SoC04 Kupunguza umri wa kustaafu kwa lazima kuwa miaka 55

Tanzania Tuitakayo competition threads

Mkoba wa Mama

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2021
Posts
208
Reaction score
91
Utangulizi.
Kwa kuzingatia mazingira ya sasa, idadi ya watu inazidi kuongezeka kwa kasi kubwa na pia changamoto za kiafya zinazowakabili watu wengi hasa katika umri wa kuanzia miaka 50, kupunguza umri wa kustaafu kwa lazima kutaweka msingi imara kwa ustawi wa wastaafu, kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na kuongeza nafasi za ajira.

Sababu na faida za kuzingatia mabadiliko haya ni kama ifuatavyo:

Kuongeza nafasi za ajira kwa vijana na kuchochea mzunguko wa ajira:

Kutokana na changamoto iliyopo ya ukosefu wa ajira ambayo inatokana na ongezeko la wasomi nchini, kupunguza umri wa kustaafu kwa lazima kutawapa fursa zaidi vijana ambao wanatafuta ajira katika sekta mbalimbali. Vijana wanahitaji kuingia katika soko la ajira na kuchangia katika ukuaji wa uchumi, mabadiliko ya utendaji kazi kuwa wa kisasa zaidi hasa katika nyanja ya matumizi ya sayansi na teknolojia na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kutokana na kuwa na nguvu na uwezo wa kutosha wa kukamilisha majukumu ya kikazi pasipo kuchoka mapema wala kusumbuliwa na matatizo ya kiafya ya mara kwa mara. Kwa kuongeza nafasi za ajira kupitia kupunguza umri wa kustaafu, tutaziba pengo la ajira na kuwezesha kizazi kipya kuchukua usukani katika kuleta mabadiliko ya kijamii na kiuchumi.

Kuongeza ufanisi wa utendaji kazi:
Ni ukweli usiopingika kuwa ufanisi wa utendaji kazi wa mtu unapungua kadri umri unavyozidi kwenda, mtu mwenye umri zaidi ya miaka 55 utendaji kazi wake hauwezi kulinganisha na kijana. Hivyo, kumuacha kazini mtu mwenye umri zaidi ya miaka 55 ukizingatia pia mazingira ya kazi hasa ya nchi zetu zinazoendelea kuna hatari kubwa; kwanza, ni kuendelea kumchosha na kumchakaza yeye mwenyewe na pengine kuwa katika hatari ya kupata maradhi hasa yasiyo ya kuambukiza (shinikizo la damu, kupooza viungo vya mwili, msongo wa mawazo n.k), lakini pia kusababisha ufanisi wa utendaji kazi kuwa wa chini zaidi ukilinganisha na utendaji kazi wa mtu wa umri wa chini.

Kuwapa wastaafu muda mrefu zaidi wa kupumzika na kufaidi mafao yao:
Kulingana na takwimu za mwaka 2022, wastani wa umri wa kuishi kwa mtanzania ni miaka 65, kwa maana hiyo, kwa kuzingatia utaratibu uliopo sasa mstaafu ana wastani wa kuishi ili kufurahia matunda ya kazi yake na kufaidi mafao yake aliyochangia kwa zaidi ya miaka 30 kwa muda wa miaka mitano tu baada ya kustaafu.
Kwa kupunguza umri wa kustaafu, wastaafu watapata muda mrefu zaidi wa kupumzika na kufurahia matunda ya kazi yao na kufaidi mafao yao. Hii itawawezesha kujijengea maisha mapya baada ya kustaafu na kufurahia maisha ya kustaafu kwa amani na utulivu bila msongo wa mawazo na maradhi mbalimbali tofauti na mtu akistaafu umri ukiwa umeenda zaidi.

Kupunguza msongo wa kazi na mawazo kwa watumishi:
Kwa kustaafu mapema, mtumishi wa umma anaweza kupunguza msongo wa kazi na mawazo ambao mara nyingi huja na majukumu ya kazi. Hii inaweza kusaidia kuboresha afya yao ya akili na kimwili na kuwawezesha kufurahia maisha bila shinikizo la kazi.

