Mparee2
JF-Expert Member
- Sep 2, 2012
- 3,092
- 5,386
Leo nimeguswa niandike kidogo kuhusu vipimo
Kuna baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wanapunja watu kwa maksudi kabisa wakiwemo masikini kupitia vipimo mbali mbali kwa;
Wengine hufanya hivyo kwa vipimo mbalimbali vya nafaka, mafuta ya maji nk
Niseme tu kuwa, hakuna mfanyabiashara atatajirika kwa kupunja vipimo na kama wewe ni mmoja wapo; jua tu kuwa, unafanya kosa kubwa sana na kwa mujibu wa maandiko, hutakaa ufanikiwe. Unaweza kushangaa unauza miaka nenda rudi biashara haikui kumbe tatizo ni laana ya kupunja kwenye mizani. Lakini hata kwa elimu ya kawaida ya masoko inakubaliana kuwa, hutakaa utajirike kwani unafukuza wateja
Kama una amini kuwa ipo siku ya mwisho (siku ya hukumu) jua tu kuwa, kupunja kwenye mizani ni sawa na kujipalilia mkaa.
Chukua hatua ya kujirekebisha ukuze biashara yako lakini pia uwe na wakati mzuri siku ya mwisho.

- Kuharibu mizani au yale mawe ya kupimia
- Kubonyeza ndoo au galoni za kupimia mazao
- Kuharibu vipimo vya vimiminika nk