Kupunguza Fraud mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Uhudumie hospitali za umma tu

Kuna baadhi ya maeneo hospitali za umma hazipo na kama zipo zinatoa huduma za ngazi ya chini ( Mfano: Litembo(Mbinga), Peramiho( Songea vijijini).
Pia Kuna suala la kupunguza mlundikano wa wagonjwa( Mfano: Bugando(Mwanza))
Pia suala la utendaji mzuri na wa haraka katika kuhudumia wagonjwa( hospitali za serikali baadhi ya wafanyakazi wanafanya kazi wanavyojisikia(hasa baada ya kuondoka Magufuli). Kwahiyo, hospitali za private ni muhimu Sana hasa katika kutoa huduma bora na za haraka(Hatahivyo, kuwepo na follow up na monitoring ya kile kinachofanyika).
 
Kwani huko NHIF hakuna kitengo Cha utafiti na uthibiti ubora? Kama kipo ndo majibu ya tafiti zao ya namna ya kuthibiti hayo matatizo?
Kwanini kila Mara NHIF inakuja na ujinga ujinga mwingi? Inashangaza sana.
Tatizo ni huyo waziri kilaza ,kila siku kutoa matamko kama chiriku
 
Hoja yako yaweza kuwa relevant kama utakumbuka masuala mawili au matatu ambayo ntakukumbusha hapa.

Kuna wakati hela ya EPA ilichotwa BOT na aliekuwa waziri wa fedha Zakia Megji akakanusha kuwa hamna fedha "imepigwa". Uchunguzi wa Ernest & Young ulipofanyika ikathibitika 133bil zimelambwa. BOT ni taasisi ya umma au binafsi, kuna controls au hazipo, fikiria, jikumbushe then tuendelee.

Kuna wakati wa Mei Mosi ya 2021 jamaa wa hazina walijiandikia vocha na kuvuta hela siku hiyohiyo, PM aliwabana na kuhoji inakuwaje within a day, voucher za malipo zimeandikwa na watu wakajilipa siku hiyohiyo tena ikiwa public holiday. Huko hazina ni public office na wala hakuna private sector ndani ya hazina. Huo upigaji ulikuwa na controls au hazikuwepo.

Huduma za afya kama zingekuwa zinatolewa kwa ubora public hosptals, hakuna mgonjwa angepoteza muda kwenda private hospitals.

By the way, kwa sasa NHIF wameboresha sana mifumo na sio manual paper filing kama zamani, vitu vingi vinafanyika kwenye mifumo na mgonjwa baada ya huduma anasaini na huwa wanapokea sms kuthibitisha kama kweli wametibiwa na kituo x ndani ya siku hiyo.

Utaratibu ambao NHIF walitaka kuuweka na Mhe. Waziri kaufuta umekaa kizamani na haukuwa na malengo ya maana kwa mpokea huduma.
Bima ni hela iliyoko kwenye mfumo kumhudumia mgonjwa akiugua kama ambavyo ukiwa na card ya bank unaweza ku-access fedha bank yako popote maadam fedha ipo kwenye mfumo na ATM au teller anaiona una akiba unapata fedha.

Say leo uko Mtwara na ulitibiwa ndani ya mwezi huu, ikatokea umesafiri mpaka serengeti na kuugua ghafla, ilitakiwa kurejea Mtwara ulikotibiwa ndani ya huo mwezi na usingetakiwa kupata huduma nje ya kituo ulichotibiwa ndani ya muda huo.
Watoa utaratibu toka NHIF hawakuona namna ya ku-improve service delivery kwenye picha kubwa. Aidha huenda mfuko una matundu mengi na wanajaribu kuziba kwa njia ambayo inaweza kuathiri maisha ya insured.

Asante mhe. Waziri Ummy kwa intervention
 
Bahati mbaya hospitali nyingi za serikali huduma zao haziridhishi. Foleleni kubwa! Utaratibu wa kupata huduma ni mgumu!
Nina kusikitikia wewe nadhani kwasasa hospitali za umma wana huduma nzuri kuliko private.

Huko private ukichunguza vizuri janjajanja nyingi fikiria ni kwann kila mgonjwa anayeshindikana private anapelekwa serikalini.

Ndugu utakuja niambie huko private tunapigwa sana
Hapa ni NHIF waache ubabaishaji
 
sidhani kama unaelewa unachokiongea
 
Tatizo maamuzi mengi yanakuwa ya kisiasa zaidi kuliko kitaalamu, hata kwenye teuzi za management, bodi , na kadhalika
 
 
Huenda na wanufaika wengine wamo humo humo !!
 
If you want extra go to private
 
Acha kusaga kunguni, hospitali binafsi ndo zinazotoa huduma zinazoridhisha........kwa hiyo lengo lako unataka kudumaza huduma binafsi za kiafya ili turudi kulekule kwenye huduma duni, urasimu, kujuana, foleni na wagonjwa kulazwa sakafuni. Polyclinic kuwa nyingi kuna tatizo gani? acha huduma za kiafya zipanuke wananchi waweze kupata huduma bora kwa uharaka zaidi bila stress.
 
