Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakuna kura ya maoni zaidi za kuipigia kura rasimu itakayopendekezwa na Bunge la Katiba! Wewe baada ya miaka 50 unaanza kujiuliza kuwa baba uliye naye ni baba yako au la, ya nini kujipa pressure ya bure? Huu Muungano ukivunjika Western Powers hazitakubali "another Somalia!" Waarabu na Al Shabaab/Al Qaeda nao hawatakubali kuona "Makafiri" wakikalia hivyo Visiwa! Don't think kwamba Tanganyika itakuwa salama eti kwa kuwa itakuwa si sehemu ya Zanzibar!
Think BIG brother/sister!
Ongeza namba 5 kwa serikali ya Mkataba.Ongeza mamba 4 kwa wasiotaka muungano.
Serikari Moja tu inatosha Kumbuka Nyerere na Karume waliasisi Muungano wakitarajia Muungano utakuwa ukiboreshwa kulingana na wakati lengo ikiwa ni Kuja Kuwa na Serikari moja tu ambayo ingepunguza wingi wa Marais na makamu wa Marais na Kuwa na Rais Mmoja tu ambaye angehamia Dodoma na kuliepusha jiji na foleni zinazozidi kuongezeka kila kukicha baada ya Serikari kuacha kuhamia Dodoma na kutumia Pesa nyingi kulea na kubembeleza Muungano huku Zanzibar wakitumia Fursa hiyo kujineemesha kirahisi kwa kuzidisha Malalamiko juu ya Kero za muungano zisizokwisha Tambua Zanzibar wapo 1.5 million tu lakini wana idadi kubwa Ya wabunge na viongozi wengi sana wanaofaidi Mavuno ya rasilimali za Tanganyika kisha wanapaza Sauti za kuwapumbaza Watanganyika wasijitambue Kuwa wanachunwa kijanja . Serikari Moja tu Ndio Tiba pekee ya kumaliza mzizi wa Fitna yaani Zanzibar atawale Gavana na huku Bara atawale Gavana kisha Rais awe mmoja tuWanaJF Kwa mda mrefu sasa kuelekea utungaji wa katiba mpya kumekuwa na mjadala mkali kuhusu muungano wetu uwe wa muundo upi sasa ningependekeza tuwe na kura ya maoni hapa JF kuhusu muundo wa muungano, upi ni muundo sahihi?
1.Serikali moja.
2. Serikali mbili.
3.Serikali tatu.
N:B ukiweza kutoa sababu za muundo wa muungano unaoutaka itakuwa vizuri zaidi
mojaa hasa, mbili na tatu ni siasa
Serikali moja ya Tanganyika. Sitaki muungano,kwa nini tunatumia rasilimali nyingi kwa kuungana na kanchi kenye uchumi mdogo kuliko Arusha na ardhi ndogo kuliko Serengeti. Tanganyika hatufaidiki kitu ni bora tuishi kwa ujirani mwema kuliko gharama zisizo na lazma. Yaani hapa tu ndo cmwelewagi Nyerere alikua anawaza nini na huu muungano.
Serikali 2 ndo mpango mzima! Tukiendekeza 3 Serikali ya Muungano itakuwa haina hata ardhi (ardhi si suala la Muungano) na itakuwa ombaomba kwa nchi washirika kwa kuwa haina vyanzo vya mapato vya kwake!