Lakini pia kutokana na wasiwasi wa watumishi wengi kuhusu afya zao na ikiwa watastaafu na watapata mafao yao ya uzeeni umri ukiwa umeenda zaidi, husababisha watu wengi kusumbuliwa na tatizo la msongo wa mawazo kama wataweza kunufaika na mafao ya uzeeni wakiwa bado wapo hai au wakiwa bado na nguvu na afya njema au mafao yao watafaidi watu wengine wao wakiwa tayari wamechoka sana na uzee au pengine wamefariki.

Kulinda afya za watumishi na kuwezesha wastaafu kufurahia mafao yao wakiwa na afya njema:
Kutokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha uliopo sasa, watu wengi sana kuanzia umri wa miaka 50 wanakabiliwa na hatari ya kupata magonjwa yasiyo ya kuambukiza na wengine tayari wana magonjwa hayo.
Hivyo kuendelea na utaratibu wa umri wa lazima wa kustaafu kuwa miaka 60 ni kuendelea kuhatarisha maisha ya watumishi hasa wenye umri mkubwa na kupunguza ufanisi wa kazi kutokana na changamoto ya maradhi. Magonjwa kama vile kisukari, shinikizo la damu, kupooza viungo vya mwili na magonjwa ya moyo yamekuwa ni tatizo kubwa hasa kwa watu kuanzia umri wa miaka 50.

Kupunguza umri wa kustaafu kutatoa fursa kwa watumishi wenye magonjwa hayo kupata mda mwingi wa kupumzika na kufuatilia matibabu au kujiuguza kwa usahihi zaidi, kwa sababu magonjwa hayo yanahitaji ufuatiliaji wa karibu zaidi wa matibabu na huduma nyingine za afya. Lakini pia itasaidia ikiwa watastaafu mapema, kutumia mafao yao katika malengo yao waliyo nayo badala ya kutumia mafao yao kujiuguza na maradhi hasa ya uzeeni.

Kukuza ujuzi na ubunifu, kuongeza ufahamu wa teknolojia na mabadiliko ya kisasa:
Ni ukweli ulio wazi kuwa katika suala la ujuzi na ubunifu, vijana wana uwezo mkubwa zaidi ukilinganisha na wazee.

Wafanyakazi walio katika umri mdogo watakuwa na motisha ya kujifunza na kukuza ujuzi mpya ili kuboresha utendaji wao kazini tofauti na ilivyo kwa wazee. Hii itasaidia taasisi na mashirika kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kuwa na ushindani katika soko.

Lakini pia, vijana ambao wanachukua nafasi za wastaafu wanaweza kuleta ufahamu mpya wa teknolojia na mabadiliko ya kisasa katika soko la ajira. Hii inaweza kusaidia kuboresha utendaji wa shirika au taasisi kwa kuzingatia mwenendo na mahitaji ya sasa ya kiteknolojia.

Kupunguza gharama zisizo za lazima kwa serikali:
Watu wenye umri zaidi ya miaka 55 wapo kwenye hatari ya kusumbuliwa na maradhi ya mara kwa mara, hii inapelekea kushuka kwa ufanisi kazini na kupunguza siku za utendaji kazi kutokana na maradhi, hivyo italazimu mtumishi apewe ruhusu na kujiuguza na kufuatilia matibabu.

Hivyo serikali kuingia hasara ya kuendelea kimlipa mshahara mtumishi ambaye haifanyi kazi kwa kiwango na mda unaotakiwa badala yake mtumishi huyu angestaafu na nafasi yake kuchukuliwa na vijana ambao bado Wana nguvu na afya njema ya kutekeleza majukumu kwa kiwango cha juu zaidi.

Fursa ya kujihusisha na shughuli mpya au biashara:
Kustaafu mapema inaweza kumwezesha mtumishi wa umma kujihusisha na shughuli mpya au hata kuanzisha biashara yao wenyewe. Wanaweza kutumia ujuzi na uzoefu wao kutengeneza njia mpya za kujipatia kipato au kuchangia katika jamii kwa njia mpya.
 
Upvote 16
Ni ukweli usiopingika kuwa ufanisi wa utendaji kazi wa mtu unapungua kadri umri unavyozidi kwenda, mtu mwenye umri zaidi ya miaka 55 utendaji kazi wake hauwezi kulinganisha na kijana. Hivyo, kumuacha kazini mtu mwenye umri zaidi ya miaka 55
Hili linahitaji utafiti. Kwani umechukuloa vigezo vyote ikiwamo ufanisi unaoogezeka kutokana na uzoefu wa kuwepo kazini muda mrefu?

