Kupunguza uzito kwa dawa

Kupunguza uzito kwa dawa

Niliona watu wanafanya mazoezi asubuhi halafu hao wanaenda restaurant kula mapochopocho, nikacheka sana maana mule kulikuwa na vibonge na havipungui...cha kwanza kabisa cha kuzingatia unakula Nini?. Badilisha kwanza namna unavyokula, unaweza punguza kilo nyingi Kwa namna nzuri ya kula tu.
 
Kuna brother angu in town namuita DON, nae amekua akihangaika Sana na madawa ya kupunguza uzito.

Kaenda Hadi Thailand, gym Sana Ila wapi, hana dalili yoyote ya kupungua.

Siku nmempitia kwake tuwai bandarini alfajiri Sana, kaamka na kumwamsha mkewe ampashie kiporo na chai, jamaa kapiga. aisee nikamshangaa sn alfajiri yote na viporo, jamaa akadai ndo kazoea hivo.

Tuko kwny foleni, nikaagiza maji baridi, Jamaa nae kanunua coca-cola ya baridi, kaipiga yote.

Tumefika bandari, mishe zikawa nyingi, Saa 3 asbh akadai njaa inauma sn, tukapate supu, nkamkatalia mpk tumalize mishe mishe Kwanza, saa 5 sio mbali.

Jamaa UZALENDO ukamshinda, kaagiza vitumbua 5 na juice ya bharesa. Kapiga vyote wkt Mi Bado Hata chupa Moja ya maji Lita 1.5 nilonunua kwny foleni sijaimaliza.

Saa 5:30 tushamaliza mishe mishe, saa 6 tuko k'koo OFSIN kwangu, jamaa anaulizia wale wadada wa delivery ya lunch Huwa wanapitisha msosi saa ngapi🤔
 
Vibonge wengi ni misosi bila mazoezi.

Unakunywa supu/mtori heavy na vyapati asubuhi, mchana ule biriani kuku, usiku ule kiepe yai na paja.
Milo yote mitatu unasindikiza na pepsi.
Kazi unayofanya ni isiyokutoa jasho kabisa.
Masokoni humo ndo wamejaa vibonge kwelikweli hasa wauza maduka.
 
Jipangie ratiba ya kula mlo mmoja, milo mingine kula matunda na maji tu.

Ukitakani kulakula kamata tunda hasa apple kula.
 
Habari wakuu naomba ushauli wa kupunguza uzito kwa haraka zaidi naona ninapoelekea sio kuzuri, je nitumie dawa gani maana kwa kufanya mazoezi nitakuwa muongo sina muda huo kabisa

Umri: 25
Uzito wa Sasa: 100 kg
Lengo: Kupunguza kilo 10-15 kwa mwezi mmoja.

Sina unene kupita kiasi, lakini nina mwili mkubwa na kitambi kidogo.
Ninaweza kukimbia na kufanya kila kitu kwa ufasaha kabisa lakini nina minyama nyama kwenye kifua imeshuka ndo kinachonikela zaidi

Nina nia ya kupunguza uzito kwa njia yoyote isio na madhara. Naomba ushauri wenu kuhusu dawa gani nzuri naweza kutumia ikafanikisha lengo langu
Asante
Kilo 10 mpaka 15 kwa mwezi ni kujitafutia matatizo ndugu. Nakushauri:
  1. Tumia zaidi matunda, mbogamboga na protein (nyama, samaki, maharage, njegere)
  2. Kula sio lazima ule mara tatu. Fanya mifungo kama intermittent fasting yaani ukila usiku subiri masaa 16 hadi 18 ndio ule tena. Mfano ukila usiku saa mbili inabidi ule tena kesho saa 6 au saa 8 mchana.
  3. Kula wanga (sukari, wali, ugali, mihogo, nk) kidogo sana na mara moja tu kwa siku.
  4. Acha any processed food/vyakula vya kiwandani kama soda, bia, juisi za kopo nk.
  5. Anza kufanya mazoezi kukimbia ndio rahisi zaidi, unaweza kutembea kwa nusu saa hadi lisali moja kila siku (ukiwa unatoka kazini jioni). Lakini kama kipato kinaruhusu ingia gym. Lifting weights (kupiga chuma) inasaidia zaidi kupunguza uzito kuliko kukimbia.
  6. Mwisho lazima uwe na consistency na hayo vinginevyo utapiga hatua mbili na kurudi kumi.
Ukizingatia hayo miezi sita utajipenda zaidi
 