Ndugu wadau, niseme kwa ufupi tu kulingana na uzoefu wa mwaka 2011 hadi 2012, NHIF inaweza kuwa imepata changamoto za kiuendeshaji kutokana na baadhi ya watumishi wake kutokuwa waadilifu mathalani baadhi yao kutaka,kuomba na kupewa % kadhaa inayotokana na malipo ya matibabu kwenye nyaraka za matibabu kwa namna wanavyojua wao.hii iliwahi kutokea kwa Taasisi ya magonjwa ya moyo (THI), kwa bahati nzuri, mkurugenzi mtendaji mkuu Dr.Masau aliwagomea katakata,kilichofuata ni kuanza mizengwe ya kupunja malipo yake kwa visingizio kadhaa wakati si kweli. Hadi THI inafungwa 200M haikulipwa kwa makusudi huku zikionyeshwa taasisi imelipwa,na kupelekea kuwa Sekeseke na mkurugenzi wa kanda ya DSM wakati akahamishiwa. Hakika kulikuwa na Madudu sana kwenye mfuko sijui kwa sasa kiukweli.
Mfuko unapaswa kujitafakari pia kwani kwa kipindi hicho,naamini baadhi ya hospital au vituo vya afya au mahali NHIF ilitoa huduma kulikuwa na baadhi malipo hayakuwa halali.
Narudi,najua vema mchezo ulivyokuwa unachezwa na Dr.Masau akikataa kuwaibia Watanzania kwa stahili hiyo.nchi iliyojaa wabinafsi sana daima maendeleo yake ni mwendo wa kinyonga tu.
 
Huduma za hospitali za umma zimeongezeka sana ,vituo vya afya vimeboreshwa hospitali za mikoa zinaanza kuwa na CT SCAN .
sikubaliani na wewe hata kidogo, kwa hiyo mkoa mzima tutegemee ct scan moja ya hosptial ya mkoa kutibu mkoa wote? bado vipimo vingi sana hospital za mkoa hazina mfano MRI, ushauri wako ni mateso kwa wagonjwa, bado sana hospital za umma kuachwa pekee kutibu wagonjwa wa nhif, waache wateja waamue wapi watibiwe, serikali ina uwezo mkubwa wa kudhibiti uwizi wowote dhidi ya nhif.
 
Mkuu umeongea jambo la maana sana. Mimi hospital za binafsi nilishapunguza sana imani. Nyingi hizi ndizo zimeufilisi mfuko. Waziri Ummy alipaswa kufanya uchunguzi wa kina (informal). Hizi hospital binafsi ndizi zinaongoza kwa forgeries za huduma. Mfano unakuta kila mgonjwa anafanyiwa operation kisa tu Dr mhusika ana commission yake, unakuta kila mgonjwa ana typhoid etc, na kibaya kabisa inawezekana uanzishwaji wa hizi hospital zinashikwa mkono na watu wasiowaaminifu NHIF. Hakika Tz tuna tatizo kubwa sana juu ya uaminifu. Cha kwanza ni kuzitoa hospital zote za private kwenye mfuko hiyo ingesaidia na kiboresha hospital za umma.
 
Hiyo ni remedial action, but lazima kuwe na scientific approach ya kusuluhisha matatizo yaliyopo ili NHIF iwe stable and sustainable.

Kwanza, wajue mataatizo yanazalishwa na kitu gani, gap kwenye sheria au uongozi mbaya;

Pili, wajitathmini kama wanahitaji kuhodhi soko lote, yaaani watumishi wa umma na raia wa kawaida;

Tatu, watengeneze catalogues of medicines and services ikiwa na indicative prices ili kupunguza ubabaishaji na ku-predict their financial liability ambayo ita determine realistic premium ambayo wanachama wanapaswa kuchangia; na

Mwisho, wa automate process zote
 
Kusema NHIF ijitoe kwenye hospitali binafsi niwazo la kijinga mmno, chamuhimu mifumo iboreshwe ili kuondoa ubambikizwaji gharama za matibabu.
Sekta binafsi inasaidia sana serikali ktk kupanua upatikanaji sa huduma na ubora wa huduma za afya. Wanaotibiwa huko na wanaotibu bado nisisi watz haspitali za serikali hazimudu kutibu wanabima wooote tuelewe
 
Watumishi wa NHIF wanalipa matibabu hewa kwa kutengeneza madai hewa pia wanajikopesha pesa ya mfuko bila riba kwa muda mrefu.

Pia magufuri alichota 56b kufadhili kundi la wasiojulikana
 
Umenena kweli mdau, baadhi ya watumishi NHIF ni na majanga sana na wamekaa kirushwa rushwa tu, hospitali binafsi zimeneemeka kutokana na malipo mengine yasiyo na ukweli wala uhalisia wowote, ninajua kile Taasisi ya magonjwa ya moyo-THI ilivyorubuniwa kuingia mjenge huo,bahati nzuri mtendaji wake mkuu akagoma kuwaibia watanzania kodi zao kwa kigezo cha matibabu na malipo hewa. Mungu anawaona NHIF baadhi hasa wasio wazalendo kwa Taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…