Kuwapa wastaafu muda mrefu zaidi wa kupumzika na kufaidi mafao yao:
Kulingana na takwimu za mwaka 2022, wastani wa umri wa kuishi kwa mtanzania ni miaka 65, kwa maana hiyo
Bahati mbaya tafiti mbalimbali pia zimependekeza umri bora wa kustaafu ni miaka HAUPO!, umependekeza watu wafanye kazi hadi watakapochooooooka kabisa ndio wakufe tu.

Yaani ingewezekana kiwa na ofisi zinazosapoti wazee na ikawa na tija kwa wote tungewatumia hawa watu hadi wanadanja.

Pamoja na pointi nyingine mfano badala ya msongo wa mawazo kutokana na kuzidiwa kazi, wengi hupatwa na msongo kwa kuishiwa kazi. Kwa kweli tunahitaji kufanya utafiti zaidi ili kulenga penye uwiano stahiki kati ya kazi na mapumziko, ajira na kustaaafu.
 
Utangulizi.
Kutokana na taratibu na kanuni zilizopo kwa sasa, umri wa kustaafu kwa lazima katika sekta mbalimbali za ajira hapa nchini ni miaka 60.

Kupunguza umri wa kustaafu kwa lazima kutoka miaka 60 hadi 55 ni suala lenye faida kubwa kwa pande mbalimbali.

Mabadiliko haya yatajikita katika lengo la kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kwa kuzingatia mahitaji ya sasa na matarajio ya baadaye.

Kwa kuzingatia mazingira ya sasa, idadi ya watu inazidi kuongezeka kwa kasi kubwa na pia changamoto za kiafya zinazowakabili watu wengi hasa katika umri wa kuanzia miaka 50, kupunguza umri wa kustaafu kwa lazima kutaweka msingi imara kwa ustawi wa wastaafu, kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na kuongeza nafasi za ajira.

Sababu na faida za kuzingatia mabadiliko haya ni kama ifuatavyo:

Kuongeza nafasi za ajira kwa vijana na kuchochea mzunguko wa ajira:

Kutokana na changamoto iliyopo ya ukosefu wa ajira ambayo inatokana na ongezeko la wasomi nchini, kupunguza umri wa kustaafu kwa lazima kutawapa fursa zaidi vijana ambao wanatafuta ajira katika sekta mbalimbali. Vijana wanahitaji kuingia katika soko la ajira na kuchangia katika ukuaji wa uchumi, mabadiliko ya utendaji kazi kuwa wa kisasa zaidi hasa katika nyanja ya matumizi ya sayansi na teknolojia na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kutokana na kuwa na nguvu na uwezo wa kutosha wa kukamilisha majukumu ya kikazi pasipo kuchoka mapema wala kusumbuliwa na matatizo ya kiafya ya mara kwa mara. Kwa kuongeza nafasi za ajira kupitia kupunguza umri wa kustaafu, tutaziba pengo la ajira na kuwezesha kizazi kipya kuchukua usukani katika kuleta mabadiliko ya kijamii na kiuchumi.

Kuongeza ufanisi wa utendaji kazi:
Ni ukweli usiopingika kuwa ufanisi wa utendaji kazi wa mtu unapungua kadri umri unavyozidi kwenda, mtu mwenye umri zaidi ya miaka 55 utendaji kazi wake hauwezi kulinganisha na kijana. Hivyo, kumuacha kazini mtu mwenye umri zaidi ya miaka 55 ukizingatia pia mazingira ya kazi hasa ya nchi zetu zinazoendelea kuna hatari kubwa; kwanza, ni kuendelea kumchosha na kumchakaza yeye mwenyewe na pengine kuwa katika hatari ya kupata maradhi hasa yasiyo ya kuambukiza (shinikizo la damu, kupooza viungo vya mwili, msongo wa mawazo n.k), lakini pia kusababisha ufanisi wa utendaji kazi kuwa wa chini zaidi ukilinganisha na utendaji kazi wa mtu wa umri wa chini.