Niliona watu wanafanya mazoezi asubuhi halafu hao wanaenda restaurant kula mapochopocho, nikacheka sana maana mule kulikuwa na vibonge na havipungui...cha kwanza kabisa cha kuzingatia unakula Nini?. Badilisha kwanza namna unavyokula, unaweza punguza kilo nyingi Kwa namna nzuri ya kula tu.
Sasa ntakula nini jamani
 
Mimi kazi yangu mda wote nimekaa kuanzia saa1 mpaka jioni sinyanyuki ni mikono tuh inayofanya kazi na kichwa
 
Kuna brother angu in town namuita DON, nae amekua akihangaika Sana na madawa ya kupunguza uzito.

Kaenda Hadi Thailand, gym Sana Ila wapi, hana dalili yoyote ya kupungua.

Siku nmempitia kwake tuwai bandarini alfajiri Sana, kaamka na kumwamsha mkewe ampashie kiporo na chai, jamaa kapiga. aisee nikamshangaa sn alfajiri yote na viporo, jamaa akadai ndo kazoea hivo.

Tuko kwny foleni, nikaagiza maji baridi, Jamaa nae kanunua coca-cola ya baridi, kaipiga yote.

Tumefika bandari, mishe zikawa nyingi, Saa 3 asbh akadai njaa inauma sn, tukapate supu, nkamkatalia mpk tumalize mishe mishe Kwanza, saa 5 sio mbali.

Jamaa UZALENDO ukamshinda, kaagiza vitumbua 5 na juice ya bharesa. Kapiga vyote wkt Mi Bado Hata chupa Moja ya maji Lita 1.5 nilonunua kwny foleni sijaimaliza.

Saa 5:30 tushamaliza mishe mishe, saa 6 tuko k'koo OFSIN kwangu, jamaa anaulizia wale wadada wa delivery ya lunch Huwa wanapitisha msosi saa ngapi🤔
Utumbo keshauzoesha hawezi tena kukaa bila kula.
Watu kama hao ndio wale wanoamka usiku wakapasha moto chakula wakala. Hatari sana hio
 
Habari wakuu naomba ushauli wa kupunguza uzito kwa haraka zaidi naona ninapoelekea sio kuzuri, je nitumie dawa gani maana kwa kufanya mazoezi nitakuwa muongo sina muda huo kabisa

Umri: 25
Uzito wa Sasa: 100 kg
Lengo: Kupunguza kilo 10-15 kwa mwezi mmoja.

Sina unene kupita kiasi, lakini nina mwili mkubwa na kitambi kidogo.
Ninaweza kukimbia na kufanya kila kitu kwa ufasaha kabisa lakini nina minyama nyama kwenye kifua imeshuka ndo kinachonikela zaidi

Nina nia ya kupunguza uzito kwa njia yoyote isio na madhara. Naomba ushauri wenu kuhusu dawa gani nzuri naweza kutumia ikafanikisha lengo langu
Asante
Ushauri wangu; usitumie njia za mkato za kupunguza unene kwani zitakuletea matatizo. bali zingatia ratiba ya mlo kwa kufunga au kupunguza kiwango Cha chakula unachokula;

Hali Ipo hivi; Mtu anaponenepa Ina maana mafuta yamezidi mwilini, yanayotokana na kiasi Cha wanga kilichozidi mwilini ambacho huhifadhiwa kwa mfumo wa mafuta.

