ili kujua muundo gani ni sahihi turudi kwenye asili ya muungano huu tulionao.
Muungano huu umepatikana kwa kuunganisha nchi mbili:
- Jamhuri ya watu Zanzibar
- Jamhuri ya Tanganyika
kabla ya tarehe 26 April 1964 kulikua na serikali Mbili nazo ni :
- Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
- Serikali ya Tanganyika
na baada ya tarahe 26 April 1964 Takawa na Nchi mbili( kwa mujibu wa katiba zote za znz na Muungano)nazo ni
- Zanzibar
- Tanzania
ukiangalia kwa makini utaona Tanganyika ni kama imebadilsha jina na kuwa Tanzania.lakini baada ya muungano nchi zimebaki mbili na serikali mbili.
kili chobadilika ni Serikali ya Tanzania kuchukua baadhi ya mambo ya upande wa zanzibar kuwa chini ya himaya yake,mfano :
- anga
- mambo ya nje
- mambo ya ndani
- elimu ya juu
- ulinzi
- posta nk
mambo mengine yaliyobaki bado yapo ndani ya serikali ya mapinduzi:
- kilimo
- uvuvi
- maji
- barabara
- umeme
- michezo n.k
ukiangalia kwa makini utaona muundo huu kuhalisia hakuna muungano....kwani serikali zimebaki mbili na ile ya mapinduzi ipo pale pale.Tanganyika wao wamebadili jina na kujinyakulia mambo fulani ya zanzibar.
hapa hakuna muungano kuna kubabaisha...
nchi mbili zikiungana kunakua na mambo mawili yanatokea:
- zinaungana nchi na serikali zao na kufanya serikali na nchi moja tu yaani union au muungano.
- au zinaungana na kutengeneza federation system of goverment , hapa kunakuwa na
- Serikali kuu itayo simamia mambo mnayo kubaliana
- kunakua na serikali za state zinazofanya federation.
serikali kuu inakua na turufu juu ya mambo ya states.
kwa vile inaonekana zanzibar ni wazi haako tayari kupoteza utaifa wao basi option iliyopo ni kufanya federation.
kila state itasimamia shughuli zake za uchumi...kutkana na vyanzo visivyo ndani ya federal control
mjii mkuu wa federation unaweza kuwa ni Dar es salaam au Zanziabr. Na mjii mkuu wa Tanganyika ukawa Dodoma.