaccomodate maswala ya Bima ya Afya kwa wote,tukijaribu modal ya Kuwa na mifuko miwili yaani NHIF kwa wale watakaotumia huduma za umma na mfuko mwingine (wa kuratibu ) bima za afya za binafsi.

Inasikitisha kuona baadhi ya uncontrolled private sector wakitaka kuufilisi mfuko huu.

Aidha NHIF iache kukurupuka kila mara na kwa kumbukumbu zangu ni kuwa ilipaswa kuratibu mfumo wa / swala la bima ya afya kwa wote japo hadi sasa hakuna kinachoeleweka.
 
Bahati mbaya hospitali nyingi za serikali huduma zao haziridhishi. Foleni kubwa! Utaratibu wa kupata huduma kwenye hospitali nyingi za serikali, ni mbovu!

Ni hospitali chache tu kama Muhimbili, Benjamini Mkapa, nk. Ndiyo zinafanya vizuri. Ukienda hospitali ya Wilaya kama Magunga pale Korogwe, unaweza ukakata tamaa.
 
Wingi wa watu Mkuu. Bima ikiwa serikalini tuu tutajaa na kushindwa kuhudumiwa.

Mfanyakazi atapoteza siku tatu kwenye foleni ya kumuona daktari, siku mbili foleni ya maabara, siku Nne foleni ya majibu n.k

Wacha ziendelee kuwepo na hospital binafsi lakini ziboreshwe.
 
Hata sikumbuki mara ya mwisho kutibiwa Hospitali za Serikali ilikuwa mwaka gani maana huko ni miboreko tupu, huduma mbovu kuanzia foleni ya kumuona Daktari hadi dirisha la dawa ambako dawe zenyewe hakuna.

Kama kuna mapungufu kama hayo ni jukumu la NHIF kujitathimini na kuchukua hatua ya kumaliza tatizo hilo la sivyo na wao NHIF wanashirikiana na hizo Hospitali kanjanja kuihujumu NHIF
 
Ni kwa nini mjadala wa Bima ya afya kupitia NHIF unazungumzia waajiriwa tu. Je wasioajiriwa hauwahusu? NHIF ni shirika la serikali. Kwa nini kuna huu ubaguzi?
 
Ieleweke kuwa kuna mlipuko wa uanzishwaji wa Hospitali binafsi almaarufu Polyclinics na Specislized clinics hapa nchini ambazo kwa maoni yangu nyingi zimejibatiza majina tu...
Kwa nini unichagulie hospitali ya kwenda kutibiwa. Baadhi yetu hatutibiwi hospitali za umma ni mwiko kwa sababu tunataka huxuma bora. Kama NHIF imefilisika serikalii itoe uhuru kila mfu ajiunge na mfuko wa bima anayotaka mwenyewe.

Siku zote wizi ni njama ya pa de mbili hao hospitali binafsi hawawezi kuiba bila kusaidiwa na maafisa wa NHIF .
 
Ieleweke kuwa kuna mlipuko wa uanzishwaji wa Hospitali binafsi almaarufu Polyclinics na Specislized clinics hapa nchini ambazo kwa maoni yangu nyingi zimejibatiza majina tu...
## Mr Jackbauer justification ya mgonjwa aliyeenda kupata huduma ktk hospitali binafsi aidha nzuri au mbaya ikiwemo vipimo + dawa, ni mgonjwa mwenyewe kufa au kupona...

## Huhitaji justification nyingine zaidi ya hii. Hayo mengine ya sijui kufilisika kwa mfuko, basi sababu haiwezi kuwa hii unayosema...

## Sababu za kufilisika kwa mifuko yote ya hifadhi ya jamii ukiwemo huu wa NHIF ni mbili kubwa ambazo ni;

1. Mifuko kuwekeza kwenye miradi isiyo na tija ya ku - generate faida ya haraka na kuwa na manufaa kwa wanachama wote ili kuwapunguzia mzigo wa mchango...

2. Serikali kuchota fedha nyingi toka kwenye mifuko hii na haizirudishi. Matokeo ya kitendo hiki ni ni shida ya mzigo ambao unawarudia wanachama wa mifuko huu. Kama hali itaendelea hivi, tusije kushangaa huku mbeleni kiwango cha % cha kuchangia kwa wanachama kikaongezwa...!

✓ Mfano kwenye mifuko ya PSPF, NSSF, LAPF chini ya mwavuli wa PSSSF wanachama wengi mpaka sasa wanasota kwa muda mrefu kwa kutopata mafao yao ya kustaafu kwa wakati kwa sababu pesa zilichukuliwa na serikali na kupelekwa kusikojulikana ikiwemo kugharamia shughuli za serikali na kampeni za CCM za chaguzi kuanzia 2020 na kurudi nyuma...