Wakati wastaafu wanapopata fursa ya kupumzika na kufurahia matunda ya kazi yao, wale walio kazini watakuwa na motisha zaidi na uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Kuwa na nguvu kazi yenye nguvu kutaimarisha uzalishaji na kukuza ukuaji wa uchumi.

Kuwapa wastaafu muda mrefu zaidi wa kupumzika na kufaidi mafao yao:
Kulingana na takwimu za mwaka 2022, wastani wa umri wa kuishi kwa mtanzania ni miaka 65, kwa maana hiyo, kwa kuzingatia utaratibu uliopo sasa mstaafu ana wastani wa kuishi ili kufurahia matunda ya kazi yake na kufaidi mafao yake aliyochangia kwa zaidi ya miaka 30 kwa muda wa miaka mitano tu baada ya kustaafu.
Kwa kupunguza umri wa kustaafu, wastaafu watapata muda mrefu zaidi wa kupumzika na kufurahia matunda ya kazi yao na kufaidi mafao yao. Hii itawawezesha kujijengea maisha mapya baada ya kustaafu na kufurahia maisha ya kustaafu kwa amani na utulivu bila msongo wa mawazo na maradhi mbalimbali tofauti na mtu akistaafu umri ukiwa umeenda zaidi.

Kupunguza msongo wa kazi na mawazo kwa watumishi:
Kwa kustaafu mapema, mtumishi wa umma anaweza kupunguza msongo wa kazi na mawazo ambao mara nyingi huja na majukumu ya kazi. Hii inaweza kusaidia kuboresha afya yao ya akili na kimwili na kuwawezesha kufurahia maisha bila shinikizo la kazi.

Lakini pia kutokana na wasiwasi wa watumishi wengi kuhusu afya zao na ikiwa watastaafu na watapata mafao yao ya uzeeni umri ukiwa umeenda zaidi, husababisha watu wengi kusumbuliwa na tatizo la msongo wa mawazo kama wataweza kunufaika na mafao ya uzeeni wakiwa bado wapo hai au wakiwa bado na nguvu na afya njema au mafao yao watafaidi watu wengine wao wakiwa tayari wamechoka sana na uzee au pengine wamefariki.

Kupunguza umri wa kustaafu kutapunguza msongo wa mawazo kwa watumishi. Hii itawawezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kwa furaha, ikijenga mazingira bora ya kazi, pia itawapa fursa ya kufurahia maisha baada ya kustaafu na kutimiza malengo yao ya kibinafsi na kifamilia.

Kulinda afya za watumishi na kuwezesha wastaafu kufurahia mafao yao wakiwa na afya njema:
Kutokana na mabadiliko ya mfumo na mtindo wa maisha uliopo sasa, watu wengi sana kuanzia umri wa miaka 50 wanakabiliwa na hatari ya kupata magonja yasiyo ya kuambukiza na wengine tayari wana magonjwa hayo.
Hivyo kuendelea na utaratibu wa umri wa lazima wa kustaafu kuwa miaka 60 ni kuendelea kuhatarisha maisha ya watumishi hasa wenye umri mkubwa na kupunguza ufanisi wa kazi kutokana na changamoto ya maradhi. Magonjwa kama vile kisukari, shinikizo la damu, kupooza viungo vya mwili na magonjwa ya moyo yamekuwa ni tatizo kubwa hasa kwa watu kuanzia umri wa miaka 50.

Kupunguza umri wa kustaafu kutatoa fursa kwa watumishi wenye magonjwa hayo kupata mda mwingi wa kupumzika na kufuatilia matibabu au kujiuguza kwa usahihi zaidi, kwa sababu magonjwa hayo yanahitaji ufuatiliaji wa karibu zaidi wa matibabu na huduma nyingine za afya. Hii ni tofauti na mtu akiwa bado ni mtumishi wa umma hatopata mda wa kutosha wa kupumzika na kufuatilia matibabu ya mara kwa mara kwa sababu atakuwa akibanwa na majukumu mengi ya kikazi na itamlazimu kuomba ruhusa za mara kwa mara kazini ili aweza kufuatilia matibabu au kujiuguza. Lakini pia itasaidia wastaafu ikiwa watastaafu mapema, kutumia mafao yao katika malengo yao waliyo nayo badala ya kutumia mafao yao kujiuguza na maradhi hasa ya uzeeni. Kupunguza umri wa kustaafu kutawawezesha wastaafu kufurahia mafao yao wakiwa na afya njema.

