Kupunguza ughali wa maisha kwa kuanza kuishi bandani mwako soma habari hii

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,925
millertinyhouse-048-edit.jpg

Couple walipoona hali ngumu ya maisha na kile wanchochuma huishia kwenye makato na rent wakaamua kufanya kitu chao wenyewe kwa mikono yao, hiyo ni nchini Marekani. Hali ya uchumi inazidi kuwa ngumu maisha yanazidi kuwa magumu kila kukicha, bora kuwa na sehemu yako ya kujihifadhi ambayo hubughudhiwi na mwingine na unachochuma ni gharama ndogongogo za kuishia maisha yanatulia.

Ujasiri kama huo ni kitu pekee nchini Marekani kwa mazingira yao, je kwa sisi Watanzania kama mtu unaweza kufanikisha kupata kiwanja itakushinda nini kuanza na banda la aina hiyo kisha unachochuma ndipo ujenge sehemu uliyoitengwa kwa dream house yako taratibu?

Vijana hawa walifanya wenyewe kwa mikono yao, ghrama ya $10,000 ni vifaa tu. Kupata habari kamili tembelea link hii ifuatayo:
Living In A Tiny House.
 
Tatizo vijana wengi hutuko na msukumo wa kujituma kufanya kitu wenyewe ila tunapenda kuhangaika kutafuta pesa ndizo zifanye kazi. Gharama kubwa za ujenzi wa nyumba hupungua kama usimamizi na baadhi ya jazi zikifanywa na mmiliki. Hili la kuwa na fundi wako mnaenda naye kwa hatua kadiri ya nafasi inavyokurusuhu huku ukisimamia na baadhi ya shughuli kuzifanya mwenyewe utashangaa gharama za utendaji zinavyopungua ukilinganisha na kukodi kampuni ikujengee.
 
10K kwa kibongo bongo unadhani ni kiasi gani mkuu ?, hii bado ipo on a high end wapo waliojenga even chini ya hapo na nyumba ikapendeza; refer straw bale houses
 
Gharama hizo za $10,000 Kwa marekani ni jambao ambalo anaweza kulimudu mfanyakazi wa kiwango cha kawaida.

Kwa Tanzania linawezekana kabisa, nimeshuhudia mtu amestaafu aliwekeza viwanja vya viwili, akauza kimoja na pesa alizopata akaamua kujenga nyumba kuanzia msingi hadi usawa wa madirisha kwa baadhi ya shughuli kuzifanya mwenyewe. Alichohitaji akiba yake nyingine kumalizia mistari iliyobaki na kupaua. Hilo lawezekana ndugu.
 
Hujapata point yangu kabisa..., ninachosema kwenye cheapest you can get cheaper than that and looking good as well; tena kwa hapa bongo kama issue ni kuanza polepole na kuondokana na adha za kupangisha kwa hio 10k mtu anajenga hata tuwili twa hivyo tena wood might be expensive kuliko matofali ya kuchoma au hizo straw bale ninazokwambia (ambazo huko nje watu wemejengea sana and they are comfortable and environmental friendly); cheaper as well
 
Vijijini huku Tanzania wanajituma na kufanya amayo yanawezekana kwa uwezo wao kuliko tunaojiona wasomi kutegemea kila kinachowezekana kufanyika lazima kufikiria pesa kwanza mijini. Nimesema hapo juu kwa vijana hao walivyofanya marekani ni ushujaa wa juu kuliko inavyowezekana Tanzania kwa vile Marekani kila kitu kinahitaji pesa, ingekuwa Tanzania baadhi ya miti wangechukua maporini bila kununua. Nilikuelewa ila basi pengine hatujakutana kwenye point.
 
Alafu kwa marekani huenda kujenga hivyo ikawa gharama.., hivi kwa pesa hiyo kweli huwezi kuchukua mortgage na kwenye mshahara wa mtu akawa analipa benki ili kumaliza mortgage.., sababu sometimes huko kwa wenzake even owning a house inakuwa liability, kuna mambo ya property tax, na makodi mengi mengi ambayo unaweza kujikuta nyumba inakufilisi badala ya kukuhifadhi..

Sadly na huku ndio tunapoelekea you can't believe kodi ya viwanja imepanda mwaka huu mara tatu hata bila ya kuwataarifu watu.. alafu wabunge wetu kimyaaa sijui wanamtetea nani, pale pale ongeza na kodi ya umeme kupanda simultaneously.., sasa mzee alichichangisha maisha yake yote hata kipato kwa sasa si mwisho wa siku na nyumba watachukua ? Tunapoenda panatisha.....
 
