Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
Serikali 3. Uchambuzi wa mzee Warioba unajitosheleza.


WanaJF Kwa mda mrefu sasa kuelekea utungaji wa katiba mpya kumekuwa na mjadala mkali kuhusu muungano wetu uwe wa muundo upi sasa ningependekeza tuwe na kura ya maoni hapa JF kuhusu muundo wa muungano, upi ni muundo sahihi?

1.Serikali moja.
2. Serikali mbili.
3.Serikali tatu.


N:B ukiweza kutoa sababu za muundo wa muungano unaoutaka itakuwa vizuri zaidi
 
Kiuchumi, serikali moja. Ila tukitaka tuwanufaishe wanasiasa basi serikali tatu.
 
Hakuna kura ya maoni zaidi za kuipigia kura rasimu itakayopendekezwa na Bunge la Katiba! Wewe baada ya miaka 50 unaanza kujiuliza kuwa baba uliye naye ni baba yako au la, ya nini kujipa pressure ya bure? Huu Muungano ukivunjika Western Powers hazitakubali "another Somalia!" Waarabu na Al Shabaab/Al Qaeda nao hawatakubali kuona "Makafiri" wakikalia hivyo Visiwa! Don't think kwamba Tanganyika itakuwa salama eti kwa kuwa itakuwa si sehemu ya Zanzibar!
Think BIG brother/sister!

Hao western power wakisema ijitenge watajitenga.
Huyo shabibi hahusu
Wamipewa base tu visiwani wanabadilisha uzi
Hizo za alshabab ni kwaya za kanisa tushazizoea.
Unayo zungumza ni kuonesha udini ndio unao wanana zanzibar.wameungana na watu wanao wwchukia waislam.
Ni kosa kubwa sana la karume.
Kwa sasa huu mungano watu wa tanganyika hasa wakristo wanavifanya visiwa vile kama karume ali wauzia.
Wameweka puppets na wamawalinda.
Lakini haki hapokwi maisha always kuna way out
 
Serikali tatu NDIYO kitu halisi mengine ni kudanganyana tu.
 
Bila woga... Serikali Moja ndio suluhu la kero zote! Ipigwe kura ya maoni kuhusu hili; Aidha serikali moja au kila mtu lwake! Uchaguzi huu ndio utakaoweka wazi iwapo waTanzania (Bara na visiwani) wanataka muungano au la! haya ya kuogopana ndio maana watu wanakuaja na viraka vya serikali 2. Kwa maoni yangu Serikali 3 ni muendelezo wa tabia yetu ya kuoneana "muhali" /"haya". ta bia hii imekuwa kichaka cha kuficha wachache wenye ajenda zao binafsi! Kiwekwe wazi tujue kama tunasuka au kunyoa.
Bora kumeza mfupa mara moja kuliko kuendeleza maumivu kwa kuoneana aibu!
 
Tatizo la CCM wanasahasu kwamba wao ni chama kongwe. Badala ya kujenga hoja ni kwanini wanataka serikali mbili wao wanasema Mwl Nyerere alisema ni serikali mbili! Huwetuzi kubadili aya za bible au korani lkn sio mawazo ya binadamu ambaye likelihood ya kukosea ni kubwa. Ndio maana kuna editions za vitabu. Baada ya muda fulani mawazo fulani yanapitwa na wakati na wanadamu wa wakati huo wanalekebisha na kusonga mbele. Ni lazima tujadiliane kama taifa kuhusu muundo wa muungano wetu na tukiona mawazo ya waasisi hayaendi na wakati wa sasa ni lazima kama taifa tutafute njia sahihi inayoendana na matakwa ya wakati huu. Njia yenyewe ni serikali tatu.
 
Serikali tatu
1.ya zanzibar 2.muungano
3.Tanganyika
hii ni kutokana na utofauti wa zanzibar na bara zenji wapo kama nchi kabisa coz wana rais, bendera,wimbo wao wa taifa. Bara rais ndiye wa kote, wimbo ndo wa kote, bendera ndo ya kote. 2ache kupigana changa la macho
 
