JAYJAY;579380]mara nyingi waandaaji tuzo za muziki au star search wanashawishi wafuatiliaji kupiga kura mara nyingi wawezavyo ,hivi hii ndio namna bora ya kupata washindi,au ndio kibiashara zaidi kutengeneza mshiko.
kwa kweli hii sio njia bora ya kupata washindi kazi ile ni ya kitaaluma hivyo ni vyema majaji wenye ufahamu na muziki ule wakatoa mshindi,ukishirikisha kura kila mmoja ana mapenzi yake lakini kwa kuwa ni biashara lazima wafanye hivyo na ndio maana mwaka jana tukaambiwa misoji ndiye mshindi wakati mtu mwenye uwezo wa kuimba na kupiga gitaa tena kwa nyimbo zake akashindwa hayo ndiyo matatizo ya kupiga kura na hata katika tuzo za kora mambo ni hayo hayo na ndio maaana tuzo za kora haziwezi kuwa na heshima kama zile za american music awards ambazo msingi wake ni mauzo tu.