Walizokwepa hao vijana ndi hizo gharama za mortgage, zinakufanya muda wa maisha yako pato lako liende huku bank. Hapo wanachotakiwa kulipa ni propert tax na gharama za utility. Huko siku hizi wengi wanaanza kutumia umeme kwa shughuliu maalum tu maana wengi wanaelekea kuchupukia mchepuko wa umeme wa jua. Maisha ghali ndugu yangu.

Property tax Tanzania ni chini mno, mtu unalipa tax TS 5,000 -10,000 kutogemea na ukubwa wa kiwanja, hiyo ni gharama ya miaka miwili. Jamano bongo tambalare. Nilipowaambia rafiki zangu wa mataifa ya nje walibaki midomo wazi kuona hilo mbona haliwezekani ila Africa tu.
 
Mkuu nchi za wenzetu kuna services, kuna homes kwa wazee, kuna hifadhi za homeless as well as council houses au flats kwa wale wasio na kazi au kipato kidogo, hivyo viwanja/nyumba wengi walizonazo wanao uwezo na wakizeeka wengine wanaziuza pesa inalipia old peoples home huko wanapata na service nyingine..

Sasa wewe tukiiga hao kuhusu malipo ya majengo na nyumba, kwa mzee ambae hata pesa ya kula ni shida kunakuwa na tatizo kubwa sana (alafu mimi siongelei wingi au udogo) naongelea kupanda mara tatu kwa wakati mmoja, kama wewe ulikuwa unalipa elfu kumi sasa hivi ni elfu 30; Ila point kubwa unapopanga kuweka kodi za hivi hakikisha kuna service za kutosha.., hivi babu yako sasa hivi ameshastaafu, pensheni yake yenyewe anazungushwa alafu umwambie kwamba kiwanja chako mwaka huu kodi imepanda mara tatu bila taarifa ?

Bongo tambalare kwa anayejiweza sio vinginevyo.., wakitaka kuiga kuwa na na property tax kama ulaya pia wasisahau kuweka service kama ulaya
 
Trust me kwa bongo hyo kitu haifanyi kazi, utakula wamekuvunjia na kukomba hadi mbao ulizojengea.

Wenzetu mbele nyumba inajengwa karibu kabisa na main road na ipo clean and safe lakini kwetu utakuta nyumba ina kuta 2 za nguvu na kuingia ndani nyumba imeshindiliwa magrili had dirishani kuogopa wezi na majambazi.

Hayo ni mambo ya mbele.
 
Serikali inapopungukiwa na pesa maana yake haikusanyi kodi kutosha, na pale inapoelekea makusanyo ya kodi yanajaribu kufikiwa kiwango dalili wazo za ongezeko la kodi itatokea kwa ajili ya kuweza kuendesha shughuli zake kifanisi. Hilo ni po pote.

Hizo nchi zilizoendelea huduma hizo wanazopewa angalia kodi inavyowabamiza, hiyo ingetozwa bongo watu wangerorokea misituni.
 
Umenivunja mbavu! Nadhani kwa jijini labda, lakini ninachofikiria mie kwa bongo si ya mbao ila matofali ay kuchoma au blocks za sement vyumba viwili vinatosha kwa akuanzia maisha ndugu yangu mambo poa.
 
Mkuu kodi inaendana na kipato cha watu.., hata ngombe anakamuliwa maziwa na kulishwa chakula ama sivyo angetoa damu.., ndio maana nikasema kuna service wanatoa kwa watu wasio na kazi, kuna service kwa wazee, kuna implementation ya kuwasaidia watu kupata kazi ambao hawana, huku misaada ya kodi wanapewa so called wawekezaji na makampuni makubwa alafu unaongeza kodi three times kwa wakati mmoja bila hata taarifa.., ukiangalia watu wengi hivyo viwanja ni vya urithi na hawana hata kipato (matokeo yake watu hawalipi kodi na wanajificha) kwahio mkuu huwezi kulinganisha like for like huku na kule, huko mbele kodi inatozwa kubwa na matokeo yake / service zinaonekana sio huku service hakuna / ajira hakuna unategemea kwahio people have no means of paying
 
Maeneo mengi Tanzania kod imekuwa chini ya kiwango vinginevyo huduma zisingekwua duni hivyo. Kodi inavyotesa nchi kama Marekani kama huduma ingekuwa kwa ajili ya taifa pekee wangekuwa peponi zaidi, lakini kinachowatesa na kulisha jeshi lake lilivyojitanua duniani.
 
Mkuu hatuelewani kwenye point moja tu.., kipato vs kodimfano England ni kati ya baadhi ya nchi zenye kodi kubwa sana kuna watu wanapigwa kodi hadi 50% (Top Premiership Footballers ambao wanaingiza malaki ya pesa kwa wiki) ila kuna watu ambao hawana kazi hawa hawatozwi kodi na wengine wanapewa mpaka job seekers allowance na wazee wanapewa some services..