UNENE; Mtu anapokula chakula hususani vyakula vya wanga, mwili hufyonza na kuingia katika mfumo wa damu ambapo Huwa katika mfumo wanaita ATP (Ndio nguvu ya kufanya kazi), wanga huo ukiwa mwingi hubadilishwa kuwa mafuta ambayo huhifadhiwa maeneo mbali mbali ya mwili

SULUHISHO LA UNENE/UZITO KUPITA KIASI
Kutokana na maelezo hapo juu, kudhibiti mafuta ni rahisi Sana kwa njia zifuatazo;

1. Kufunga; Kufunga ni dawa, kwa nini? kwa sababu mchakato wa kufunga huunguza mafuta mwilini Kwani mafuta Yale yaliyohifadhiwa huchakatwa Tena kuwa ATP (Nguvu ya kufanya kazi), hali hii hupumzisha mfumo wa chakula na kuondoa mafuta maeneo mbali mbali ya mwili.

2. Kupunguza Ulaji; Anza asbuhi yako na kifungua kinywa chepesi, unaweza ukaupitisha mchana bila kula. Ukala jioni pia chakula chepesi na matunda. Nayo hii hupunguza mafuta mwilini. Ukifanya hivyo kuanzia mwezi mmoja na kuendelea uzito wako utapungua taratibu.
 
Nikweli sina muda
Bwana kibonge pole sana mwili unakera mno kwa taarifa zako ni kwamba wewe huli sana wala kufakamia fakamia mamisosi, iko hivi watu wengi wanakimbilia kuchangia pasipo kuangalia sababu moja , kwa maelezo yako wewe una mwili wa asili

Mwili wa asili ni mbaya sana utafanya mazoezi ,utafanya diet ila ukitulia wiki tu huooo ndambi hilooo , kwanza unatakiwa uangalie je una asili ya mwili kama una asili ya mwili piga mazoezi kutia wepesi uwe kibonge mwepesi ila kupungua sahau kabisaa
 
Acha kula vyenye sukari (candy, ice cream n.k), fat (eggs, meat n.k) na wanga nyingi. Do exercise at least x3 a week (you may start little by little) unaweza Fanya kwa dk 10 per day na ukaongeza taratibu Hadi nusu saa kwa siku. Mwisho ila sio kwa umuhimu water fasting, Anza kufunga kula kuanzia asubuhi Hadi saa 7 huku ukiwa na uwezo wa kunywa maji then Kila bàada ya wiki unaongeza saa Moja, mfano kutoka saa 7 Hadi 8 kwa wiki inayofuata Hadi kufikia 12 nakuendelea. Angalizo unapofungua usile chakula kingi sana ni vyema kula matunda na salad zaidi uku ukipunguza vyakula vya wanga kwenye mlo wako.

Hope it will be helpful for many of us.
 
Bwana kibonge pole sana mwili unakera mno kwa taarifa zako ni kwamba wewe huli sana wala kufakamia fakamia mamisosi, iko hivi watu wengi wanakimbilia kuchangia pasipo kuangalia sababu moja , kwa maelezo yako wewe una mwili wa asili

Mwili wa asili ni mbaya sana utafanya mazoezi ,utafanya diet ila ukitulia wiki tu huooo ndambi hilooo , kwanza unatakiwa uangalie je una asili ya mwili kama una asili ya mwili piga mazoezi kutia wepesi uwe kibonge mwepesi ila kupungua sahau kabisaa
Unachosema ndiyo sahihi
Miye ni miongoni mwa watu wenye mwili wa asili ratiba zangu za chakula ni kula jioni tu lakini uzito haupungui, ukipungua labda kg 2.
Kwa sasa nina kg 90 huwa nashangaa kumuona mtu analalamika njaa muda wa saa 6 mchana kwangu naanza kusikia njaa saa 1 jioni
 
Back
Top Bottom