✓ Juzi kati ilitolewa ripoti ya serikali kudaiwa na mifuko hii zaidi ya trilioni 3.4 ambazo ni fedha za wanachama wa mifuko hii. Mpaka leo serikali inadaiwa matrilioni kadhaa deni lililotokana na ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma - UDOM..!

## Matokeo ya matendo haya ya serikali ni mzigo na usumbufu mkubwa kwa wanachama wa NHIF...

## Inashangaza sana kuwa, badala ya serikali kutatua matatizo halisi yanayoukabili mfuko huu, wanaanza kusumbua wanachama kwa kuwawekea taratibu za kitumwa za kupata huduma ya matibabu ambayo ni haki halali ya mwanachama...

## Mathalani, mfuko wa NHIF unashindwaje kuja na mbinu salama za kuthibiti forgery toka kwa wanachama wasio waaminifu wanaoshirikiana na baadhi ya hosipitali bila kuathiri kundi kubwa la wanachama wasio na hatia...????

## Hebu, tujaribu kufikiri na hili;

Kwamba, NHIF wanathubutuje kuwapangia watu waende hospitali mara mbili au tatu hospitali?

Kwani magonjwa yanapangiwa kuja kwa mtu..?

Na kwanini wapunguze idadi ya wanufaika wa bima kwa mwanachama..??

Hii siyo sawa na haingii akilini.!!
 
Bahati mbaya hospitali nyingi za serikali huduma zao haziridhishi. Foleleni kubwa! Utaratibu wa kupata huduma ni mgumu!

Ni hospitali chache tu kama Muhimbili, Benjamini Mkapa, nk. Ndiyo zinafanya vizuri. Ukienda hispitali ya Wilaya kama Magunga pale Korogwe, unaweza ukakata tamaa.
nadhani bado unaiishi historia na sio uhalisia
 
Ieleweke kuwa kuna mlipuko wa uanzishwaji wa Hospitali binafsi almaarufu Polyclinics na Specislized clinics hapa nchini ambazo kwa maoni yangu nyingi zimejibatiza majina tu.

Nyingi ya clinic hizi zinategemea malipo kutoka mfuko wa bima ya afya (NHIF) na kiukweli bila NHIF nyingi zitakufa.
Clinic hizi ndio vinara wa kuandika vipimo na dawa bila justification.

Kwa muktadha huu ni vyema Sera ya Afya ihuishwe na kuaccomodate maswala ya Bima ya Afya kwa wote,tukijaribu modal ya Kuwa na mifuko miwili yaani NHIF kwa wale watakaotumia huduma za umma na mfuko mwingine (wa kuratibu ) bima za afya za binafsi.

Inasikitisha kuona baadhi ya uncontrolled private sector wakitaka kuufilisi mfuko huu.

Aidha NHIF iache kukurupuka kila mara na kwa kumbukumbu zangu ni kuwa ilipaswa kuratibu mfumo wa / swala la bima ya afya kwa wote japo hadi sasa hakuna kinachoeleweka.
Habari,

Ni vyema kuja na hoja zenye mantiki katika suala hili:

1: Polyclinic/superspecialized clinic husajiliwa na NHIF kutoa huduma kwa mujibu wa vigezo vya wizara ya afya na NHIF wenyewe kujiridhisha.

2: NHIF hufanya malipo baada ya kujiridhisha juu ya huduma zilizotolewa kwa mteja wao pamoja na REJECTION juu yake.

3: NHIF wana anti-fraud na quality officers wao, hili ni jukumu mama lao (kuhakikisha value for money) kwa huduma zinazotolewa. Je wamefeli??

4: Hizi clinics zimelipwa bilions ngapi ndani ya miaka mitano?? Je ndo total loss ya NHIF hela inayotafutwa??

5: NHIF wana kesi ngapi mkononi za fraud dhidi ya /miongoni mwa hizi clinics mpaka ziwe generalized kwa wizi??

6: Kama mgonjwa anatoka at National/Regional/district hospital level kwenda kufanya kipimo au kupata dawa ambavyo amevikosa huko na kurudi kwenye clinics. Tafakari wazo lako. Utakata mti uliokalia labda kama uko nje ya nchi hii au mfumo wa afya.

NB: NHIF waangalie walipojikwaa, na.si walipoangukia ili kutatua tatizo. Nenda upandw wa pili kwa watoa huduma pia wanainyooshea kidole NHIF.
 
Wingi wa watu Mkuu. Bima ikiwa serikalini tuu tutajaa na kushindwa kuhudumiwa.

