HOJA Kupunguziwa muda wa Visa kwa Mabaharia wa meli za Marekani kumetuathiri Watanzania wengi

HOJA Kupunguziwa muda wa Visa kwa Mabaharia wa meli za Marekani kumetuathiri Watanzania wengi

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Tunaomba mtupazie sauti sisi mabaharia wa meli za Marekani, baada ya Marekani kuweka baadhi ya nchi kwenye orodha ya nchi zilizowekewa vikwazo vya kuingia Marekani (restricted countries), wafanyakazi wa melini tumeathirika sana, na mamia ya Watanzania wamekosa ajira.

Awali, walikuwa wakitupatia visa ya C1/D ya miaka miwili, kwa sababu hii ni visa ya transit na sisi tunapitia majini muda wote, sasa baada ya katazo hilo, Ubalozi unatoa C1/D ya miezi mitatu tu.

Sasa hakuna kampuni inayokubali kutoa ajira ukiwa na C1/D ya miezi mitatu. Nchi nyingine zimefunguliwa, kama Zimbabwe, ambapo serikali yao iliwasaidia mabaharia wao kupata C1/D ya miaka miwili.

Tunaomba Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ndani kutufanyia mpango kwa kuwa wao wana nafasi ya kuzungumza na wanaohusika ili watusaidie, mabaharia C1D kwa miaka miwili tuendelee na kazi za melini.
photo_2026-10-12_11-38-55.jpg

Hii ni mfano wa email ya kujulishwa kukataliwa kuhusu Visa​
 
Back
Top Bottom