Kukuza ujuzi na ubunifu, kuongeza ufahamu wa teknolojia na mabadiliko ya kisasa:
Ni ukweli ulio wazi kuwa katika suala la ujuzi na ubunifu, vijana wana uwezo mkubwa zaidi ukilinganisha na wazee.

Kupunguza umri wa kustaafu kunaweza kuchochea ukuaji wa ujuzi na ubunifu kazini kwa sababu vijana watashika majukumu na nyadhifa mbalimbali, hivyo kutumia uwezo wao wa ziada katika kulete mabadiliko ya kimfumo na utendaji kazi.

Wafanyakazi walio katika umri mdogo watakuwa na motisha ya kujifunza na kukuza ujuzi mpya ili kuboresha utendaji wao kazini tofauti na ilivyo kwa wazee. Hii itasaidia taasisi na mashirika kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kuwa na ushindani katika soko.

Lakini pia, vijana ambao wanachukua nafasi za wastaafu wanaweza kuleta ufahamu mpya wa teknolojia na mabadiliko ya kisasa katika soko la ajira. Hii inaweza kusaidia kuboresha utendaji wa shirika au taasisi kwa kuzingatia mwenendo na mahitaji ya sasa ya kiteknolojia.

Kupunguza gharama zisizo za lazima kwa serikali:
Watu wenye umri zaidi ya miaka 55 wapo kwenye hatari ya kusumbuliwa na maradhi ya mara kwa mara, hii inapelekea kushuka kwa ufanisi kazini kutokana na mtumishi kusumbuliwa na maradhi ya mara kwa mara lakini pia kupunguza siku za utendaji kazi kutokana na maradhi, hivyo italazimu mtumishi apewe ruhusu na kujiuguza na kufuatilia matibabu.

Hivyo serikali kuingia hasara ya kuendelea kimlipa mshahara mtumishi ambaye haifanyi kazi kwa kiwanco na mda unaotakiwa badala yake mtumishi huyu angestaafu na nafasi yake kuchukuliwa na vijana ambao bado Wana nguvu na afya njema ya kutekeleza majukumu kwa kiwango cha juu zaidi.

Kuimarisha utawala bora na uongozi: Kustaafu mapema kunaweza kusaidia kuleta mabadiliko katika utawala na uongozi wa umma. Kwa kuwa na kizazi kipya cha viongozi na watumishi wa umma, serikali inaweza kuimarisha utawala bora na kuleta mabadiliko chanya katika utekelezaji wa sera na miradi ya maendeleo.

Fursa ya kujihusisha na shughuli mpya au biashara:
Kustaafu mapema inaweza kumwezesha mtumishi wa umma kujihusisha na shughuli mpya au hata kuanzisha biashara yao wenyewe. Wanaweza kutumia ujuzi na uzoefu wao kutengeneza njia mpya za kujipatia kipato au kuchangia katika jamii kwa njia mpya.

Hitimisho
Kwa kuzingatia faida hizi, ni wakati wa serikali na wadau wengine kufikiria kwa uzito juu ya kupunguza umri wa lazima wa kustaafu. Kwa kufanya hivyo, tutaweka misingi imara ya ustawi wa jamii na ukuaji wa uchumi kwa vizazi vijavyo.
 
Kuongeza ufanisi katika utendaji kazi, yaani umeona fresh graduate ni sawa na mzee aliyekaa ofisini miaka 20 ??? kabisaa??

Kupunguza gharama kwa serikali pia haiko sawa, waki staafu mapema means kunakuwa na pool kubwa ya wastaafu ambao watajitaji kipindi kirefu cha kulipwa pension, huoni mzigo unarudi kwa serikali?? nimekupa vote though...
 
Mfumo wa ajira za umma kwa baadhi ya kada unapaswa kufanyiwa marekebisho. Mathalan, kada za afya na nyinginezo zenye ujuzi wa kipekee ndio ziwe unastaafu ukiwa na miaka 55 ua 60 na hata 70 kwa specialists. Ila hizi taaluma nyinginezo ajira ziwe za mikataba ya miaka 5 au 10 then utendaji na manufaa yako yapimwe ndipo uongezewe makataba au mkataba kukoma.
 