Mfanyakazi atapoteza siku tatu kwenye foleni ya kumuona daktari, siku mbili foleni ya maabara, siku Nne foleni ya majibu n.k

Wacha ziendelee kuwepo na hospital binafsi lakini ziboreshwe.
Huduma za hospitali za umma zimeongezeka sana ,vituo vya afya vimeboreshwa hospitali za mikoa zinaanza kuwa na CT SCAN .
 
Habari,

Ni vyema kuja na hoja zenye mantiki katika suala hili:

1: Polyclinic/superspecialized clinic husajiliwa na NHIF kutoa husuma kwa mujibu wa vigezo vya wizara ya afya na NHIF wenyewe kujiridhisha.

2: NHIF hufanya malipo baada ya kujiridhisha juu ya hudhuma zilizotolewa kwa mteja wao pamoja na REJECTION juu yake.

3: NHIF wana anti-fraud na quality officers wao, hili ni jukumu mama lao (kuhakikisha value for money) kwa huduma zinazotolewa. Je wamefeli??

4: Hizi clinics zimelipwa bilions ngapi ndani ya miaka mitano?? Je ndo total loss ya NHIF hela inayotafutwa??

5: NHIF wana kesi ngapi mkononi za fraud dhidi ya /miongoni mwa hizi clinics mpaka ziwe generalized kwa wizi??

NB: NHIF waangalie walipojikwaa, na.si walipoangukia ili kutatua tatizo. Nenda upandw wa pili kwa watoa huduma pia wanainyooshea kidole NHIF.
Kuna kipindi niliwahi kuwaza kuwa NHIF awe na hospitali zake kabisa kuondokana na hii kadhia lakini kwa sasa hospitali za umma ni nyingi na zinaendelea kuboreka,
walipokosea ni pale walipoanza kiherehere cha kupeleka huduma hii huko private leo ndio matokeo yake tunayashuhidua...utatuzi...wajikite na public sector,waziwezeshe public hospitals mfuko ubaki salama....

Private sector ipewe mratibu wake ambaye atacoordinates bima shindanishi za private.

Kama kweli unakiri kuwa private specialized clinics na poly clinics hazichangii kuua mfuko kwa nini ziogope kuondokewa na huu mfuko?

Hizi clinics ndio zinamvuta NhiF aondoke katika kufinance afya msingi na kuanza kujiumiza na complicated health care services.
 
Ni kipi kwa data kinakupa ufahamu kuwa hizi clinics ndio tatizo la msingi au private health sector??

Mwanzoni mlidhani kuna ghost clients, mmeanzisha online registration and authorization then claiming. Sasa inadaiwa ni hujuma na wizi. Je ni ghost patients au wizi?

Kwani hakuna sekta nyingine za serikali zinafanya kazi na private sectors??

NHIF ijisimamie vyema, walete hesabu ya clinics/private health facilities dhidi ya hela iliyopotea tuone madai yao na uhalisia.

Kama NHIF ikiweza kuonyesha value for money. Waangalie kwa pamoja na serikali ambayo ina sera ya husuma ya afya nafuu kwa makundi haya:
1: Watoto
2: Wajawazito
3: Wastaafu/wazee zaidi ya 65 years.
4: Walemavu

Serikali ipitie NHIF kuongeza nguvu kwa idadi ya wahusika waliosajiliwa huko. Badala ya ku-stress zaidi haya makundi, na wakati huo NHIF itakuwa inaimarishwa kifedha na yenyewe ikihakiki matumizi sahihi kupitia vyombo vyake.

Ni kweli kuna hatua imepigwa kwenye hospitali za serikali, lakini si kiasi hicho.

Bado tunawapokea watu hawajameza dawa zao wiki mbili na zaidi wakiwa wanafukuzia dawa huko juu. Ikishindikana wanarudi chini, ukiuliza kwa nini BP iko hivi, jibu niliambiwa kurudi baada ya wiki nipate dawa na bado sijapata. Na hapo ni DSM, a very big hispital. Je huko mkoani? Tusiwe na maamuzi ya haraka, tutibu mambo ya msingi kwa busara na hekima. Si kutibu tunachofikiria tu.

Tuna majengo mazuri, lakini bado watu wanayakimbia kwa kukosa watendaji na vitendea kazi kutoka huko. Nadhani suala la ajira ulilisikia lilivyokua kama hukuona.Tunaleta au hitaji ni 10, lakini kata hao 6, utapata 4.

Sera ni de-centralize services na si re-centralization.

Hivi, kati ya NHIF Vs Strategies ukilinganisha na ugumu wa kupata wachangiaji na masharti kwenye matumizi, ni nani angekuwa wa kwanza kufirisika??
 