Serikali tatu hazikwepeki kero za mungano zimeshinda kutatuliwa kwa miaka 50 sasa,tatazo tanganyika imevaa koti la mungano na kuonekana mungano unafaida kwa tanganyika tu, ukichukulia bunge la mungano wabunge wa zanzibar hawana kazi shuhuli zote zinahusu tanganyika ila wasuburi mpaka bajeti kwa wizara nne za mungano wakimaliza hapo hawana kazi tena mpaka bajeyi ijayo.na wala kamati za bunge haziendi zanzibar kukagua miradi ya kimaendeleo.hata TFF ni mungano lakini inafanya kazi za tanganyika tu,serikali inaomba misaada inatumika tanganyika ,na hailaumiki tanganyika kwa hilo ila mfumo wa mungano inalazimika kuwa hivyo sasa muda umefika wa serikali tatu
 
Kiuchumi, serikali moja. Ila tukitaka tuwanufaishe wanasiasa basi serikali tatu.

sawa kabisa kuna baadhi ya vyama vinaona Serikali tatu ndo mkombozi kwao kwa sababu vinakubalika sehemu moja tu ya muungano (Tanganyika/Zanziba) wao waaona dawa ni Serikali tatu pia kuna vinapendekeza serikali mbili kwa kuhofia tu kuimarika. baadhi ya vyama na hivyo kuupungunza nguvu
Serikali moja yatosha
 
umekaririshwa na pinda??? mbona mh Warioba alishajibu hoja zote?


Kwahiyo akijibu Warioba ndo TZ? tupo 45 million je mawazo yetu yabebwe na mtu mmoja?

unatumia nini kufikiri? ulipata ngapi matokeo ya juzi?
 
WanaJF Kwa mda mrefu sasa kuelekea utungaji wa katiba mpya kumekuwa na mjadala mkali kuhusu muungano wetu uwe wa muundo upi sasa ningependekeza tuwe na kura ya maoni hapa JF kuhusu muundo wa muungano, upi ni muundo sahihi?

1.Serikali moja.
2. Serikali mbili.
3.Serikali tatu.


N:B ukiweza kutoa sababu za muundo wa muungano unaoutaka itakuwa vizuri zaidi

Napendekeza serikali mbili na Muungano usiwepo. Wao na serikali yao na sisi na serikali yetu. Tuwe majirani tu kama tulivyo na Kenya au Malawi.
 
Hakuna kura ya maoni zaidi za kuipigia kura rasimu itakayopendekezwa na Bunge la Katiba! Wewe baada ya miaka 50 unaanza kujiuliza kuwa baba uliye naye ni baba yako au la, ya nini kujipa pressure ya bure? Huu Muungano ukivunjika Western Powers hazitakubali "another Somalia!" Waarabu na Al Shabaab/Al Qaeda nao hawatakubali kuona "Makafiri" wakikalia hivyo Visiwa! Don't think kwamba Tanganyika itakuwa salama eti kwa kuwa itakuwa si sehemu ya Zanzibar!
Think BIG brother/sister!
eti wewe ndio Lusinde
?
 
Binafsi ningependa iwe serikari ya mfumo mmoja kwani sabab ni kwamb nchi yetu ndo inaendelea hivyo basi kutakua na msongamano wa viongoz kibao wa pande zote mbili na kufanya mikopo kuwa mingi kwa ajiri ya kulipa viongozi tu.
 
Serikali Moja ndo komesha upuuzi! Mzanzibar akileta za kuleta mnamhamisha anakuja kupewa ardhi ya bure huku kwetu Katavi! Halafu JK akubali kumwachia umwinyi Sheni! Mnasemaje?
 
serikali 1.zanzibar iwe mkoa tu au wilaya.nchi gani ina idadi ya wakazi sawa na jimbo la ubungo?
 
Serikari moja Ndio Njia pekee ya kupunguza Gharama na Misafara ya Viongozi kwani Rais atakuwa Mmoja tu kule Zenji atasimikwa Gavana Pia Tanganyika atakuwepo Gavana hii itakuwa Serikari moja Bora isiyotumia Mamilioni ya Pesa kuulea na kuubembeleza Muungano Kama ambavyo ilivyo sasa Pesa Nyingi inapelekwa Wizara ya Muungano ili itumike kutatua kero za Muungano lakini inaliwa bure kisha kero zinaendelea Kama kawaida suluhisho pekee ni Kuwa na serikari moja tu
 
Kumbuka Leo Hawa wanaomba 3 kesho akija mwingine ataomba serikari za kanda ya ziwa, kusini, kasikazini, mashariki nk yaani kutakuwa na Maserikari kibao Kama utitiri ktk Nchi masikini ya kujitakia kwani Ina Rasilimali nyingi lakini imeshindwa kubuni namna ya kujikwamua na Kuwa Nchi Tajiri Kama South Africa
 
Back
Top Bottom