TUJITEGEMEE
Platinum Member
- Nov 6, 2010
- 27,646
- 28,747
Solution iko kwenye Ibara ya 98 ya Katiba ya JMT, 1977, yaani kupeleka Azimio Bungeni la Kuvunja Muungano! Lazima zipatikane kura theluthi 2 kila upande, otherwise Muungano is here to stay!
Mkuu sasa hivi tunatengeneza mpya ...hiyo ya zamani ni reference tu kwa ajili ya kuendesha mchakato wa kupata mpya...lakini
mleta uzi hajafafanua vizuri...kuhusu kipengele cha serikali mbili...
Kwani unaweza kuwa na serikali mbili zilizo huru, zinz viti huko UN, yaani Serikali ya Zanzibar na serikali Tanzania Bara zilizo huru. Ama serikali mbili kwa muundo wa sasa (Muungano na Zanzibar). Hivyo ningeshauri...poll irudiwe (upigaji kura wa uzi huu urudiwe)...ili options zote mbili ziwe 'captured'. Ni hayo tu.
SERIKALI MOJA TU, na roho yangu itapona....!!!
Sababu ninazo nyingi sana, ila siwezi kuzitoa kwenye hiii JF ya sasa, labda ingekua ya kipinde kile.
Ndoa ni makubaliano ya watu wawili, mmoja asiporidhia ndoa inakuwa haipo hapo. Hilo ndilo jibu la swali lako mkuu.Wazo zuri ila tatizo langu ni kuwa je ikitokea watu wa Zanzibar hawataki muungano hali watu wa Tanganyika wanataka Muungano, ili tatizo litatuliwaje?
Hakuna kura ya maoni zaidi za kuipigia kura rasimu itakayopendekezwa na Bunge la Katiba! Wewe baada ya miaka 50 unaanza kujiuliza kuwa baba uliye naye ni baba yako au la, ya nini kujipa pressure ya bure? Huu Muungano ukivunjika Western Powers hazitakubali "another Somalia!" Waarabu na Al Shabaab/Al Qaeda nao hawatakubali kuona "Makafiri" wakikalia hivyo Visiwa! Don't think kwamba Tanganyika itakuwa salama eti kwa kuwa itakuwa si sehemu ya Zanzibar!
Think BIG brother/sister!
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 inasema kuwa maoni ya kutokuwepo kwa Muungani ni marufuku! Wewe unazungumzia "Nchi Mbili Huru" maana yake hakuna Muungano! Just imagine zile States za Marekani kila State moja iwe na kiti UN ku-represent nchi moja (USA) Sijui kwa nini suala la Muungano linawafanya watu ku-lose focus kiasi hiki!
Na hilo la ku-refer Katiba ya JMT, 1977 ni sawa kwa kuwa ndio inayotumika, au ulitaka nirejee rasimu ya Katiba Mpya? Be serious, plse!
Serikali tatu.zanzibar walishatukataa walishavunja katiba ya muungano.tushilikiane mambo ya muhimu tu ila kila nchi iwe mamlaka yake.jila la nchi yetu libaki Tanzania na sio Tanganyika.
Ndoa ni makubaliano ya watu wawili, mmoja asiporidhia ndoa inakuwa haipo hapo. Hilo ndilo jibu la swali lako mkuu.