Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Serekali tatu sio mbaya kama rasimu ya pili ya katiba ilivyo pendekeza. Ila hofu ni uhuru unaodaiwa na wabia wa muungano yaani Zanzibar . Ukiwa na serikali tatu zenye mamlaka hakuna namna muungano utakavyo pona. Kwa maoni yangu kama serikali tatu zikikubalika ni lazima tuwe na Rais mmoja tu wa jamhuri ya muungano na hizi serikali mbili yaani ya Tanganyika na Zanzibar ziongozwe na Mawaziri viongozi na mamlaka ya Dola yabaki mikononi wa Rais wa jamhuri.
Serikali iwe moja ambayo itaongozwa na Rais mmoja then kuwepo na waziri mkuu wa Zanzibar na Tanganyika hapo mambo yataenda sawa lakini eti maraisi watatu mmmmhhh hapana kwakweli
Na ndivyo itakavyokuwa.
Serekali tatu sio mbaya kama rasimu ya pili ya katiba ilivyo pendekeza. Ila hofu ni uhuru unaodaiwa na wabia wa muungano yaani Zanzibar . Ukiwa na serikali tatu zenye mamlaka hakuna namna muungano utakavyo pona. Kwa maoni yangu kama serikali tatu zikikubalika ni lazima tuwe na Rais mmoja tu wa jamhuri ya muungano na hizi serikali mbili yaani ya Tanganyika na Zanzibar ziongozwe na Mawaziri viongozi na mamlaka ya Dola yabaki mikononi wa Rais wa jamhuri.
Watanzania kama tunataka muungano wetu uwe mzuri ni kuwa na serikali moja tu, katiba ya Zanzibar na Tanganyika ziwekwe kwenye droo na uwepo mkoa wa zanzibar na Pemba na hii mikoa ya bara watakuwepo magavana,Rais wa Tanzania akitoka bara makamu wake awe zanzibar kama Rais ni mzanzibar makamu ni mbara. Hapo ndiyo tutakuwa na muungano imara.
wanajf kwa mda mrefu sasa kuelekea utungaji wa katiba mpya kumekuwa na mjadala mkali kuhusu muungano wetu uwe wa muundo upi sasa ningependekeza tuwe na kura ya maoni hapa jf kuhusu muundo wa muungano, upi ni muundo sahihi?
1.serikali moja.
2. Serikali mbili.
3.serikali tatu.
N:b ukiweza kutoa sababu za muundo wa muungano unaoutaka itakuwa vizuri zaidi
CCM wanasema serilaki ziwe mbili, lakini mambo ya muungano na ya bara yatenganishwe kwenye bunge, baraza la mawaziri nk...
Swali langu kwenu CCM lina vipengele a, b, na c kama ifuatavyo...
a. Ni nani atakuwa mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa Tanzania bara? Kama ni raisi wa muungano, Je, ikiwa anatokea bara hakutakuwa na conflict of interest atakapokuwa anasimamia mambo ya muungano? Na kama anatokea Zanzibar, je, kunatakuwa na uhalali aongoze baraza la mawaziri wa muungano?
b. Ni nani atateua mawaziri wa Tanzania bara? Kama ni raisi wa muungano, rejeeni sehemu ya pili na tatu ya kipengele a hapo juu
c. Ni nani atakuwa kiongozi wa shughuli za serikali kwenye bunge la Tanzania bara? Kama ni waziri mkuu, itakuwaje kama Waziri mkuu anatokea Zanzibar?
Maswali kama hayo pia yatahusiana na uteuzi wa maofisa mbalimbali wanaohusika na Tanzania bara...
CC Ritz, chama, MwanaDiwani, lusungo, Nape Nnauye, Mwigulu Nchemba et al...
Huu muungano ni matatizo matupu hauendani na karne 21; serikali 2 sio suluhisho; Tanganyika tulishakubali kupoteza identity yetu kama Zanzibar hawataki kupoteza identity yao huu muungano na uwe basi hatuna sababu hata moja ya kuubembeleza muungano ambao haunà tija kwa wananchi wa kawaida; suluhisho ni serikali mmoja tu kama wanataka na iwe hivyo hawataki basi!
Mkuu Tuko, umeisha wahi sikia viongozi/wabunge wa magamba wakijenga hoja yenye mashiko popote!? Wenyewe hua ni watu wa mazoea tu, maadamu hiki kitu kiko hivi tokea miaka hiyo na basi tuendelee hivyo hivyo tu! Hayo maswali ukikutana na akina Nape pamoja na wote ulio wa copy hapo hawatakujibu na watakwambia kua hakika una point yenye mashiko but wakiwa kwenye public, utasikia wanaongea vitu visivyo na maana yoyote ile.
Wewe unaona mbili na huo muungano wa serikal tatu umewahi kuuona wap?