Una point kwakweli ila tukirudi ktk uhalisia hilo jambo linakuwa gumu,kutokana na hali ilivyo nchini.....huduma zitolewazo na hispitali za serikali haziridhishi kwa asilimia kubwa....

TUENDELEE TU HIVIHIVI.

Sent from my PBBM00 using JamiiForums mobile app
 
Kuna kipindi niliwahi kuwaza kuwa NHIF awe na hospitali zake kabisa kuondokana na hii kadhia lakini kwa sasa hospitali za umma ni nyingi na zinaendelea kuboreka,
walipokosea ni pale walipoanza kiherehere cha kupeleka huduma hii huko private leo ndio matokeo yake tunayashuhidua...utatuzi...wajikite na public sector,waziwezeshe public hospitals mfuko ubaki salama....

Private sector ipewe mratibu wake ambaye atacoordinates bima shindanishi za private.

Kama kweli unakiri kuwa private specialized clinics na poly clinics hazichangii kuua mfuko kwa nini ziogope kuondokewa na huu mfuko?

Hizi clinics ndio zinamvuta NhiF aondoke katika kufinance afya msingi na kuanza kujiumiza na complicated health care services.
Hivi tafsiri sahihi ya "huduma kuboreka kwenye hospitali za umma" ni ipi hasa...?

Ndugu Jackbauer kama ubora wa huduma kwenye hospitali za umma ni kuongezeka kwa majengo, basi utakuwa uko sahihi kwani serikali imejitahidi kiasi chake kwenye eneo hili...

Lakini kama kuboreka kwa huduma ktk hospitali zetu za umma (serikali) ni upatikanaji wa huduma bora za dawa, vipimo + customer care, nakuhakikishia kwenye eneo hili kwa hospitali za serikali ni hovyo sana at the rate that ranges below 50%...!!

Hakuna dawa. Hakuna madaktari na kama wapo, hawatoshi kuhudumia maelfu ya wagonjwa wanaofurika kila siku huko. Wachache waliopo hawako motivated wala committed na kazi yao...

Nilienda kituo cha afya kimoja kijiji fulani huko Simiyu nikiwa na mgonjwa wangu alipata ajali... Ilinishangaza sana mganga aliyepokea kila hatua ya check up hadi ku - prescribe dawa ilikuwa lazima a - google kwenye simu yake...!!!!

Huku vijijini usiseme kabisa maana hali ya huduma za afya ni mbaya sana..

Ni kweli majengo mengi yamejengwa na kuitwa zahanati za vijiji lakini ni ukweli pia kuwa, hayo ni majengo tu yasiyokuwa na chochote cha maana...

I can confidently say, hayo ni machinjio ya watu kwa sababu utaitaje jengo fulani ni hospitali wakati huduma na facilities za ki - hospitali hazipo...???

Sekta ya afya bado sana Tanzania. Inahitajika kuboreshwa sana...
 
Kwani huko NHIF hakuna kitengo Cha utafiti na uthibiti ubora? Kama kipo ndo majibu ya tafiti zao ya namna ya kuthibiti hayo matatizo?
Kwanini kila Mara NHIF inakuja na ujinga ujinga mwingi? Inashangaza sana.
 
Hata sikumbuki mara ya mwisho kutibiwa Hospitali za Serikali ilikuwa mwaka gani maana huko ni miboreko tupu, huduma mbovu kuanzia foleni ya kumuona Daktari hadi dirisha la dawa ambako dawe zenyewe hakuna.

Kama kuna mapungufu kama hayo ni jukumu la NHIF kujitathimini na kuchukua hatua ya kumaliza tatizo hilo la sivyo na wao NHIF wanashirikiana na hizo Hospitali kanjanja kuihujumu NHIF
Hospital ya rufaa Mbeya si miongoni mwa hizo. Tena wanufaika wa bima ya afya, wanapewa kipaumbele.
 
Ni kwa nini mjadala wa Bima ya afya kupitia NHIF unazungumzia waajiriwa tu. Je wasioajiriwa hauwahusu? NHIF ni shirika la serikali. Kwa nini kuna huu ubaguzi?
Kwa mtu ambae sio muajiriwa wanamashariti magumu sana.
 
Sasahivi tuna NIDA,simu,Mpiga kura nk
Waboreshe mbinu za kuhakiki na wagonjwa kama kweli wametibiwa
Na wametibiwa vitu hivyo vinavyodaiwa
Hasa kwa claims za service providers binafsi hao ndio wana risk kubwa ya kufake kuliko Taasisi zinazopata ruzuku ya Serikali

Na data analytics ukiwa na defined objectives zako zitaonyesha trend flani,look for exceptions,normals, nk

Pigia simu wagonjwa to confirm
 
Back
Top Bottom