Sikatai watu kukatwa kodi.., ila kipato chao kipo vipi ?, Je tuwatoze wakulima vijijini na wauza karanga mitaani wakati makampuni makubwa yanatozwa yanapewa Tax Heaven na misamaa ya kodi ? Ndio maana nikasema mambo mengine kabla hayajaja huku kwanza tuweke mazingira.., kabla ya kuanza kuwafyeka kila mtu kodi za viwanja na nyumba pesa nyingi tuhakikishe kuna cheap flats, au nyumba za kuweza kuwahifadhi watu watakaoshindwa kulipa hizo gharama ili wasimiliki hivyo vitu.. Kwa ulaya its people who are well off ambao wanao uwezo wa kumiliki nyumba ila hata wale wasio na uwezo wanaweza wakaa kwenye nyumba za bei nafuu ambazo zipo kwa watu kwa ajili hio. Au mortgage is affordable kwa mtu kutumia theluthi ya mshahara wake kuweza kuishi kwenye nyumba
 
Good idea.! Unajua wabongo bado hatujawa na uthubutu wa maamuzi magumu.,pia kuonekana na mtazamo tofauti katika jamii huenda ikawaogofya wabongo ktk maamuzi ya namna hii. Maisha inapanda siku hadi siku,kuanzia kodi,bills na gharama za maisha cha msingi ni kutafuta eneo thabiti na kuhamia kwko unaanza na banda mengine huja maana ile pesa ambayo ungelipia rents, na bills..ndo itaendeleza ujenzi mwingine wa kudumu. Alutã continúá
 
Last edited by a moderator:
Umenivunja mbavu! Nadhani kwa jijini labda, lakini ninachofikiria mie kwa bongo si ya mbao ila matofali ay kuchoma au blocks za sement vyumba viwili vinatosha kwa akuanzia maisha ndugu yangu mambo poa.

Kama hyo nyumba ipo imara sana sawa ila kama ya kujishikiza basi usiweke cha thamani au usiwe umemuuzi mtu lasivyoa kija atakipiga teke kianguke.

Kuna design flani ya nyumba niliionaga mbele nikaipenda, imejengwa kwa mbao tupu ila ni imara sana.

Nikataka kuijaribu hapa bongo nikaogopa sana hii kitu inayoitwa majambazi.
 
Yes! Kuna mitindo mingi, lakini kwa huu inaonekana property si yao wameikodi tu na hivyo hiyo ni mobile home. Wanaweza kuihamisha muda wo wote watakapoona inafaa au kupata property yao kabisa.

Bongo ukiwa na kitu kama hicho kwa na wajulikana mfukoni kumejaajaa hutakosa wageni wa kukushtukiza, lakini kama ni mwenzangu mimi mwenye hali isiyoonyesha kujaza vya dhamani inawezekana, mbona kuna nyuma za makuti na mbao nyingi tu lakini haziingiliwi ila wanafuta zile zenye nondo wanajua ndani kuna vya thamani.

Ukiwa na kaji-lanch kako naona aina hii inafaa maana ni mapumziko ya muda na unapoondoka kurudi mjini vya thamani wavibabe na hata kama una solar yako ndogo utaibeba na kuirudisha unapohitaji.
 
Good idea.! Unajua wabongo bado hatujawa na uthubutu wa maamuzi magumu.,pia kuonekana na mtazamo tofauti katika jamii huenda ikawaogofya wabongo ktk maamuzi ya namna hii. Maisha inapanda siku hadi siku,kuanzia kodi,bills na gharama za maisha cha msingi ni kutafuta eneo thabiti na kuhamia kwko unaanza na banda mengine huja maana ile pesa ambayo ungelipia rents, na bills..ndo itaendeleza ujenzi mwingine wa kudumu. Alutã continúá

Umenena, maana gharama za rent hizo ukiwa makini kwa bongo kufanyia kazi wewe mwenyewe zinaweza kuibua kijibanda kama hiki, sina shaka gharama za ujenzi wa dream home yako itakuwa ngumu kwa vile ukisha kuwa na sehemu yako ya kulaza kichwa mapigo ya moyo hayapandi sana, unabaki kidogo kidogo unachochuma kuanza msingi na kusimamisha kuta taratibu. Ndivyo wajasirimali wengi walivyofanikiwa kujenga nyuma zao iweje wasomi wengi yatushinde?
 
Umenifungua sana macho kwa wazo lako nadhani badala ya kuingia gharama kubwa mahali tunakowekeza wakati unakaa siku chache ni bora kufanya hivi
View attachment 149621

Back
Top Bottom