Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,925
Couple walipoona hali ngumu ya maisha na kile wanchochuma huishia kwenye makato na rent wakaamua kufanya kitu chao wenyewe kwa mikono yao, hiyo ni nchini Marekani. Hali ya uchumi inazidi kuwa ngumu maisha yanazidi kuwa magumu kila kukicha, bora kuwa na sehemu yako ya kujihifadhi ambayo hubughudhiwi na mwingine na unachochuma ni gharama ndogongogo za kuishia maisha yanatulia.
Ujasiri kama huo ni kitu pekee nchini Marekani kwa mazingira yao, je kwa sisi Watanzania kama mtu unaweza kufanikisha kupata kiwanja itakushinda nini kuanza na banda la aina hiyo kisha unachochuma ndipo ujenge sehemu uliyoitengwa kwa dream house yako taratibu?
Vijana hawa walifanya wenyewe kwa mikono yao, ghrama ya $10,000 ni vifaa tu. Kupata habari kamili tembelea link hii ifuatayo: Living In A Tiny House.