Ajira za mkataba zitaongeza vipi ajira?
 
Ajira za mkataba zitaongeza vipi ajira?
Ukijua kuwa baada ya miaka 10 mkataba utaisha utajiandaa kujenga mtaji wako na kujiajiri au pia kuajiri wengine baada ya mkataba wako kuisha. Tofauti na ilivyo sasa ukiwa na miaka 60 una nguvu na kimwili wa akili za kuanza miradi enedelevu.

Lakini baada ya Mkataba kuisha unatoa nafasi kwa waajiriwa wapya kuajiriwa.

Lakini ajira ya Mkataba inamfanya mtu kufanya kwa weledi na bidii kwani unajua baada ya 5 au 10 yrs kuna tathmini.
 
Ufanisi vs Umri.

Namcheki mzee Perez anavyochapa kazi pale Madrid.

Sisi tunaonekana kuzeeka mapema na kupoteza nguvu sababu ya mfumo wetu wa maisha unaotuzeesha mapema kabla ya umri kuwa mkubwa sana.
 
Ukijua kuwa baada ya miaka 10 mkataba utaisha utajiandaa kujenga mtaji wako na kujiajiri au pia kuajiri wengine baada ya mkataba wako kuisha. Tofauti na ilivyo sasa ukiwa na miaka 60 una nguvu na kimwili wa akili za kuanza miradi enedelevu.

Lakini ajira ya Mkataba inamfanya mtu kufanya kwa weledi na bidii kwani unajua baada ya 5 au 10 yrs kuna tathmini.
mnh, kwa rate zipi za mshahara? wangapi wanafanya kazi ili tu wale na hawana savings...tena wengine wamefanya kazi maisha yao yote??...

Ajira za mkataba hazisaidii kupunguza tatizo la ajira... unamtoa mtu mmoja ofisini unaweka mmoja halafu unasema umepunguza tatizo la ajira nchini??
 
".....kupunguza umri wa kustaafu kwa lazima kutaweka msingi imara kwa ustawi wa wastaafu, kuongeza ufanisi katika utendaji kazi......." Wewe unafikiria kwenye angle moja tu ya kuongeza ajira. Pamoja na kupinga uwezekano wa aliyefanya kazi kwa 10yrs kuweza kuajiajiri na kuunda ajira mpya, mimi ninasisitiza kwamba kuna uwezekano mkubwa kuliko mtu aliyestaafu akiwa na miaka 60.
 
Haya mkuu...kuna nchi zenye hizo kazi za mikataba???...wananchi wamejiajiri???
 
Kuongeza ufanisi katika utendaji kazi, yaani umeona fresh graduate ni sawa na mzee aliyekaa ofisini miaka 20 ??? kabisaa??

Kupunguza gharama kwa serikali pia haiko sawa, waki staafu mapema means kunakuwa na pool kubwa ya wastaafu ambao watajitaji kipindi kirefu cha kulipwa pension, huoni mzigo unarudi kwa serikali?? nimekupa vote though...
Kwanza ukisema Watujishi wenye umri wa miaka 55 wastaafu hiyo mifuko ya kulipa pension itafirisika yote.
Kumbuka serikali ilipokopa fedha kwenye hiyo mifuko hadi leo inajikongoja haina mitaji na hata uwekezaji wao umepungua sana na baadhi ya miradi yao imekaribia kufa hili unaweza liona ukienda Posta mpya majengo mengi ya mifuko hayana wapangaji na ukizingatia wateja wao wakubwa ambao ni Serikali imehamia Dodoma..
 
Tatizo kubwa Tanzania ajira nyingi ni za umma, kwa hiyo watu wakiendelea na ajira kwa muda mrefu huwanyima vijana ajira hizo. Iwapo kungekuwa na ajira nyingi sana, basi experience ingekuwa inaangaliwa sana na hivyo ku-extend retirement age. Hakuna retirement age inayotoshgeleza kwa kila field. Kuna fields ambazo optimal retirement age ni miaka 80 (law) na kuna fields ambazo optimal retirement age ni miaka 34 (athletics) kulingana na nature ya kazi yenyewe.
 
Back
Top Bottom